Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Habari
zamda tunapenda kukutoa wasiwasi kuwa hakuna
pesa inayopotea kupitia M-PESA. Tafadhali tutumie namba ya simu PM
ukitufahamisha kutoka NMB uliufanya lini.

nilihamisha kuja mpesa ili kulipia zuku,sikulipa zuku na hela ilikuwepo mpaka ilivyoyeyuka juzi.
 
Last edited by a moderator:
Habari
zamda tunapenda kukutoa wasiwasi kuwa hakuna
pesa inayopotea kupitia M-PESA. Tafadhali tutumie namba ya simu PM
ukitufahamisha kutoka NMB uliufanya lini.

Nimesha PM namba yangu..sijui nimepatia sio mtaalam sana.
 
Last edited by a moderator:
Afadhali Vodacom mmeamua kuja na huku ili tuwe tunapeana makavu.Kuwazowea kwetu mtulipe huduma maridhawa!
 
TAHADHARI KWA WATEJA WA VODACOM TANZANIA

Kuna Ujumbe unaosambaa unaofanana na hivi

Vodacom Center precissionsprings@gmail.com
31 Aug (5 days ago)
Dear Vodacom Customer,
We noticed some problem login in your Vodacom account and need to be fixed within 12 hours To avoid clossing your account.-
Please Click Here For quick verification.

Thanks & Regards,
Vodacom.co.za
Customer Team

Huu Ujumbe ni wa kitapeli

Ukimpa huyo jamaa taarifa zako atakuwa na uwezo wa kuingia kwenye akaunti yako kwa njia ya mtandao kwa nia ya kufanya uhalifu haswa wa kuhamisha fedha .
 
Kama unaelewa mambo ya kimtandao waweza ona kabisa hiyo meseji ilivyojaa utapeli...

Check the email address, then kwa wateja wa Vodacom Tanzania huwa hakuna mambo ya akaunti za wateja...
 
Naona voda hata taarifa hawatoi sijui wanasubiria kupokea malalamiko kwanza
 
Naona voda hata taarifa hawatoi sijui wanasubiria kupokea malalamiko kwanza
Usikute wenyewe ndo wachoraji wa utapeli. Si unajua mwarabu kauza shares zake, sasa hivi ni kutafuta mapato kwa lazima. Unaweka alfumkumi unapiga simu moja ya dk 2 unaambiwa pesa imeisha
 
Ndugu mteja kuna barua pepe inasambaa inayohitaji utume taarifa zako za siri za Tigo Pesa.Tafadhali usijibu ombi hilo wala kutoa taarifa zako.TigoPesa!
 
TCRA shughulikieni hii as soon as possible

TCRA wanazurura tu kwenye vituo vya television eti wanatoa elimu ya matumizi ya mtandao wakati kigogo mkubwa wa chama chetu anamiliki mtandao unaoitwa Tanzania nchi yetu site. Unapost ishu za ngono kila siku hawachukuliwi hatua licha ya kuripotiwa
 
Back
Top Bottom