Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Nilikuwa kwenye harakati za kununua salio, sasa badala ya kuandika 3,500 (elfu tatu mia tano) nikaandika 35,000 (elfu thelathini na tano). Na hofu yangu kubwa ni kuwa hii hela italiwa muda wowote....maana yaweza kuwa kifurushi kimeisha wakaanza kukata kwenye salio bila kujua..matokeo yake nitakuja kukuta salio ni sifuri.

Na nina kazi nyingine na hii pesa, siwezi kutumia pesa yote hiyo kwenye simu.
Hapo no way bro..tafuta watu wauzie kwa kuwarushia mkuu
 
ah ah acha kupanick mzee ..watu walinunua kifurushi cha million...nenda *150*01# nenda 11 halafu nenda 7 hapo utazuia bando lisikatwe hata kama internet ipo on..utanunua vufurushi vya 3500 mara 10
Shukran kwa ushauri huu.

Wanasema bora nusu shari kuliko shari kamili ingawa nilihitaji sana pesa yangu irudi nikafanyie mambo mengine.
 
Hii ni kiendacho kwa mchungaji hakirudi.
Ila Wakuu mnaunga mkono lakini huu sio ukatili wa mitandao ya simu?

Hapa lazima tuongee na TCRA, hii ni njia ya kikatili ya kulazimisha Mtu atumie pesa kwenye huduma zao kwa nguvu...walipaswa kuwa na option ya kumrudishia Mtu pesa yake hata kwa kuweka adhabu kidogo....hata wakikata 2000 sio mbaya badala ya kumkwamisha Mtu shughuli zake.

Hivi kwa mfano ndio nipo safarini na hiyo ndio pesa pekee naitegemea kulala gesti, kula na nauli ya basi kwa siku inayofuata?
 
ah ah acha kupanick mzee ..watu walinunua kifurushi cha million...nenda *150*01# nenda 11 halafu nenda 7 hapo utazuia bando lisikatwe hata kama internet ipo on..utanunua vufurushi vya 3500 mara 10
Hii huduma haikubali Mkuu, nimejaribu hamna kitu badala yake inanielekeza jinsi ya kuomba 'nitumie salio kwa M-Pesa'
 
Nimeelekezwa hivyo nikaenda kwa Jamaa wanaouza, wakaniambia wanipe 20,000 kwa salio la 30,000 sasa ni ujinga gani huo? na wanaringa hawakutaka hata ku negotiate.

Walau wangeniambia wakate 2000 au 3000.
Duuh, ndivyo walivyo wajinga hao. Kama hali inaruhusu wanunulie tu hata ndugu zako muda wa maongezi, ni bora kuliko kumpa mtu baki 10000 nzima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila Wakuu mnaunga mkono lakini huu sio ukatili wa mitandao ya simu?

Hapa lazima tuongee na TCRA, hii ni njia ya kikatili ya kulazimisha Mtu atumie pesa kwenye huduma zao kwa nguvu...walipaswa kuwa na option ya kumrudishia Mtu pesa yake hata kwa kuweka adhabu kidogo....hata wakikata 2000 sio mbaya badala ya kumkwamisha Mtu shughuli zake.

Hivi kwa mfano ndio nipo safarini na hiyo ndio pesa pekee naitegemea kulala gesti, kula na nauli ya basi kwa siku inayofuata?
Hatuungi mkono mkuu tunakuambia ukweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Laini yangu ya simu imefungwa leo na tcra
line ilikuwa na shiling 25,000/
kwakuwa line ninaitumia nyumbani kwa shughuli za internet haikuwa imesalijiwa kwa alama za vidole, leo nimefika nafanya usajili mpya ikaja sms kuwa natakiwa kutoa hela za kwenye mpesa ili niweze kufanya usajili mpya,

usajili mpya maana yake niweze kutumia majina yangu na sio yaliyosajiliwa mwanzo kimakosa.
swali langu nitawezaje kutoa hizo hela kama line imefungwa?

nimeenda vodashop nao wanasema hakuna jinsi labda tusubiri taratibu mpya. kwanza walilaumu kwanini nimechelewa usajili, nikawaambia sikuwa na namba ya nida. na nimepta leo.

sina shida na hiyo hela iliyopo kwenye mpesa ila nataka usajili tu. wananiambia niitoe , sasa naitoaje ilhali line imefungiwa?

msaada tafadhali.

nipo mkoani kilimanjaro , vodacom kilimanjaro wameshindwa hata kutoa wazo. na ukipiga simu customer care wanasema nenda vodashop. duh
 
Hii huduma haikubali Mkuu, nimejaribu hamna kitu badala yake inanielekeza jinsi ya kuomba 'nitumie salio kwa M-Pesa'
Sorry nenda *149*01# nenda 11 huduma nyengine halafu nenda 8 matumizi bila bando hapo utazuia bando lisikatwe hata kama internet ipo on..utanunua vufurushi vya 3500 mara 10
 
Nilikuwa kwenye harakati za kununua salio, sasa badala ya kuandika 3,500 (elfu tatu mia tano) nikaandika 35,000 (elfu thelathini na tano). Na hofu yangu kubwa ni kuwa hii hela italiwa muda wowote....maana yaweza kuwa kifurushi kimeisha wakaanza kukata kwenye salio bila kujua..matokeo yake nitakuja kukuta salio ni sifuri.

Na nina kazi nyingine na hii pesa, siwezi kutumia pesa yote hiyo kwenye simu.
Pole
 
Wakuu Habarini
Hivi ni kwangu tu au ni kwa wote!?
Mbona nikiunga bundle la voda linawahi sana kuisha na nikifatilia sioni matumizi yoyote makubwa niliyofanya zaidi ya ku browse tu!?

Mfano hao nimeunga bundle ijuma
Jioni (bundle lile la Uni offer kulingana na mkoa uliopo) nikapewa 800mb
Sija download video yoyote kubwa zaidi ya hizi video clips za whatsap ambazo hazizidi 5MB, wala sija stream Youtube
Lakini nashangaa jioni hii ya jumapili nacheki balance nakuta nimebakia na 150mb

Inawezekana vipi !?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania

Nyie mnaojiita watumishi wa vodacom nashindwa kuelewa hizi mb mnazotoa kwa ajili ya facebook mnamaanisha nn.Sababu ukiangalia mb zenyewe zinatumika kwa speed ya 2G inakuwa haina maana,ni wizi na utapeli tu huo.

Ukiangalia vifurishi vyenu navyo saiv ni wizi wa mchana kweupe,kwa sababu huwezi kunipa kifurushi cha siku halafu ndani ya masaa mawili eti mb zimeisha ma wakati huo labda umeingia google kuangalia rate za dola.Jaribuni kuangalia na kufikiria gharama za maisha ya mnaowahudumia ambao ni wateja wenu.
 
voda mnazingua kinoma,
huduma kwa wateja iko busy
bundle zetu hakuna net
si upuuzi huu!!!!!!!
 
Voda vipi? Network ipo hovyo toka Jana, na mmekili kuwa network mbovu kwa sms mmetutumia.

Kinachonishangaza mnavyokula MB zangu km mazimwi aaahh acheni wizi kweupe.
 
Vodacom majizi wakubwa nyie tunanunua mb halafu network iko low kiasi hicho.

Rudisheni mb zangu majizi wakubwa nyie vinginevyo mseme nivunje hii laini yenu niende kwenye mitandao mingi.

Majizi wakubwa nyinyi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom