Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Wadau, hiki kitengo cha Vodacom huduma kwa wateja ([HASHTAG]#100[/HASHTAG]) kinatoa huduma kweli? Nimekuwa nikipiga leo inaita tu wala haipokelewi. Kuna mwenye alternative number? Aisee hawa jamaa kichefu-chefu kuhama tu
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Kitengo chenu cha huduma kwa wateja siku ya terehe 9/3/2017 ilikuwa mbovu kuliko maelezo. [HASHTAG]#100[/HASHTAG] ilikuwa ukipiga inaita tu bila kupokelewa, hii ni mbaya sana. Mfano nilikuwa na tatizo la M-PESA nikashindwa kusaidiwa hakuna mpokea simu. Hadi alfajili ya leo saa 11 nilipojaribu ndio nikafanikiwa. Mkiendelea hivi mnajiweka kwenye hali tata maana kwasasa same namba mitandao yote nothing to worry about.. Mjiongeza!
 
VODA ACHENI UJINGA WA KUNITUMIA MSG ZA PROMOSHENI ZA KUPIGA SIMU INDIA, CHINA AU KOKOTE KULE...SIJAWAHI WAAMBIA KUWA MIMI NINA SHIDA YA KUCHAT AU KUZUNGUMZA NA WATU WA NJE...!! MNANISUMBUA NA MIMESEJI YENU...!!
 
Kwenye MB hamrembi mwandiko aseee.
Ila napenda huduma zenu japo huu ni mwezi wa tano M-PAWA hata mia sikopi wakati vigezo na masharti natimiza kila kukicha ila no worry mnanipa hamasa ya kufanya kazi kwa bidii.

Love VodaCom Tanzania and MTN Uganda
 
Hongereni kwa kuleta kuleta hisa za bei nafuu,hata sisi wenye uchumi wa kawaida tunaweza kumudu.
On my way to buy
 
1.Voda wamekuwa wanatoa gawio kutokana na transaction za Voda
2.Jana wametoa sms kwa wateja wakijulisha kuwa kuna gawio la M pesa lakini shart usajiri ukamilike ndipo mteja husika apate gawio

MASWALI
1.Kwa nini mteja akatwe gharama anapotuma M pesa na Voda wanapokea kwa kutambua hiyo namba lakini namba hiyo hiyo iwe haramu kupokea gawio?

2.Namba nyingi zimesajiriwa na wakala mitaani ambao wana vibali vya voda sasa kama hao hawafikishi taarifa voda nani tapeli?
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania

Nimenunua bundle ya internet ya mwezi Lakini internet haina Kasi kubwa pia nimenunua SMS za mwezi mzima Lakini haziendi nini tatizo??
765200767
 
Mkoa wa simiyu hususani wilaya ya baridi mjini Vodacom netrwok hakuna leo siku ya tatu kuna tatizo gani na maaana hakuna taarifa yeyyote
 
KAMPUNI ya Vodacom Tanzania Limited, hiki mnachokifanya ni wizi na unyang'anyi kama ulivyo ukabaji, kuvunja nyumba ya mtu na kumuibia au kumpora Mali yake kwa nguvu na hata kumjeruhi au kumuua. Kinachotia hasira na hasara zaidi ni kuona TCRA wanajua wizi na utapeli huu lakini wakijifanya kutoona au haiwahusu. Wanashiriki wizi na utapeli huu wa VODACOM. Shame indeed!

Iko hivi, katika huduma zenu za vifurushi mtu ananunua "bundle" la Tsh 1,000.00 mnampa MBs 200 mkiita za saa 24. Kwamba saa 24 zikiisha basi MBs 200 zinakuwa zimeisha. Wizi mnaufanya pale ambapo mteja hakutumia huduma ya internet (data) au katumia kidogo mno. Lkn saa 24 zinapofika tu, tayari mnambania pua, "Ndugu mteja kifurushi chako cha internet kimekwisha, kununua piga *149*03#" Mimi nimeshanunua bidhaa kutoka kwako, Bando ambayo sasa ni Mali yangu halali maana hata risiti umenipa, kwa nini unipangie muda wa kutumia Bando langu? Kwani nikishanunua kifurushi kwenu bado kifurushi hicho ni Mali yenu hadi mnipangie namna ya kuitumia? Huu ni wizi! Msinipangie muda wa kutumia unless ni kifurushi cha bure lkn si niliyonunua kwa hela yangu. Mkome!
[HASHTAG]#UzalendoKwanza[/HASHTAG]!

MY TAKE
Napenyezewa hapa kwamba si Vodacom pekee Bali makampuni karibu yote ya simu yanashiriki ujambazi huu na Rais JPM anatazama tu wanyonge wanavyonyongwa. TCRA mjipime.
 
[emoji38] [emoji23] [emoji23] mwanaume wa chato huyu... siku ya kwanza kununua bando
 
Tatizo wanafanya kazi kwa Mazoea sana..
Yule Mgr wa [HASHTAG]#Moshi[/HASHTAG] mjini anaejiita Mallya ndio alinifanya nihame Voda jumla jumla..
 
KAMPUNI ya Vodacom Tanzania Limited, hiki mnachokifanya ni wizi na unyang'anyi kama ulivyo ukabaji, kuvunja nyumba ya mtu na kumuibia au kumpora Mali yake kwa nguvu na hata kumjeruhi au kumuua. Kinachotia hasira na hasara zaidi ni kuona TCRA wanajua wizi na utapeli huu lakini wakijifanya kutoona au haiwahusu. Wanashiriki wizi na utapeli huu wa VODACOM. Shame indeed!

Iko hivi, katika huduma zenu za vifurushi mtu ananunua "bundle" la Tsh 1,000.00 mnampa MBs 200 mkiita za saa 24. Kwamba saa 24 zikiisha basi MBs 200 zinakuwa zimeisha. Wizi mnaufanya pale ambapo mteja hakutumia huduma ya internet (data) au katumia kidogo mno. Lkn saa 24 zinapofika tu, tayari mnambania pua, "Ndugu mteja kifurushi chako cha internet kimekwisha, kununua piga *149*03#" Mimi nimeshanunua bidhaa kutoka kwako, Bando ambayo sasa ni Mali yangu halali maana hata risiti umenipa, kwa nini unipangie muda wa kutumia Bando langu? Kwani nikishanunua kifurushi kwenu bado kifurushi hicho ni Mali yenu hadi mnipangie namna ya kuitumia? Huu ni wizi! Msinipangie muda wa kutumia unless ni kifurushi cha bure lkn si niliyonunua kwa hela yangu. Mkome!
[HASHTAG]#UzalendoKwanza[/HASHTAG]!

MY TAKE
Napenyezewa hapa kwamba si Vodacom pekee Bali makampuni karibu yote ya simu yanashiriki ujambazi huu na Rais JPM anatazama tu wanyonge wanavyonyongwa. TCRA mjipime.
Kimfano ukahamia tigo kwenye halichachi au Airtel - haupimiwi utajisikiaje? [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Pole inaonekana umeanza kutumia simu juzi juzi uliza majirani basi
 
dah! Leo nimecheka balaa yaani nilijua umeibiwa kweli kumbe ni ushamba tu wa kumiliki simu kwa Mara ya kwanza
.
chamsingi ni kwamba kila kifurushi cha mtandao wowote ule kina expire date and time (ukiacha hivi vipya vya halichachi na hatupimi bando) kama ulikuwa huyajui hayo ndio ujue sasa.
.
karibu kwenye ulimwengu wa teknolojia na digitali
 
Back
Top Bottom