myplusbee,
Sijakimbia mjadala. Nyinyi mmeshasema tukiwa nje ya nchi tunafanya kazi na ni kweli nilikuwa kazini na siko hapa kushinda mitandaoni, tena kwa kujibu hoja dhaifu.
Unapotoa mfano wa mtu mmojammoja kama ile unaokota punje ya mchele hapa na pale uwe na uhalisia wa unachokileta. Hapa hujadili na genge la mazuzu wanaokushangilia bali unaongea na watu waanaweza kupitia kila unachotuletea.
Nilishaisahau kampuni unayosema iliingia inaitwa TRITEL ni kweli ndiyo hiyo na hapo ndipo ninapokushuruku kwa kunikumbusha lakini si kwingine kote ulikochemka kama ifuatavyo.
Kwanza mambo yako hivi. Baada ya ubinafsishaji kuanza kampuni ya kwanza ya simu za mkononi ilikuwa ni MOBITEL uliyoitaja. Kampuni ya pili kuja huko Tanzania ni TRITEL uliyonikumbusha.
Sasa nimehakikisha unapayuka na hujui lolote zaidi ya ushabiki. Unasema hivi,
Sitaitaja Tritel kwa sababu mifumo ya Tritel ilikuwa tofauti na Buzz na hao Vodacom!!!
Huu ni ushamba uliopitiliza.MOBITEL ndiyo walianza na mfumo tofauti yaani ANALOGUE. Simu zao zilipapatikiwa kwa sababu ya ushamba wa nchi hii kama unaouonyesha hapa, tena hata ukipigiwa simu ulikuwa unalipia. Lakini pamoja na hayo ikawa na wateja wengi.
Kampuni ya pili kuingia hapo nchini ni hiyo uliyotaja yaani TRITEL. Hii ndiyo ilileta mfumo wa DIGITAL na hata matangazo yao yalikuwa yanaikandia MOBITEL kwamba wao ni DIGITAL na MOBITEL ni ANALOGUE.
TRITEL ikawa na shida kadhaa. Kwanza kwa sababu simu ni DIGITAL zilikuwa expensive ikaonekana ni kampuni ya matajiri tu. Pia hawakujitanua sana. Mjomba wangu alikuwa na simu ya TRITEL lakini aliishia kupata D’Salaam, Mwanza na Arusha. Hata pale D’Salaam sehemu nyingi tu ulikuwa hupati TRITEL. Hili likawa tatizo.
Kingine ni kwamba TRITEL haikudumu ikaanza kuyoyoma. Kimsingi ilishindwa kuitoa ulingoni MOBITEL kwa sababu MOBITEL walikuwa wabunifu. Umedanganya watu humu kwamba MOBITEL ilikuwa inaitwa BUZZ. Hapana. BUZZ ilikuwa ni moja tu ya products zao. Tena kuna wakati walikuwa na product inaitwa KADI POA.
Hivyo, MOBITEL iliishi kwa ubunifu ikijijua mfumo wao ni ANALOGUE.
Wakati VODACOM inaingia ilikuta TRITEL inachechemea lakini MOBITEL inadunda tu, lakini MOBITEL yenye ANALOGUE. Alichofanya VODACOM ni kuja ma mfumo uleule wa TRITEL yaani DIGITAL lakini VODACOM ikaenea nchi nzima. Tofauti na TRITEL aliyeishia vimikoa vitatu tu. Tofauti na MOBITEL aliyekuwa na ANALOGUE.
Hivyo, waliochukia ANALOGUE ya MOBITEL wakahamia VODACOM kupaa DIGITAL. Walichukia TRITEL kukosekana mikoani wakahamia VODACOM.
Hivyo, VODACOM ilikuja na wingi wa mtaji na ikaenea nchi nzima kama hivyo. Hivyo acha kudanganya mambo usiyoyajua wewe wana wanaokuamini.
Tuendelee tena mdogomdogo, hapa chini unasema hivi,
Yaani hivi sasa nikukumbushe hadi uliyosema mwenyewe kwamba:-Sasa ikiwa Vodacom iliongoza tangu mwanzo kwa miaka yote hiyo, how come tena Dr. Idris Rashid akimbie "mziki mnene" wa Vodacom?! Hivi unafahamu Dr. Idris Rashid aliingia Vodacom wakati haijafikisha hata mwaka mmoja?
Ninakujibu hivi, Idrisa Rashid alikwenda pale VODACOM kwa hoja za kijinga kama mnazoleta sasa. Ujinga uliompeleka Dr. Idrisa ni kwamba VODaCOM ilipoingia haikutimiza siku kadhaa ikaanza kuongozwa na Managing Director mkenya anayeitwa
James Rege.
Ninajua ninakuguseni kwenye mfupa maana hamtaki kukumbushwa kwamba MD wa kwanza wa VODACOM ni mkenya, maana ndiyo hoja yenu ya sasa.
Kampeni yenu mnataka tusahau na tusikumbuke kwamba VODACOM TANZANIA imewahi kuongozwa na
mkenya na mnaelekea kufaulu kampeni hiyo.
Hivyo kama VODACOM iliongoza tangu mwanzo sifa huwezi kumpa Idrisa Rashid utampa huyu mkenya anayeitwa
James Rege.
Sasa kwa nini Idris Rashid aliondoka VODACOM. Idrisa Rashid aliondoka hakudumu hata kwa miaka miwili. Alipeleka majungu huku na kule kwamba wenzake kwenye Bodi wanamzunguka kwa sababu yeye ni mzawa lakini haikusaidia akaishia kuondoka.
Nimesema mahala fulani humu sasa hivi huyu Idrisa Rashid ameishia kuzunguka huku na kule kwenye vibenki vidogovidogo tena vingine vina harufu ya udini. Kule VODACOM alitumia uzawa sasa kila aliko anatumia udini.
Turejee tena kwenye VODACOM kuikuta sekta tangu upya. Kimsingi VODACOM ilikuta ni kama hakuna uwekezaji. Kwa sababu TRITEL ilikuwa inachechemea na MOBITEL haijawekeza kwenye DIGITAL.
Kama TRITEL ingekuwa na mtaji wa kuenea nchi nzima, VODACOM isingekuwepo au ingepata taabu sana kusimama. Hivyo, mafanikio ya VODACOM ni uzembe wa waliotangulia yaani MOBITEL na TRITEL kwa sababu wangeweza kujitanua na DiGITAl nchi nzima.
Hivyo, huyo Dr. Kimei na hao wazawa wengine mmoja-mmoja unaowataja, huwezi kuwapima kwa mikikimikiki waliyoikuta akina VODACOM. Siyo mikikimiki waliyoikuta huko CRDB na kwingine walikopitia ndiyo maana mwenzao Idrisa Rashid alishindwa pale VODACOM.
Lakini hata huko mnakosema walifaulu Dr. Kimei na wenzao akina Mchechu na Mafuru, nimeuliza swali rahisi sana humu hamnijibu.
Je wako wapi sasa hivi na waliondokaje huko mnakosema walikuwa? Maana moja ya hoja zangu mimi ni kwamba watanzania wana uvivu, majungu, wivu, fitina na wizi?
Hoja nyingine ni kwamba bahati nzuri wote tunakiri kwamba VODACOM iliingia kwa mafanikio tangu mteja wa kwanza, yenzi ya akina James Rege. hivyo mafanikio ya VODACOM ni tangu siku inaingia.
Sasa hayo mafanikio mnayoyasema kwa Dr. Kimei na wenzake iliwachukua miaka mingapi kuyafikia?
Ni mtanzania gani aliyeongoza kampuni inagombaniwa na wateja tangu siku ya kwanza? Ni mtanzania gani aliyedumisha sifa ya kushinda ushindani tangu siku ya kwanza?
Tunachosikia ni kampuni wanaanzisha hatujui wamekopa benki gani na kisha baadaye zinaanguka. ndiyo hizi zinazolalamika sasa kwamba
vyuma vimekaza.
Hivyo walaumuni watanzania wenzenu walipewa fursa kama huyu Idrisa Rashid na wadogo zake aliowatumia na nyinyi mnaomshabikia.
Binafsi ninaona VODACOM wamecheza kama pele. Hawataki kurudia kosa walilfanya alipoondoka mkenya yaani James Rege na kumleta zezeta mtanzania akachemka.
Sasa kama pale VODACOM alichemka mtu aliyewahi kuwa Gavana BoT sasa wewe unayeishi madongokwinama ndiyo itakuwa balaa.
Heko VODACOM. Heko Hisham. Sasa pigeni kazi mrudi katika ushindani kama zamani maana watu hawajui kwamba mtandao unaoogoza sasa ni TIGO ukijumlisha na patner wa ZANTEl.
Kuna hoja kwamba eti yule mama Sylvia, mkenya, angeiua VODACOM ili SAFARICOM iendelee. Mbona James Rege hakuiua VODACOM na kinyume chake ndiye aliyeingiza wateja wengi siku za kwanza.
Hivi mfano VODACOM iwe kampuni yangu, iweje mimi kampuni ni yangu, ninachagua Managing Director aongoze kampuni yangu, halafu wewe ambaye hata karanga hujawahi kuuza unasema eti huyo MD ataangusha kampuni yangu ili SAFARICOM ibaki hewani. Sijawahi kuona hoja za kipunguwani kama hizi.
Watanzania acheni uvivu, majungu, fitina. Chapeni kazi. Na mkome kabisa kutumia hoja ya uzawa ndiyo itakayowadumaza miaka yote.
Kwa mtu mwenye akili moja kwa moja anajua wewe ndo mshamba!!
Kwahiyo?! Hivi unafahamu maana ya management wewe?! Yule Omar Issa ambae alikuwa CEO wa Celtel alitokea sekta ipi?! Mchechu ambae aliiongoza NHC kwa mafanikio makubwa alitokea sekta ipi? Idris Rashid ambae alienda kuwa MD wa TANESCO alitokea sekta ipi?!
Unashindwa kutofautisha kati ya technical positions na management positions!
Kwahiyo unataka kusema mafanikio ya CRDB ni kwa sababu ipo kabla ya hizo benki zingine?! Yaani bado unaita wenzako washamba ikiwa unaishia kutoa hoja nyepesi kama hizi?! Kama ndivyo, kwanini NBC isiwe ndiyo the most successful bank kulinganisha na CRDB?! Kwanini Benki ya Posta isiwe ndio the most successful bank kulinganisha na NMB?!
Umesahau kwa sababu hujui lolote zaidi ya majigambo yako! Na kwavile hujui, wacha nikukumbushe kwamba Vodacom wameingia wakati kuna Mobitel na Tritel ambao walikuwa pale jengo la SIDO karibu na Tanganyika Library! Btw, kama kutangulia ndo kunafanya kampuni iwe bora zaidi, kwanini basi nafasi ya Vodacom isingekuwa ya Mobitel/Buzz/Tigo?! Vodacom wameingia Tanzania wakati Mobitel/Buzz wakiwa na takribani miaka 6!
Nikukumbushe wewe ambae unaonekana unatakiwa kukumbushwa mengi! Nakumbuka vizuri wakati bro anamaliza pale UDSM mwaka 2000, ndipo Vodacom walikuwa wanakaribia kuanza kutoa huduma!
Umesema moja ya sababu za CRDB kuwa juu ni kwa sababu walianza mapema zaidi kulinganisha na foreign banks! Kama hiyo ni hoja, ni kwanini basi Vodacom wakawaacha Buzz ambao walikuwa in business kwa takribani miaka 6!! Sitaitaja Tritel kwa sababu mifumo ya Tritel ilikuwa tofauti na Buzz na hao Vodacom!!!Voadcom walianza from the scratch lakini bado waliwaacha Buzz ambao walikuwa in busines kwa takribani miaka 6 kabla yao, na kwahiyo hoja yako haina mantiki!
Hoja nyepesi kabisa hii manake kama ingekuwa na uzito, basi Tanzania Postal Bank ingekuwa kubwa kweli kweli! Lakini tukiachana na TPB, basi angalau NBC ingekuwa ni kubwa kuliko CRDB! Na ni kichekesho kudai mafanikio ya Dr Kimei ni kwa sababu alianza hapo kabla ya foreign banks hazijaingia kwenye game wakati anayefahamu masuala ya kibenki anafahamu moja ya sababu iliyozifanya foreign banks kuwa pale ni kwa sababu wakati wanaingia walikuwa very selective! Hawa wali-target corporate market kwenye nchi iliyokuwa na uhaba wa corporate customers! Walifanya hayo wakiamini the poors are unbankable hadi walipokuja kuamshwa usingizini na NMB kwamba even the poors are bankable, and all you need to know is their needs! NMB walitumia vizuri ideas za Hernando de Soto Polar, a Peruvian Economist aliyepata kusema usione mtu anaishi kwenye nyumba ya udongo ukadhani ni useless creature in the economy!
Omar Issa alienda Celtel akitokea industry ipi?!
Yaani hivi sasa nikukumbushe hadi uliyosema mwenyewe kwamba:-Sasa ikiwa Vodacom iliongoza tangu mwanzo kwa miaka yote hiyo, how come tena Dr. Idris Rashid akimbie "mziki mnene" wa Vodacom?! Hivi unafahamu Dr. Idris Rashid aliingia Vodacom wakati haijafikisha hata mwaka mmoja?
Hahahahahaha, kama akijibu hizi hoja mimi JF naacha na sirudi tena. Hata ingekuwa ni mimi hizi hoja ningekimbia kuzijibu. Mkuu ahsante sana, uwe na usiku mwema.
Unajua nimelazimika kusoma michango yake kwenye hii mada! Yaani ana tatizo lakini hajui kwamba ana tatizo! Yaani "watanzania nyinyi wa huko hivi, watanzania nyinyi mlio local vile" na yote hayo yakiashiria Watanzania ni mabogasi! Halafu anataka kuaminisha watu kwamba telecom industry ni very complex industry ambayo, ambayo kuiweza kwake ni ama uwe telecom guru au rocket scientist, na kama ni Mtanzania, basi hata uwe Quantum Physicist basi huwezi kuongoza kampuni ya simu hususani Vodacom!
Mkuu jamaa ana kiburi cha kipumbavu sana, lakini nashukuru umetusaidia sana kumnyamazisha. Kama atakuwa na akili nzuri basi ataona ni wapi amekosea na ajirekebishe.