Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke

Mtoto wa Samia, umelewa?
 
Nijuavyo mimi kaka Pasco huwa haandiki kitu kwa kubahatisha. Maandiko yake yote huwa yanaeleza bayana yajayo kutoka jikoni yaliyokwisha pangwa na wapangaji wa hatma ya Taifa.

Ukisoma mabandiko yake huwa anatumia kauli za kutuhadaa kwa kugusia vitu ambavyo mwenye akili kubwa ndo atang'amua uhalisia wa mambo.

Bandiko lolote la Mkuu wetu Pasco au ndugu Tumia Akili usilichukulie kawaida, soma vizuri between lines kwa kutuliza ufahamu maana huwa wanatupasha habari na mipango ambayo imekwisha iva bado kuliwa tu.

Ubarikiwe kwa kutunyetisha yajayo japo huenda yakawa yanahuzunisha kwa baadhi lakini hakuna namna. Umeshasema, ni nani awezaye kupinga?, jibu ni hakuna isipokuwa Mungu pekee.
 
Asante, ila unisamehe kama nimekukwaza.
No elvischirwa , hujanikwaza bali umesaidia sana kuwaelimisha watu humu jinsi ya to read in between the lines kwa kutenganisha Mungu na mungu, na kiukweli kuna sauti mtu anaisikia akadhani ni sauti ya Mungu kumbe sio sauti ya Mungu bali ni sauti ya mungu.

Hili la the voices from within ni sauti ya nani, pia nimelizungumza pale mwanzo.
P
 
Asante mkuu
 
Assuming maono haya yakatimia, maana yake Dr. Hussein anaweza kupiga ungwe 2, 2025-35;

Mwanamke anaeweza kuchukua kwa Dr. Hussein atakuwa ni nani?
Ni katika hawa wanawake ambao tunawajua wanatamba kwa sasa katika majukwaa ya siasa au atakuwa mtu mpya ambae kati ya sasa na 2035 anatengenezwa na kuandaliwa au atajiandaa?

Itawezekana mkulu wa sasa kutema ngese au kile alichosema akiwa US chaweza kutimia. Alisikika akisema ikiwezekana hata kuupoteza 'ukulu' atafanya hivyo ili kujenga demokrasia hapa nchini.

Je, alisema kwa uvuvio kama huu wa Paskali au ni coincidence?

Japo in politics hakunaga coincidences, in most cases mambo hupangwa, unless Yeye alie juu ya Falme na Mamlaka aweze ku-step in ili kusudi lake juu ya Watanzania litimie.

Mambo yaliyosemwa na kinabii hutumia ila mengine huwa yanaweza yasitimie pale wahusika wanapomwomba Alie Juu acheleweshe au asifanye kwa wakati huo.

Paskali ni moja ya Watanzania wachache wenye guts za kusema pasi woga maadam hawajavunja sheria.

Bila shaka hatawekwa kitimoto kama kule mjengoni kwa kusema yale ambayo kuna wengine hawapendi kuona yakisemwa/kuandikwa.

Mungu ubariki Tanzania, wabariki viongozi wetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…