Vodacom waonesha ukinara wao, waleta 5G nchini

Vodacom waonesha ukinara wao, waleta 5G nchini

Kwa gharama hizi? Najua hiyo 5G ina wateja wake - wengi wao wakiwa wanufaikaji wa tozo
 
Kampuni ya simu ya Vodacom wamefanya kweli, leo wametambulisha teknolojia ya 5G nchini na kuwa kampuni pekee mpaka sasa nchini yenye 5G.

Nimefurahi sana, tumekuwa na simu za 5G mpaka zinaelekea kuchakaa tumeshindwa kuziutilize kwenye eneo hilo. Muhimu mtandao uwe reliable na vifurushi vya mtanzania.

Hongereni Vodacom, mimi mgeni wenu. Tigo nitawatafutia kisimu kidogo.
Tandao lenu Leo kila ukijiunga na bando la SMS linakataa
 
Vodacom kila kitu huwa wanakuwa wa kwanza.
Huduma za PESA kwa maana ya MPESA walikuwa wa kwanza

Kuunga vifurushi badala ya kutumia vocha walikuwa wa kwanza, yaani zamani ilikuwa unaweka vocha na kutwanga tu.

4G walikuwa wa kwanza

Kuna huduma ya email wao ndio walikuwa wa kwanza ingawa ilikufa. Yaani namba yako ilikuwa ndio utambulisho wako mfano 0763000000@vodamail.co.tz

THEGRID
Lakini pia voda ndio mtandao wa kwanza kukomba salio lililobaki kwenye simu

Usisahau voda ndio mtandao wa kwanza kukuunganisha na huduma ambazo hujaomba.
Wapo vizuri sana, Hio the Grid ilikuwa n social media, ilikuwa na map unaweza ona rafiki zako walipo, unaweza post picha n.k ilikuwa 2008 hio sijui kama bado ipo, ila wangeendelea leo ungekuwa mtandao mkubwa, nakumbuka ilikuwa kwenye symbian..
 
Kama 4G yenyewe bado chenga, hiyo 5G itabaki tu kuwa hadithi za alinacha...
 
Back
Top Bottom