Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Nyie voda kwa nn internet yenu jamani inasumbua haswa kwenye video call na voice call inakatakata tu
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania

Bado ufafanuzi wa serikali kuhusu laini moja ni tata! Kwa nini wanakosa akili ndogo tu ya kuangalia aina za huduma zitolewazo na makampuni haya ya simu ili waweze kutunga vizuri hizo sheria zao za kishamba!

Binafsi ninamiliki laini tatu za mtandao mmoja, na zote zinatumika kwasababu ni huduma halali zinazotolewa na huo mtandao.
1. Laini ya simu kwa maongezi.
2. Laini kwenye modem.
3. Laini kwenye GPS kit ndani ya gari.

Hizi ni huduma zinazotolewa na makampuni yote ya simu na kila mtu ana uhuru wa kuchagua mtandao wake kwa sababu zake na mahitaji yake.

Akili za hawa watu huwa wanazitoa wapi! Vodacom jaribuni basi kuwaelewesha, maana tupo wateja tunaotumia laini zaidi ya moja kutokana huduma mbalimbali mtoazo kama nilivyoanisha!
 
(1) kwa nini mmeacha kutoa gawio la m-pesa?

(2)zaidi ya mara mbili nilijiunga kifurushi cha mb,ya kwako tu,lakini hapohapo nikaambiwa kifurushi kimeisha bila hata kukitumia,kwa nini mnakua wezi kiasi hiki!?

(3)nilikua tabora wiki iliyopita,network ikawa shida(internet),iliporudi kifurushi kikawa kimeisha muda wake,kwa nini hamrudishi mb kiungwana kama wenzenu tigo!?
 
yaani hamjaacha,nimeweka kifurushi mb 100,sijatumia,mnanitumia msg nimebakiza mb 30!!!..nyie wangese nawahama baada ya siku mbili
 
JAMANI, SASAHIVI UKINUNUA BANDO KWA MPESA KAMA PINDUA PINDUA HAIKUBALI..HATA UKINUNUA SALIO KWA MPESA HARAFU UKAIGEUZA KUWA BANDO HAIKUBALI..KWANINI VODA HUDUMA YENU INAKUWA OVYO KIASI HIKI??
 
Mtandao wenu Tangu wiki iliyopita network inakuja na kukata tatizo nini?
Maajabu zaidi unarudi unaambiwa kifurushi kimeisha!

Aiseeee nna mpango nibadilishe laini mambo uakiendelea hivi
 
Mara kwa mara mnanitumia msg kua kiwango cha kukopa m power kimeongezeka ila cha kushangaza nikitaka kukopa mnasema niwasiliane na huduma kwa wateja. Mnazingua sana sitaki tena mi msg yenu hiyo
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Tutalipwa lini gawio la share zetu?
 
1. Mtu unakuta niko na simu nzuri kabisa ya kisasa(samsung/apple n.k) na settings zangu ziko sawa kabisa lakini kumekua na tatizo la internet kiasi mpaka inatia hasira.muda unaonunua kifurushi ndo unakuta muda unanyimwa huduma nzuri,mtandao unakua chini sana na upo town wala si porini kusema kwamba labda hakuna network la hasha.

2. Wateja tunanunua kifurushi na muda unapofika ule ulionunulia kifurushi kama ni 24hrs kifurushi kinaishia hapo hata kama MB bado uko nazo,huu nauita ni wizi mkubwa.kwa nini msiache mpaka MBs ziishe ndipo mtu anunue zingine?na kwa nini msiache mtu anapoingiza muda wa maongezi iwapo kifurushi cha internet kimekwisha ukiweka vocha inaliwa ghafla eti mpaka uzime data.kwa nini msiache muda wa mtu wa maongezi uwepo hewani mpaka tu pale yeye mwenyewe atakapoaamua kununua kifurushi cha internet?kuna aina ya ujanja ujanja m'baya sana mnaufanya.

3. Ninaamini 80% ya wanatumia mtandao wa Vodacom kama isingekua huduma ya m pesa yamkini mngekimbiwa na wateja wengi sana nikiwepo na mimi.
Jaribuni kubadilika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una hoja dhaifu sana!. Kwan si kuna vifurushi visivyoisha muda?. Ni upuuzi ununue kifurushi cha 24 hours halafu utake kidumu miez 3 kwanini usinunue kisichoisha?

Namba 1 sijui huko lkn huku Mbeya mjin at least wanavutia Voda compared to others hivyo tafuta mtandao wenye uafadhar utumie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom