Yah natumia voda ila huku flesh wala haisumbuiChangamoto sana master, na wewe unatumia Voda?
Siyo voda tu kwa sasa ni kilio kote.mawasiliano mabovu,bando zinaisha bila mpangilio ni vurugu tupu.sijui majirani zetu nao wanapata adha hizo?tangu Oktoba 29 hali haijatulia hadi leo.Ndugu zangu kwema?
Hivi na nyie mnapata changamoto ya kimtandao hususani kwa watumiaji wa Vodacom kama mimi?
Ukituma meseji haziendi, ukijaribu kupiga simu muda mwingine simu inabaki kwenye connecting mode tu hata kwa dakika mbili bila hata kuita.
Ukijaribu kutumia M-Pesa Menu ya kawaida yaani 150*00# simu inazunguka mwisho wa muda inakuandikia "USSD connection failed.
Kuhusu kutumia Internet na yenyewe changamoto tu, unawasha data inakuwa on, then baada ya dakika kadhaa inaji-switch off yenyewe. Kwa ufupi changamoto sana.
Tatizo ni nini wakuu?
Hapana.77 wanabana internet na mawasiliano.
Kama wanazingua vunja line mkuu hiyo siyo TANESCO wapo peke yao.Hapana.
Hawa jamaa mda tu mtandao wao ulianza kuwa hovyo internet speed ya kobe.
Mtandao wangu mkuu kwa internet ulikuwa voda ila kwa sasa nimeweka pembeni laini yao angalau halotel na yes wanajitahidi.
Sijui shida yao nini.