Naomba kusema hii tabia ni ya KIPUMBAVU, kuweka vocha then inayeyuka bila matumizi, WIZI uliokithiri.
Ni takribani wiki mbili sasa nimekuwa nikinunua muda wa maongezi katika simu, nimeweka 'vocha' ya elfu tano, zaidi ya mara nane, hii ikiwa kila vocha ninaitumia ndani ya siku mbili hadi tatu, Tena hapa kila siku mtu unajiunga kwa vifurushi vya kila siku vya CHEKA.(Intaneti, muda wa maongezi na ujumbe mfupi wa maneno).
Tatizo hili lilishawahi kunitokea hapo kipindi cha nyuma na baada ya mzozo mrefu HQ Mlimani City walirudiaha vocha ya 20,000/= .Sasa hii tabia imejirudia, Acheni usanii wa kuomba namba za simu hapa na kisha kutofanya marekebisho.
Kitu kibaya ni kuwa nimekwisha tupa karatasi(vocha hizo nikizozitumia) lakini kama mkihitaji namba nitawatumia. Hii tabia inakera, mtu unaweka vocha pengine unakwenda sehemu isiyo na huduma kwa uharaka then unakuja kudhtuka eti hua salio na unakuta hujafanya matumizi yeyote tena hapa umejiunfa kwa vifurushi vyenu. Ninaomba kusema acheni UPUMBAVU huu na jirekebisheni.