Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

sio voda tu mume wangu ametumia tigo line long time kama sio 6/7 years juzi imeanza kupoteza network mara haisomi
kwenda tigo shop wanasema sio line yake akawauliza ya nani wakasema ni ya mtu anaitwa ELIZABE
akawatupia line yao akaondoka akahamia kwingine
hawa voda ,tigo ,zantel na airtel hawajui kuwa kuna
viettel na Smart wamekuja wameshajiona sana subirini
Yaani ilichoandika ni copy & paste ya kilichompata shemeji yangu. Laini ya tigo kaitumia zaidi ya miaka 6, then tigo wakamsajilia namba hiyo hiyo mtu mwingine.

Ikawa ukipiga hiyo namba mara anapokea shemeji yangu, mara anapokea huyo mwingine. Ikawa inaleta utata sana. Hawa ni wa kuwapeleka mahakamani tu, hakuna jinsi.
 
Kuna tatzo jingine zaid hata ya hili. wafanyakazi wa customer care nao ni janga. Unaripoti tatizo lakini jibu utakalopewa hata mtu wa mtaani hatoi jibu kama hilo

Kabisa mkuu. kama hapa katikati ya nchi ni shida tupu si wao tu hata walinzi wao wa mlangoni nao ni taabu ukimkuta kashika kirungu chake hapo mlango utafikiri anamtafuta muuza madawa ya kulevya, utasikia kaa pembeni, unataka nini? huwa nabaki najiuliza hawa jamaa walipata darasa kabla ya kuanza kazi? au. Kwa kweli Voda bado saana
 
...asante kwa mrejesho, namba hii bado tunaitumia na ipo kwenye taarifa zetu nyeti na muhimu, mara ya mwisho ametumiwa fedha kiasi cha Tzs 150,000/= na huyo mteja wenu kaulizwa wewe ni fulani akakubali wakati anajua si yeye. so akatuibia fedha hiyo, nitawasilisha malalamiko yangu kwa maandishi TCRA....
Gefu katika usajili namba hiyo ni ya mteja mwingine kwa sasa, hamuitumii bali ipo katika nyaraka zenu, ingekuwa vyema kama kijana wako angewafahamisha watu aliokuwa anawasiliana nao kuwa kwa sasa hatumii tena namba hiyo nanyi mna jukumu la kubadilisha(update) namba katika taarifa zenu muhimu na nyeti ili kuepuka na hasara inayoweza kujitokeza.
 
Last edited by a moderator:
Voda mmezidi nimewahi kuweka salio 500 naunga bundle wananiambia sina salio la kutosha na wala aikuwa nimekopa arrrrghhh
 
Habari bahati, tumekutumia PM kwa msaada zaidi. Ahsante

Mi mwenyewe nina summons yenu nataka niwaletee niwaburuze mahakama ya mwanzo ya kimbiji maaana mnanisababishia usumbufu usio wa lazima mara kwa mara na mimeseji yenu ya promosheni
 
Last edited by a moderator:
Voda mmezidi nimewahi kuweka salio 500 naunga bundle wananiambia sina salio la kutosha na wala aikuwa nimekopa arrrrghhh

Wezi kweli hawa ni wa kupeleka mahakamani tu..kutwa wanazubgusha makalio kule kwenye chipsi karibu na Mlimani tower badala ya kufanya kazi
 
Wadau wa Jf na watumiaji wa vodacom kama mimi yaani kwa slogan ya kazi ni kwako, hatuna budi kujibeba sasa hivi. Kifupi ni hivi, Niliona humu kuna baadhi ya wana jamii wenzangu wakilalamika kuhusu hawa jamaa ni wezi nami nikasema nitakomaa nao hadi mwisho.

Lakini hapana naomba niishie katikati najitoa nimeshindwa mimi, haiwezekani vifurushi vibadilishwe bila sisi watumiaji kupewa Taarifa. Eti mia 4 dk15 buku dk50 na hiyo ni kupiga voda-voda?
 
Ni majanga tupu, nimeunganisha cheka ya wiki ya Tsh 2800 hata sikupewa sekunde moja ya kupiga mitandao yote, nikaamua kuunga tena ya mitandao yote Tsh 399 nimeongea sek 6 kimeisha!

Hvi vodacom wanakusanya kwa wizi zile 9b za donation za afya walizoahidi?, ama kuna hasara walipata? Karibu 40% ya watz hawajui kusoma wala kuandika, je, huwa wanachukua hatua gani endapo hujuma hizi zikiwapata?! Asante vodacom kwa miaka yote mi 7 tuliokuwa wote pamoja!
 
Up to now you it use vodacom ? You am not know Tigo or Airtel. Why it waste time with useless network Voda ? Me it not break break voda line only. it break break and burn and flash the ashes in toilet.
Voda is much uselessful. I am recommend Tigo for you.
 
Sijaelewa kabisa hii lugha ya malkia
 
Ushauri wako ni mzuri mkuu, japo ungerekebisha uandishi wako wa kingereza ingeleta mantiki nzuri zaidi! Embu jaribu kuweka mpangilio wa kisarufi! Ama una lengo la kutuondoa kwenye mada, kama sivyo uweke vizuri ndugu
Up to now you it use vodacom ? You am not know Tigo or Airtel. Why it waste time with useless network Voda ? Me it not break break voda line only. it break break and burn and flash the ashes in toilet.
Voda is much uselessful. I am recommend Tigo for you.
 
Up to now you it use vodacom ? You am not know Tigo or Airtel. Why it waste time with useless network Voda ? Me it not break break voda line only. it break break and burn and flash the ashes in toilet.
Voda is much uselessful. I am recommend Tigo for you.

People they dont no everyday of god vodacom they say"ze job is urself"foristance wat do they mean?they mean use it on ur own risk.!!finish.
 
Up to now you it use vodacom ? You am not know Tigo or Airtel. Why it waste time with useless network Voda ? Me it not break break voda line only. it break break and burn and flash the ashes in toilet.
Voda is much uselessful. I am recommend Tigo for you.

Teeeh teeeeh kaz ipoooo......kiingereza n lugha ya watu jaman chetu n kiswahil
 
Back
Top Bottom