Ndiyo wapo wenye pesa hizo ila ninaamini pia customer base hii yenye disposable income ya kutosha, asilimia kubwa wanaishi au ofisi zao zipo kwenye maeneo ambayo tayari wana Raha, Simba, Zuku, Liquid au mtoa huduma mwingineyo wa Fibre hivyo wanacheaper options.
Pia, unapaswa kuangalia variables kadhaa unapofanya ununuzi kama huu, maana iPhone na Router ni vitu viwili tofauti. iPhone unaweza kuitumia miaka kadhaa kisha ukaiuza na bado ika retain value nzuri.
Hii Router kuna mengi ya kujiuliza. Je, Vodacom kwa mfano baada ya miezi kadhaa labda kutokana na mabadiliko ya sheria wakaondoa hivi vifurushi vya unlimited (mfano mzuri wa hali kama hii ni ile huduma ya Tigo Home Internet) utabaki na kopo hili la laki 8? Utaliuza? Kwa nani? Na kwa bei gani?
Imetokea siku moja unatoka nje unaona TTCL (Au mtoa huduma mwingineyo) kapitisha Fibre mtaani kwenu wakati umeshapoteza 800k kwenye hili kopo (Je, utaweza kulitumia walahu kama Wifi 6 Router au functionality hiyo imezuiwa).
Airtel nao pia wamenunua spectrum za 5G na wana mipango ya kuzindua wireless home broadband, je ukiona wana offer nzuri kuzidi Vodacom unaweza kuhama na kutumia kopo hili na Airtel au lazima ununue jingine? Kuna mengi ya kufikiria.