Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Kwa wanaotumia windows phone
------------------------------
1. Manual Guide
2. Select "Settings" > "access point" > "add" > "Connection name"
3. Enter Tigo WAP
4. Select "Access point name"
5. Enter tigowap
6. Select "Proxy address / WAP gateway (URL)"
7. Enter 10.168.20.80
8. Select "Proxy port"
9. Enter 8080
10. Select "ok"
11. Enter Tigo WAP
 
Mimi nilikuwa na no ya voda nikaa kwa muda bila kuitumia. Nikajaribu hivi juzi nikakuta wameshaifunga na wamempa mtu mwingine nikawamaindi wakasema ukikaa zaidi ya miezi 3 wanaifunga, kwa vile nilikuwa nahitaji nikanunu nyingi. Hii ndio ilikuwa majanga kabisa ilikuwa ya mtu mwingine full usumbufu kupigiwa na watu msg za ajabu. Voda mjicheki bana
Habari Kitotoro, ni kweli kwamba laini ikikaa zaidi ya siku 90 bila kutumika inafutwa, kilichotokea kwenye laini mpya ni kwamba wale ndugu, jamaa na marafiki wa mteja wa awali bado wanadhani ndugu/rafiki yao anatumia namba hiyo. Pole sana kwa usumbufu uliojitokeza.
 
Unastahili tuzo ya uvumilivu kwa kuendelea kuwa na hao jamaa.
 
Hiyo kero mi nilishakutana nayo.
Nilikasirika sana wakati haya mambo yanatokea.
Nadhani TCRA inabidi waingilie kati hili suala.
 
Last edited by a moderator:
Habari Kitotoro, ni kweli kwamba laini ikikaa zaidi ya siku 90 bila kutumika inafutwa, kilichotokea kwenye laini mpya ni kwamba wale ndugu, jamaa na marafiki wa mteja wa awali bado wanadhani ndugu/rafiki yao anatumia namba hiyo. Pole sana kwa usumbufu uliojitokeza.


Kwahiyo Vodacom mnaona fahari sana kuyumbisha ndoa za watu. Mimi nilikutana na the same instance, nimekwenda ku-renew line nikapewa line iliyokuwa inatumiwa na mtu mwingine, nikawa napigiwa simu usiku wa manane na wanawake nisiowajua na kila nilipowaambia siwafahamu nilipokea matusi, meseji zisizo na staha kiasi cha kuiyumbisha sana ndoa yangu, hatimaye nikanyosha mikono, maswahibu niliyokutana nayo yamenifanya niwachukie milele, kwanza hapa ninaghadhabu sana nanyi.
 
  • Ndio
  • VPN hata katika simu waweza kutumia
  • Mfano fungua hizi site NETFLIX, VEVO , utaona kwamba hutoweza kuzitumia
  • Ila ukitumia VPN utachagua server mfano ya USA hivyo utaweza kuzitembelea na kuangalia videos kama kawaida
  • SEma OS ya simu yako ili nikupe mapendekezo ya VPN nzuli.:cool2:
Mkuu,naomba hiyo VPN, natumia android 4.4.4
 
Mkuu,naomba hiyo VPN, natumia android 4.4.4
GOCoXJw_DpAfnbIxMlLKI33hipQQJH2y0RtOymwhB1wGE8x4QY5sOIuSFuwxjBVNMy0=h310-rw

Karibu
 
Vodacom mnakera,sasa maji yametufika shingoni wateja wenu,hausshi mwezi bila Mpesa kusumbua..

Tangu asubuhi leo mpesa haipatikani,hamuonei huruma wateja wenu,hamuoni aibu wapinzani wenu.?
IMG_20140814_112124.png
 
Mitandao iko mingi kwa nini maung'ang'ania huo mtandao mbovu?
 
Mtandao wa Vodacom una haja ya kufahamu kuwa Watanzania sio wale wa miaka ya Tisini! Mambo yamebadilika kama kuibiwa kwa ujanja ujanja tuliibiwa sana!

Vodacom wana boa sana kwa sasa ukiweka air time inaisha ghafla hata iwe 10,000 kwa dakika 5!

Lakini Vodacom pia wana toa kifurushi kwa kujiunga vifurushi hivyo kwa siku hadi mwezi,sasa ya siku wametoka dakika 25 Mpaka 18 kwenda mitandao mingine ambapo ni shida sanaa nayo ukiongea dakika 2 unaletewa sms kuwa Kifurushi kina isha ghafla! Vodacom ipo kisiasa sana yani ni Shidaaa
 
Nilisha sahau mtandao unaitwa Vodacom niwababaishaji sana sana! Tatizo watanzania hatujui haki zetu! Achaneni na mitandao ya hovyo hiyo itawapa adabu wata jiregebisha
 
Nilisha sahau mtandao unaitwa Vodacom niwababaishaji sana sana! Tatizo watanzania hatujui haki zetu! Achaneni na mitandao ya hovyo hiyo itawapa adabu wata jiregebisha
Kwa hiyo tutumie mtandao upi? Yote naona ni majanga tu
 
mitandao yote ina kero za msimu. Leo voda baada ya muda watahamia tigo mara airtel.
 
Back
Top Bottom