Vodacom wazindua Router za 5G, bei pasua kichwa

Labda unisaidie na waliokufanikishia zoezi zima maana mimi nimeongea nao, then mtu akanipigia, nikamtumia eneo ninapoishi sasa ni wiki ya 3 hamna ripoti na nikimtafuta ni majibu yasiyo eleweka.
Surveyor ishapita?
 
Hadi surveyor apite, mi surveyor walikuja mara 2
Mapema tu ndani ya siku 1
Baadae nikasajili line, nikalipia wakaleta

Sawa nitaendelea kuwa na subira kwa kuwa sina namna , Fibre haifiki, Copper haipo. Je, zaidi ya deposit na kusajili line walihitaji nini kingine?
 
Tatizo kwa maelezo ya Waiziri wa haya mambo ya mitandao hiyo ni huduma ya ziada, unaweza ukatoa 850,000 ukakinunia hicho kikopo halafu ghafla ukaambiwa gharama za bando zimebadilika hakuna hiyo unlimited volume ya data tena ukaungishwa hizi za 50,000 unapata gb 24 ambazo zinafyekwa kwa kasi ya 5G. Hakuna consumer protection....
 
Tanzania mfanyabiashara ndiye boss na mteja ni kama mtumwa. Hii mentality iko kila mahali. Kwa nini wasiweke utaratibu wa malipo ya kila mwezi kidogo kidogo yalipwe pamoja na fees ya kila mwezi? Itapunguza mzigo wa kutaka wateja walipe kwa mkupuo.
 

Hiki kitu ni cha kweli kabisa maana hapa nilipo nina Router ya Tigo ya Home internet ambayo haina kazi maana hiyo huduma kwa sasa inatoa vifurushi sawa na hivi vya kawaida; tofauti na vile vya awali.
 
Sawa nitaendelea kuwa na subira kwa kuwa sina namna , Fibre haifiki, Copper haipo. Je, zaidi ya deposit na kusajili line walihitaji nini kingine?
Copy ya ID
TIN
 
Mtu ananunua iphone 3M anashindwa toa 800k kununua router?

Just priorities.
 
Mtu ananunua iphone 3M anashindwa toa 800k kununua router?

Just priorities.

Ndiyo wapo wenye pesa hizo ila ninaamini pia customer base hii yenye disposable income ya kutosha, asilimia kubwa wanaishi au ofisi zao zipo kwenye maeneo ambayo tayari wana Raha, Simba, Zuku, Liquid au mtoa huduma mwingineyo wa Fibre hivyo wanacheaper options.

Pia, unapaswa kuangalia variables kadhaa unapofanya ununuzi kama huu, maana iPhone na Router ni vitu viwili tofauti. iPhone unaweza kuitumia miaka kadhaa kisha ukaiuza na bado ika retain value nzuri.

Hii Router kuna mengi ya kujiuliza. Je, Vodacom kwa mfano baada ya miezi kadhaa labda kutokana na mabadiliko ya sheria wakaondoa hivi vifurushi vya unlimited (mfano mzuri wa hali kama hii ni ile huduma ya Tigo Home Internet) utabaki na kopo hili la laki 8? Utaliuza? Kwa nani? Na kwa bei gani?

Imetokea siku moja unatoka nje unaona TTCL (Au mtoa huduma mwingineyo) kapitisha Fibre mtaani kwenu wakati umeshapoteza 800k kwenye hili kopo (Je, utaweza kulitumia walahu kama Wifi 6 Router au functionality hiyo imezuiwa).

Airtel nao pia wamenunua spectrum za 5G na wana mipango ya kuzindua wireless home broadband, je ukiona wana offer nzuri kuzidi Vodacom unaweza kuhama na kutumia kopo hili na Airtel au lazima ununue jingine? Kuna mengi ya kufikiria.
 
Spacex huwezi inunua wala kuilipia kama hii inakutoa jasho.

Kwa kuwa umeona Starlink inalipiwa 99$ Marekani haimaanishi kuwa na Afrika itakuwa bei hiyo hiyo. Ninaamini watachukua strategy kama ya Spotify, Apple Music na Netflix ya kuangalia Purchasing Power Parity (PPP) ya nchi husika. Ukiangalia wanacholipa Marekani kwa mwezi na tunacholipa nchi za Afrika na India kwa mwezi -- ni vitu viwili tofauti huku huduma tunapata ileile.

Ninafuatilia kwa umakini Nigeria na Mozambique (nchi ambazo zimeiruhusu Starlink) kuona Pricing strategy yao. Lakini naona mambo yatakuwa mazuri kulingana na mifano hapa chini:

France wanalipa 50€ SpaceX Starlink’s Variable Pricing Pilot in France Is Good Business and Good Karma

Mexico 55$ Starlink internet service cuts monthly fee in half
 
Okay, ila sema wameweka bei kubwa sana kwasisi watumiaji wa kawaida ilifaa wawe na kianzio cha chini kidogo walau hata 70K
Mkuu, in short ni kwamba kwa nchi kama Tanzania hii technology imekuja mapema sana kulingana na hali ya uchumi wa wengi. Inapaswa kuja Tanzania endapo south Africa wapo na 6G
 
Hujaelewa.

Usikaze fuvu na story ya kopo la 800k.

Wangapi wananunua tv, radio, fridge za milion na zinaharibika anatupa ananunua ingine?

Na wengine hiyo 800k wanaifanya kama investment. Ndani ya miezi 6 inarudisha hela yote hata akiitupa haimuumizi akili.

Nimekupa mfano wa mtu anaetoa 3M ananunua simu manake akitoa 800k haogopi nani ataleta internet ya aina gani na ni hela ndogo sana kwake kumuumiza kichwa.

Wewe unaetoa 800k ukiogopa airtel ataleta internet ingine utafanyaje na hilo kopo. Wengine wanalitupa hilo kopo tu au wanaweka ndani.

Mwingine akishapata satisfaction inatosha. Hayo mengine hayampi presha.
 
Ulivyoiongelea mwanzo ulionesha Starlink utapewa bure na utakuwa unalipa $5 kwa mwezi.

Hiyo €50 ni sawa na internet ya vodacom ambayo inakutoa jasho tangu awali.
 

Huu ni wizi
 
Mkuu hio Nokia Fastmile ni Bei ndefu, si Chini ya Milioni 1 maeneo mengi duniani, Hapo voda pengine wame subsidize mpaka kufika 850k na kama unavyoona ni Enterprise device, capacity mpaka watu 200, sio kifaa cha majumbani.

Tusubirie tu router zetu za watu 10.
 
Ulivyoiongelea mwanzo ulionesha Starlink utapewa bure na utakuwa unalipa $5 kwa mwezi.

Hiyo €50 ni sawa na internet ya vodacom ambayo inakutoa jasho tangu awali.
Mimi natamani sana Starlink ije hapa Tz tuone Fanboy wake kama wataridhika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…