Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Hello Vodacom Tanzania. Mbona siku hizi nikiuliza balance airtime napewa kwa dakika tu bila sekunde? Mmerudisha utaratibu wa zamani kukata kwa dakika? Kwa mfano "Balance for Cheka Tsh499 is 4 min all net,292 SMS and 1MB. To be used by 2014-09-26 19:56:45.Get up to 90 min with Cheka Zogo.Dial*149*01#
 
Last edited by a moderator:
Vodacom Tanzania naomba nijue ni akina nani ambao namba zao zimefutwa na still hela ipo maana tuna ndugu ambao hatujui kama wana line ya voda je zile zinazobaki hua zinapelekwa wapi BAK
 
Last edited by a moderator:
Upande wa university promo mnapitwa na mitandao mingine Kama Airtel na tigo. Wameeeka hadi bando la wiki kwa gharama nafuu.. Jiongezeni ili tuhamie voda
 
Mi Binafsi Voda wananifurahisha sana. Kwanza kabisa wametoa fursa ya vijana kujiajiri kwa M pesa.
Lakin Jambo kubwa zaidi la kusikitisha wamewapa matapeli ulaji. Mfano ni Mim Binafsi niliomba uwakala toka mwaka Jana mwezi wa kumi na Moja mpaka leo ni nimeambulia patupu. Baada ya kufatilia kwa ukaribu nikagundua line (Till) yangu. Nilishindwa kushangaa!!! Nikawaeleza kwanin m2 atumie till kwa jina langu na document zangu kwa mwaka mzima. Na mim nimekaa mwaka mzima nyumbani sina Kazi. .Sasa wameniambia nikafanye SWAP Ngoja nione watachukua Muda Gan. Kwa hali hiyo voda Waliangalie kwa jicho la 3.
 
Voda wahuni hata nami hapa moro wameuza line yangu ya uwakala kwa wqtu wengine
 
Mkuu Shark ni aje? Sijaelewa kwenye hili swali lako zuri, ID yangu inaingiaje?

Vodacom Tanzania naomba nijue ni akina nani ambao namba zao zimefutwa na still hela ipo maana tuna ndugu ambao hatujui kama wana line ya voda je zile zinazobaki hua zinapelekwa wapi BAK
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Shark ni aje? Sijaelewa kwenye hili swali lako zuri, ID yangu inaingiaje?

ok mkuu ni kwa kuheshimu uchambuzi wako makini katika mada tofauti je hizi hela zinazopatikana wakati namba za watu wanapofariki na wana m pesa hua zinaelekea wapi
 
Last edited by a moderator:
Tanzania haina usalama katika maeneo mengi, nchi si shwari

Wizi, wa pesa za wateja



  1. [*=center]benk, mikopo mingi wizi mtupu, ATM, Masalio benk(akiba zetu0 hayako salama

    [*=center]kampuni za simu
    [*=center]rushwa ndogondogo
    [*=center]kodi katika bidhaa
    [*=center]kutokula milo salama
    [*=center]afya za wananchi dawa gharama

    [*=center]siku hizi hata haja ndogo gharama
kweli mnyime elimu umuone/oppress, walimu wanayeyushwa maslah duni kwa sabb wakiwezeshwa elimu itapaa na wanafunzi, wahitimu watakuwa hatari kwa tabaka tawala...mnalikjua hilo?
 
@Vodacom Tanzani hivi hakuna njia nyingine mbadala tofauti na kupiga simu kama nataka kurudisha pesa nilioituma kimakosa kwa mpesa?
 
Ukiweka Salio ukataka kujiunga kifurushi unaambiwa salio halitoshi,ukiangalia Salio unakuta bado linatosha.Unaamua kuchagua kifurushi cha bei ya chini unaweka kifurushi inakubali,,lkn ukiangalia salio unakuta bado lipo ukikaa baada ya muda unakuta limepotea.
Hawa jamaa wanakata kushinda hata lile tozo la mwezi lililolalamikiwa kipindi kile bungeni.Hapa nasubiri kurenew laini yangu ya mtandao mwingine
 
Kwanza habari za kazi kwenu nyote mnao husika?
Pili niende kwa linalo nisibu haijalishi mtanisaidia ama mtapotezea,mhimu kwangu mlitambue. Mnapo anzisha huduma zenye kulenga kumsaidia mteja kweli mlenge ktk hilo,siyo mnaanzisha ktk mfumo huo kumbe mpo ktk mfumo wa ninyi kujiingizia kipato{mauzo} kwa kiwango cha juu. Hapa naomba nigusie mfumo wenu wa cheka na hasa hii cheka bombastick na hasa inayo husu mitandao yote. Nimekuwa mhanga wa hili kwa kipindi kirefu sana. Imani kwamba dk.zote ninazo nunua ninazitumia haipo tena hapa kuna usanii flani unafanyika na mbaya zaidi ni kama umenunua kifurushi cha wiki au mwezi hapo sahau kufika nacho mwisho.Na kwa kuthibitisha hilo nimejaribu kununua kifurushi cha aina hiyo kwa mtandao mwingine na kingine chenye thamani kubwa tena kimoja kwa ajili ya off net & on net na kingine kwa ajili ya on net tu kwa upande wenu bado hivi vya kwenu vimeisha haraka ilihali kile cha mtandao pinzani mpaka leo natumia. Hebu jitathiminini kwa hili.
Lakini pia mna ugonjwa wa mtu kupiga simu kama ana kifurushi na kika isha ndani ya maongezi kama ana salio mstoe taarifa na wakati mwingine hata akipiga simu nyingine na pale salio liishapo tu ndiyo mnatuma taarifa ya kuisha kwa kifurushi. Maana yake nikanunue vocha nyingine. Kama hiyo ndiyo ilikuwa budget yangu ya vocha kwa siku,wiki ama mwezi! Niende nje ya budget si ndiyo? Na kama niko sehemu ambayo upatikanaji wa vocha ni mgumu? Nikae bila mawasiliano ama niwe nasubiri kupigiwa? Au ndiyo kunipeleka ktk huduma ya kunilazimisha nikope kutoka kwenu ili mtengeneze faida mara mbili kwa kupitia vocha nitakayo inunua kulipa na kunikata zaidi kutokana na mkopo wenu?
Hebu tuchukulieni kama wateja wenye kustahil huduma bora na siyo manyanyaso kwamba wamesha ingia wataenda wapi?
Ni hayo tu mnaweza kufanyia kazi ama kupotezea kama ikionekana hayana mashiko kwenu!
 
na mbona napata shida nikiwa huku Uganda napata network ya MTN lakini siwezi pata hudumma ya vodacom menue nataka kununua salio toka kwene m-pesa yangu na kila nikijaribu 0752-898906 *150*00# inajibu REQUEST NOT COMPLETE" AMA MENUE IMEBADILIKA KWA MTU ALIYE NJE YA NCHI?
sasa kweli mnategemea nifanye nini???????????
i need reliable service
 
hivi kukopa nipige tafu 400 unarudisha mia 500 ,riba 100, sawa na asilimia 1/4 X 100=25% BOT hawaoni ni wizi?ktk siku moja?Mtu anayekopa a kurudisha kila siku kwa mwezi ni km amekopa kwa riba ya mwezi 25%X30= 750%, kwa mwaka ni utashika kichwa.Pamoja na hizo asilimia bado airtime nayo ni nadra sana ikatumika taratibu.huku ni kufilisi tz. 750%x 12= 9000%, yaani ukikopa 400/= ya voda...kila siku na kurudisha siku hiyohiyo kwa mwaka unarudisha 400+(400x 9000)/100=36,400/= sijui wanaokopa zaidi ya mara moja kwa siku inakuweje?
 
Nimekumbana na tatizo kama hili. Nimefatilia miezi mitatu sasa. Nimeenda Arusha summit, vodashop mlimani city, nikapigiwa simu toka makao makuu kuwa kitambulisho hakionekani vizuri. Nikarudi summit wakatoa photocopy kama wiki tatu zimepita lakini shida ipo palepale

Pole sana, tafadhali tunaomba namba ya simu kwa msaada zaidi.
 
Hello Vodacom Tanzania. Mbona siku hizi nikiuliza balance airtime napewa kwa dakika tu bila sekunde? Mmerudisha utaratibu wa zamani kukata kwa dakika? Kwa mfano "Balance for Cheka Tsh499 is 4 min all net,292 SMS and 1MB. To be used by 2014-09-26 19:56:45.Get up to 90 min with Cheka Zogo.Dial*149*01#
Salama Amante, makato ya vifurushi hajabadilika bado ni kwa sekunde.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom