Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Watu tushaswitch-on zamaaaaaaaaaaaaani,nyie endeleeni kupigwa tu,hata waziri mkuu alishasema mpigwe tu,so vodacom wapo sawa wanaendeleza kaulimbiu ya waziri mkuu,na mimi nasema pigweni tuuu
 
Mimi nawashukuru tu mods maana skuhz hawafuti threads zinazowalenga voda kama zamani. Vodacom ni tatizo kwa wengi
 
Ni kweli kazi ni kwako...! Kubaki au kuondoka! Mm ni mteja wao wa miaka mingi sana tangia vodacom inaingia nchini ila kwa sasa nimewahama hasa jwebye data receiving natumia sana mtandao wa tigo au Airtel ni nafuu na sio wezi km vodacom...vodacom ni wezu balaa! Wanakuibia mteja mchana kweupeee...hawafai hawa jamaa.mkuu hama mapema watakufilisi hawa...

internet ikifika 7 mchana paka 4 usiku ipo very slow au haipo kabsa
 
Vodacom imekua ya kihindi kuliko hata Airtel ya wahindi. juzi niliweka vocha ya alfu kucheki salio nakuta kuna mia mbili tu.

Wew ni kosa lako pengine ulijisahau kuzima mobile data lakin pamoja na hayo voda nimeshaanza kuwahama taratibu maana wanatuona sis mazuzu. Hasa kwenye hiyo MPESA yao.
 
Mitandao ipo mingi,njia pekee ni kuhamia kwenye unafuu,ndio faida ya soko huru
 
Tigo ndo habari ya mjini wanapigaga hadi simu kukuuliza ubora wa huduma zao na kama una maoni juu huduma zao!! Wananipigiaga binfsi cjui mitandao mingine vp!!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
Mi sihami wala nini ngoja nikomoane nao hadi nione mwisho wake.
 
Voda ni najisi,joka limezalo watanzania,Fedha za damu,mie na familia yangu tunahama,bora tig0,.
Hii naiweka insyagram na fb watu tuhame
 
Mkuu unaweza ukawa uko sawa, lakini maoni yangu si lazima yafanane na watumiaji walio wengi.. nina laini 3za na 1 ya airtel, 1 ya tigo, familia yangu yote ni voda lakini bado naona voda wako juu kwa huduma zao.. nazungumzia clarity na internet speed.. kuhusu bei za kuongea wako sawa na mitandao mingine ya airtel na tgo mfano... voda 20,000 kwa mwzi ni DK 375, na Airtel ni DK 375, na tigo ni hivo hivo.........ila wanaweza imarisha ushindani wao kwenye bei... suala la kuwa kata kwenye kila kona sio haki.. kwenye internet wako comparatively Very fast...

huwezi kugundua matatizo ya voda kama ww ni wa kuweka vifurushi vya mwezi.. tuongelee wale watumiaji wa gharama za chini(kuanzia 500)...
sina utaalam sana na tigo lakini at least sasa hivi nimetumia airtel kwa mwezi tangu nimeiweka hii voda hewani tu bila kuongeza vocha ili marafiki zangu wasinikose hewani wakt nawajuza taratibu namba zangu mpya ya airtel..

iko hivi.. airtel wameboresha huduma zao za vocha( mjini tunaiita mmasai) ipo ya 500 na ya 600, kwa 500 unapata dk 15 kupiga mitandao yote, MB125 na sms 300, hii kitu haipo voda..

voda kwa 500 unapata dk 20 voda - voda( kitu ambacho me huwa kinaniboa sana kwa sababu watumiaji tuna wateja wa mitandao mingine, so uwanja wa uhuru unakuwa mdogo) sms 100 na MB 100, HAPA WAMEPIGWA BAO..
 
Mi am willing kuhama ata now lkn sema uku nlipo mimi wao tu ndo wananipa internet ya 3G na H+ km cvyo long tym sn ningekua pengine… hawana uzalendo

usijali huduma zikiboreshwa huko ulipo utajiunga nasi tu..
 
huwezi kugundua matatizo ya voda kama ww ni wa kuweka vifurushi vya mwezi.. tuongelee wale watumiaji wa gharama za chini(kuanzia 500)...
sina utaalam sana na tigo lakini at least sasa hivi nimetumia airtel kwa mwezi tangu nimeiweka hii voda hewani tu bila kuongeza vocha ili marafiki zangu wasinikose hewani wakt nawajuza taratibu namba zangu mpya ya airtel..

iko hivi.. airtel wameboresha huduma zao za vocha( mjini tunaiita mmasai) ipo ya 500 na ya 600, kwa 500 unapata dk 15 kupiga mitandao yote, MB125 na sms 300, hii kitu haipo voda..

voda kwa 500 unapata dk 20 voda - voda( kitu ambacho me huwa kinaniboa sana kwa sababu watumiaji tuna wateja wa mitandao mingine, so uwanja wa uhuru unakuwa mdogo) sms 100 na MB 100, HAPA WAMEPIGWA BAO..

mi nahama leo rasmi
 
Mie nna sehem nafanyia uwakala mpesa na juzi kati nilifanya muamala wa kumnunulia mteja LUKU kwa gharama ya sh 10,000 na mwingine Azam tv kwa sh 12,500 na nikaomba wanisitishie muamala coz wateja hao wote walikuwa account zao hazikuwa active kuweka hela. Cha kushangza hadi leo sijarudishiwa hela yangu na bado kuna commission kiduchu za kila mwezi tofauti na Airtel na Tigo. Mwaka huu watajibeba mbona..ntawahama soon.
 
chelewa chelewa tu.. wanatufanya sisi maboya..
 
niliwahi kusikia tetesi kua kuna viongozi wa twawala wana hisa humo voda sasa isije ikawa wanatimiza ilani yao maana nimeliwa nilikopa 900 sasa wakati wa kulipa ikawa kila nikiweka vocha ya buku inakatwa hadi ikafika 5000 wanakula tu nilipowapigia wakazingua sina hamu

Wanachezea sana Servers zao za billing - najua watakuwa Waswahili wanao fanya ujaja huo, Raia wa Mataifa mengine wana mahadili mema - Waswahili tulio wengi ni wezi by default, wanachukulia ignorance ya walio wengi kwa kuwaibia bila huruma, mambo yao hayako transparent hata kidogo! Unambiwa Internet bila kikomo kwa masaa 24 hawasemi bila kikomo wana maana gani?

Wanaweka mitego kwenye DB software zao kukata hela bila idhini yako, kinacho angaliwa ni balance hiko kiasi gani - ukiweka command moja ina-append mambo mengine kwenye background bila ya wewe kujua kinacho endelea na hela inakatwa, wanalazimisha kuweka nyimbo, habari za mipira, kukupigia simu za matangazo bila ya wewe ku-subscribe. Sijui jeuri hii wanaipata wapi? Sasa hivi wameingiza modem za ovyo kweli kweli wanashindwa na Kampuni ndogo ya Sasatel - yaani inaoneka modem hizo zimeingizwa sokoni haraka haraka bila ya kuangalia wenzao software za modem zao zimekaa kivipi, za wenzao ni nzuri sana - kampuni ya ZTE haiwezi kushindana na Huawei, yaani jeuri ya kuwa na wateja wengi unawafanya wajione wanaweza kufanya lolote bila ya kuwa challeged na Dora au wateja.

Siku zinavyo kwenda naona wateja wengi watawakimbia au watabaki ni SIM Card zao kwa kupokelea simu basi, wanahudhi sana.
 
Back
Top Bottom