Naona haters wanajaribu kuchota maji kwa kutumia chujio, mbaya zaidi inavyoonekana hawana hata elimu ya masoko kipengele cha matangazo, wacheni niwape desa advertising(kutangaza) ina malengo matatu makuu la kwanza kufanya umma utambue uwepo wa huduma, lengo la pili kushawishi watu kununua Huduma na la mwisho kuhakikisha watu wanaikumbuka huduma, hivi vyote vishakamilika kwenye hayo mabango, so malengo yashafikika ni mwendo wa kusonga Mbele kwa mikakati mingine, kitu kingine kuna break even point ambapo biashara inabidi ifanye kazi pale ambapo faida izidi matumizi ama ilingane na matumizi, gharama za kutangaza hayo mabango huenda ikawa inataka kukiuka kanuni za break even point maana voda washatumia biioni na kitu kumshawishi mnyama huyu mnaemkeshea kwenye keyboard zenu asaini mkataba,