Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Vodacom Tanzania: Support thread (Maswali, malalamiko na Ushauri)

Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (M-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)
- Maeneo gani? (Tukifahamu location, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate physical assitance toka kwa vendor wetu aliye karibu nawe)
- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?
- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza
- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.

Karibu

Vodacom Tanzania
Habary..!mie kama mteja ningeomba kipindi hichi wengine tumejifungia!na kupunguza mishe zetu kwa kiasi kikubwa...!maana yake hata vipato vya uhakika hakuna tena!so ombi ni uhitaji wa kupunguziwa angalau baadhi ya vifurushi vya internet..!angalau tutafarijika kua tuko pamoja katika shida na raha.muda wa maongezi sio muhimu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kujua kama tatizo lipo kwangu tu au ni kote..
Toka nimenunua kifurushi masaa manne yamepita, hata signal ya data haionekani..
 
Hii ni tabia yao mpya. Unanunua bundle wao wanalimit usitumie kwa muda. Zikibaki dakika kuanzia 30 za kifurushi kuisha utakutana na speed tuiite 8G kwakuwa wanapima matumizi yako na kujua huwezi kumaliza kifurushi chao.
Dah bas ni washenzi wa tabia..
 
Hii ni tabia yao mpya. Unanunua bundle wao wanalimit usitumie kwa muda. Zikibaki dakika kuanzia 30 za kifurushi kuisha utakutana na speed tuiite 8G kwakuwa wanapima matumizi yako na kujua huwezi kumaliza kifurushi chao.
Hapa nimejaribu kuweka line isiyo na kifurushi naona iko poa tu.. [emoji3]
Kama ni mbinu ya wizi basi wako vizuri..
 
Hapa nimejaribu kuweka line isiyo na kifurushi naona iko poa tu.. [emoji3]
Kama ni mbinu ya wizi basi wako vizuri..

Ndio wizi walioanzisha. Mimi kuna siku niliwapigia kuwauliza mbona line isiyo na kifurushi kwa simu hiihii na setting ileile inafanyakaza wakati line yenye bundle inagoma. Wakajibu line isiyo na bundle haiwez kufungua data.

Nikawaelekeza hata freebasics natumia ambayo ni bure. Yule dada nahisi alikuwa kalewa. Akajibu kuwa hakuna sites unaweza kuingia bila kuwa na MB, nikacheka sana mpka akauliza tatzo. Nikamuuliza '"kwahiyo hata ile fb ya bure wanayotangaza niuongo?"

Akakaa kimya, nikampa dozi yake akaleta porojo za kusubiri saa 24. Nikamuuliza huo muda wote, kifurushi kitahesabiwa ama watastopisha mpka ttzo litatuliwe? Akasema kitahesabiwa muda. Nikaona ujinga huu, nikamwambia najua nn kinaendelea sitaki upuuzi.

Nilimtisha akaaga ila nilipojaribu kuwasha Data kitu kikasoma🤔🤔 Ndio nikagundua shida ni wao. Sasahv kila nikinunua bundle lazima niwachimbe mkwara ndio kifanye kazi. Wanaudhi sana.
 
Naomba kujua kama tatizo lipo kwangu tu au ni kote..
Toka nimenunua kifurushi masaa manne yamepita, hata signal ya data haionekani..

Majambazi hayo..ukinunua kifurushi unaweza shangaa internet inakata tu bila msingi wowote,inakuhangaisha kama masaa mawili ndo inakubali,na muda wa kumalizika kifurushi ukiwa unaelekea mwisho kinakua slow tena bila kujali una hata 2GB kwenye kifurushi chako

Voda ni wezi sana na hii ikiwezekana wanapaswa kuja kubanwa na serikali kama hawawezi waondoke, mtumizi ya mtu wayaache mpaka mtu atakapomaliza kutumia kile alichonunua na si muda wa kununua ulipoanzia ukifika tu kama kesho yake hapo hapi yenyewe yamekata. Majambazi makubwa hayo

JAH Rastafari Morning Africa.Trust JAH respect nature
 
Wapumbafu sana ilinitokea week iiliyoisha.

Sijarudisha laini natumia kwa mambo mengine ila si internet.
 
Muache tabia ya kutuma sms kwangu kuhusu vifurushi vya Dar Uni wakati mie niko Lindi. Mnashindwa kujua hii cm tunayoitumia sms inasomeka mnara wa mikoa gani.

Mjipange vizuri mnapotea kwa uzembe. Kama mnataka wekeni Lindi Uni ili sms zenu zinuhusu na si kunijazia sms kwenye simu bila tija 0744422580

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom