Hivi malalamiko haya yanashughulikiwa na nani? Maana tunatuma kero zetu, hakuna reply yoyote inayojibiwa na wahusika, wala hawajali. Kwa maana hiyo wameshatosheka na kujiona wapo juu sana na kuwa kila mtanzania hana ujanja wa kukwepa huduma zao.
Haya maudhi nimeyashuhudia nilipofanya muamala wa kulipia malipo ya bill ya maji, Idara ya maji mjini Tabora Tuwasa Trh 22/11/2016.
Malipo hayo hayakufika sehemu husika, hali iliyopelekea kampuni kuja kusitisha huduma.
Nilipofuatilia nikaanza kupigwa danadana kwamba pesa ipo hewani! Hewa gani inayomeza pesa za watu?
Pia nikaelezwa kwamba nivumilie na kusubiri masaa 72.
Nikasubiria masaa72 na hakuna marejesho yoyote yaliyofanyika. Nilipo fuatilia tena, nikaelezwa kuwa wamewasiliana na mtu anaeitwa biller wa maxcom ulipokwamia muamala.
Sasa tunaelekea siku ya 10 bila muafaka wowote.
Nabaki kujiuliza, hivi kampuni kubwa kama Voda, yenye watu wenye uweledi mkubwa, yaweza kufanya ujinga huu bila kutanzua tatizo la kawaida la kiufundi siku zote hizo?
Nimekuja kugundua suala hili limekuwa sugu kwenye kampuni hiyo, yaani hivi sasa imekuwa ni kijiwe cha kudanganyia watu. Ukituma pesa, yaweza kukuletea usumbufu sana na bila msaada wowote hasa inapotokea una jambo la dharula kama nililokuwa nalo mie.
Siku niliyopanga kuchukua hatua za kisheria, hapatakuja kuwa na lugha za kitapeli tena za kunituliza kama wanazotumia sasa kunitapelia. Na nitapenda kila mdau wa mawasiliano ya Voda ambaye hajaguswa na kadhia hii, ajiandae kupata suluba ya maudhi kama niliyopata mimi, hata kama hajapatwa, basi aelewe uozo wa miamala ya kifedha unaofanywa na Vodacom hivi sasa, ili aweze kuchukua tahadhari.
Na kwa usumbufu niliopata, katika maisha sitakuja kuthubutu tena kupitishia muamala wangu kwenye kampuni hii ya simu ya kitapeli. Baada ya kumalizana nao sitahitaji kwa njia yoyote ile kutumia huduma za aina yoyote za Vodacom kutokana na uharamia huu wa mawasiliano niliofanyiwa.
Kama habari hii itasomwa na wahusika, waangalie namba hii 0752-914659 kuhakikisha ninayoyasema kabla sijachukua hatua madhubuti ninazozijua mimi.