Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni kweli kazi ni kwako...! Kubaki au kuondoka! Mm ni mteja wao wa miaka mingi sana tangia vodacom inaingia nchini ila kwa sasa nimewahama hasa jwebye data receiving natumia sana mtandao wa tigo au Airtel ni nafuu na sio wezi km vodacom...vodacom ni wezu balaa! Wanakuibia mteja mchana kweupeee...hawafai hawa jamaa.mkuu hama mapema watakufilisi hawa...
Vodacom imekua ya kihindi kuliko hata Airtel ya wahindi. juzi niliweka vocha ya alfu kucheki salio nakuta kuna mia mbili tu.
Mi sihami wala nini ngoja nikomoane nao hadi nione mwisho wake.
Mkuu unaweza ukawa uko sawa, lakini maoni yangu si lazima yafanane na watumiaji walio wengi.. nina laini 3za na 1 ya airtel, 1 ya tigo, familia yangu yote ni voda lakini bado naona voda wako juu kwa huduma zao.. nazungumzia clarity na internet speed.. kuhusu bei za kuongea wako sawa na mitandao mingine ya airtel na tgo mfano... voda 20,000 kwa mwzi ni DK 375, na Airtel ni DK 375, na tigo ni hivo hivo.........ila wanaweza imarisha ushindani wao kwenye bei... suala la kuwa kata kwenye kila kona sio haki.. kwenye internet wako comparatively Very fast...
Mi am willing kuhama ata now lkn sema uku nlipo mimi wao tu ndo wananipa internet ya 3G na H+ km cvyo long tym sn ningekua pengine hawana uzalendo
huwezi kugundua matatizo ya voda kama ww ni wa kuweka vifurushi vya mwezi.. tuongelee wale watumiaji wa gharama za chini(kuanzia 500)...
sina utaalam sana na tigo lakini at least sasa hivi nimetumia airtel kwa mwezi tangu nimeiweka hii voda hewani tu bila kuongeza vocha ili marafiki zangu wasinikose hewani wakt nawajuza taratibu namba zangu mpya ya airtel..
iko hivi.. airtel wameboresha huduma zao za vocha( mjini tunaiita mmasai) ipo ya 500 na ya 600, kwa 500 unapata dk 15 kupiga mitandao yote, MB125 na sms 300, hii kitu haipo voda..
voda kwa 500 unapata dk 20 voda - voda( kitu ambacho me huwa kinaniboa sana kwa sababu watumiaji tuna wateja wa mitandao mingine, so uwanja wa uhuru unakuwa mdogo) sms 100 na MB 100, HAPA WAMEPIGWA BAO..
Mie nna sehem nafanyia uwakala mpesa na juzi kati nilifanya muamala wa kumnunulia mteja LUKU kwa gharama ya sh 10,000 na mwingine Azam tv kwa sh 12,500 na nikaomba wanisitishie muamala coz wateja hao wote walikuwa account zao hazikuwa active kuweka hela. Cha kushangza hadi leo sijarudishiwa hela yangu na bado kuna commission kiduchu za kila mwezi tofauti na Airtel na Tigo. Mwaka huu watajibeba mbona..ntawahama soon.
niliwahi kusikia tetesi kua kuna viongozi wa twawala wana hisa humo voda sasa isije ikawa wanatimiza ilani yao maana nimeliwa nilikopa 900 sasa wakati wa kulipa ikawa kila nikiweka vocha ya buku inakatwa hadi ikafika 5000 wanakula tu nilipowapigia wakazingua sina hamu