Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

tuhamie wapi mana nachokiona owners wa hii mitandao wanakaa vikao vya kupanga bei za kuwanyonya watumiaji..thats why ukiangalia tigo mb 500 ni sh. 999 wakati voda mb 500 ni sh. 1000
Kwa nchi za wenzetu makampuni kula njama na kupanga bei ni kosa la jinai lenye adhabu ya kuifuta kampuni zilizohusika. Lakini hapa kwetu sisi ni vichwa vya wendawazimu ambapo baada ya kuwanunua waliopaswa kuisimamia haki wawekezaji wako huru kuwanyonya, kuwaibia na kuwanyanyasa wananchi wapendavyo! TCRA wanahangaika na kazi zisizo zao wala tija kwa watanzania!
 
Vodacom hakuna ofa zinazoeleweka. Nilihama huu mtandao tangu mwaka juzi walipoondoa ile ofa ya kupiga namba moja niliyokuwa natumia kuongea na mpenzi wangu.
Pia hata sasa bado sijashawishika kurudi kutokana na shutuma za kuwaibia wateja salio, kukosa ofa za uhakika na za muda mrefu.
Ishukuruni M-Pesa inafanya laini zenu zinasoma mara chachechache.
Mawasiliano si anasa hata yawekewe gharama kubwa hivyo.
 
Kwa nchi za wenzetu makampuni kula njama na kupanga bei ni kosa la jinai lenye adhabu ya kuifuta kampuni zilizohusika. Lakini hapa kwetu sisi ni vichwa vya wendawazimu ambapo baada ya kuwanunua waliopaswa kuisimamia haki wawekezaji wako huru kuwanyonya, kuwaibia na kuwanyanyasa wananchi wapendavyo! TCRA wanahangaika na kazi zisizo zao wala tija kwa watanzania!
Ata hapa kwetu ni kosa pia..sema Hawa jamaa wanaomiliki mitandao ni magient yaliyoshindikana
 
WALE CUST SERV NI SHULE SHIDA NAOMBA WAHURUMIE..NILIWAHI MKUTA MMOJA WA DIV .....O KWENYE OFISI MMOJA

QUOTE="Lole Gwakisa, post: 8232006, member: 12458"]Kuna wizi mkubwa kwa fedha za salio za wateja unaoendelea sasa hivi katika mtandao wa Vodacom.
Kwa vile hili si jungu bali ukweli nimisha report wizi huo katika kitengo cha malalamiko TCRA kwa hatua zaidi.

Nimeweka salio la Tsha 10,000 mchana wa leo kwa Mpesa ref Y23SY687 na baada ya muda mfupi nikakuta salio langu la maongezi ni sifuri.

Nikanunua vocha na kutumiwa tshs 10,000 na hela yote imekatwa tena.

Wateja wa Vodacom jihadharini, kuna mwizi kaingia mtandaoni Vodacom

UPDATE
=====
VODACOM wamefanya ustaarabu wa kunipigia baada ya kuona detail ya transaction hapo juu, na kuiona kwenye mtandao wa Jamiiforums.
Kimsingi wameapologise kwa mtafaruku uliotokea lakini wamenieleza nifike ofisini kwao kuona aian ya simu ninyotumia isije ikawa data apps ziko wazi.
Na kweli baada ya maongezi ya kuchunguza, mobile data setting ilikuwa ON, na mimeizima sasa.

Hata hivyo ni vema nitaenda kupata maelezo ya kuyeyuka kwa salio langu , karibu 20,000, kwa siku moja.
Wanabodi mtajulishwa inawezekana kuna wenye tatizo kama langu.

UPDATE
=====
Nimeonana na waheshimiwa sana wa Customer Care pale Block 4 Mlimani City.
Cha kusikitisha ni wao kushindwa kuchukua malalamiko yangu na kuyafanyia kazi, na hii ni licha ya kuwaelewesha kuwa hili tukio nalijawahi kunitokea na hii kuwa ni mara ya kwanza.

Hawa jamaa wa Customer Care ni kama mabalozi waliopewa jukumu la kusafisha kampuni ya VODACOM hata kama inanuka kwa wizi uliodhahiri.
Kitu ambacho hawajui ni kuwa nilifanya due diligence kupitia wafanyakazi ndani ya VODACOM walionidhihirishia kuwa kuna wafanyakazi wasio waaminifu ambao wana access na personal security settings za wateja.

Na wafanyakazi hao huwa "wapiga kishenzi" fedha za wateja.

Kwa kifupi mtu wa Customer Care ameshindwa kuniconvince na maelezo yake ya upotevu wa Tshs 20,000 katika mtandao wa VODACOM.[/QUOTE]
 
Habari Vodacom
Nimefika kwenye moja ya ofisi zenu asubuhi ya leo kuomba huduma ya statement ya transactions zangu kwenye account yangu ya M-Pesa, nikaambiwa nipeleke nakala ya kitambulisho na barua ya maelezo kwanini nahitaji statement hiyo, ndipo nitapewa statement kwa gharama ya Tshs 7,000/= kwa statement ya mwezi mmoja.

Nimejiuliza maswali,

  • Kwanini niandike barua ya maelezo kuhusu kuhitaji statement ya fedha zangu mwenyewe?
  • Je kuna siri gani nyuma ya pazia mpaka kuwe na restrictions kiasi hicho?
  • Inakuwaje mnatoza fedha nyingi kiasi hicho kwa ajili ya kupata statement ya mwezi mmoja badala ya kutoza kiasi kinachofanana na benk za kawaida?
  • Kuna haja gani kumtaka mteja akaprinti statement ya fedha yake vodacom na kuwalipa kiasi kikubwa hivyo cha fedha ukizingatia kuwa wapo wananchi wenye kipato cha chini sana ambao hawawezi kumudu kiasi hicho cha gharama za huduma hiyo, na kwa maana hiyo kama kuna wizi unafanywa na kampuni yenu basi wananchi hao hawatajua ni fedha ngapi inapotelea kwenu?
  • Kwanini msiwe na utaratibu wa kuwapa wateja wenu huduma ya kujua mwenendo wa transactions zao kupitia mtandao hata kama mtawatoza kwenye account zao, lakini iwe ni kiasi wanachoweza kumudu?
Utaratibu wenu unatudhoofisha kwa kiasi kikubwa sana wateja wenu, nazishauri mamlaka husika kulitazama hili jambo ili kuwe na transparency, na siyo kuweka conditions ngumu ambazo zinatulazimisha tusifuatilie mwenendo wa flow ya fedha kwenye account zetu za M-Pesa

Mbaya zaidi ukienda kwenye website yenu, mmeyapa kipaumbele kikubwa matangazo kuliko namna rahisi ya wateja wenu kuweza kuwasiliana nanyi (tazama kiambatanisho)

Vodacom

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom