Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke

Mimi Mbona ni mwenzenu TU!!?

"Rasimu ya Warioba irudi mezani Sasa iwe Katiba mpya"!
 
Kwa nini uwaze watu wale wale? Sura na majina yale yale!! Kwani hakuna mtanzania mwingine anayefaa? Lazima tusikie ubini wa akina Mwinyi, karume, lowassa, kawawa, nape, makamba, etc...?

Sema mmefunzwa na kulelewa kulinda system/state.
 
Hii sauti itakunyima ubunge EAC usipokuwa makini
Mkuu Proved, kugombea kwangu EALA ni baada ya kujitathmini kuwa ninaweza kusaidia, hivyo ikitokea nikateuliwa, niteuliwe kwa ability na capabilities na sio kuteuliwa kwa hisani, hivyo ikitokea mtu mzuri, una uwezo wa kusaidia nchi yako, lakini ukakatwa kwasababu ya kuusema ukweli, then be it!.

Japo kuna vitu vinaonekana kama sio vitu vizuri, lakini ndio vitu vinavyosaidia. Angalia hoja zilizoshushwa kwenye nyuzi hizi, laiti waliotajwa wangesikia and act accordingly, labda yaliyowakuta, yasingewakuta "Ombeni Mtapewa", Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je Wajua Kauli Huumba? Angalia Kauli Hizi Ziliumba Nini!. Laiti Zingesikizwa...!.
P
 
Nami nimesikia sauti ikiniambia Mayalla atakuwa rais wa Burundi 2025!
Joke. Lakini Watanzania tuwe na subira. Kazi ya urais si rahisi hivyo uonavyo. Na wala msimfananishe Samia na Magufuli. Kila mtu na style yake.
Ninachokiona, ingawaje rasi Samia ana makosa kadhaa ya uongozi, kubwa kuto 'regn' juu ya viongozi wachache wanaomharibia.....lakini ni rais mzuri sana anayejua 'siasa ya uchumi'. Kwa vile bado namchukulia mgeni katika cheo hiki tena bila maandalizi, natumai atajirekebisha. Akifanya vitu viwili vitatu tu, serikali yake itakuwa ya mafanikio sana. Sio kama Magu ambaye sera aliyokuwa akienda nayo hatimaye ingeiangamiza kabisa uchumi na mshikamano wa nchi hii, ingawaje pia alikuwa na mazuri fulani- kutouonea haya ufisadi, msisitizo juu ya nidhamu na kuleta haiba ya dola.
 
Kaka Paskal
Hii
 
Leo nimemsikia Spika Dr. Tulia kwenye swali la Mhe. Luhaga Mzima, Tulia akiendelea hivi kutanguliza mbele maslahi ya Taifa, usiku huyu ndiye yule mwanamke niliielezwa kwenye ile sauti kuwa 2030 ni mwanamke!.

Niliwahi kumzungumza Dr Tulia hapa Je, Wajua, Naibu Spika, Chini ya "Bora Spika", Anaweza Kuwa "Spika Bora?". Dr. Tulia, "Ukitulia, Una Fursa ya Kuwa Spika Bora Sana!" Hongera Sana! nilisema
Msikilizeni hapa Spika wetu Dr. Tulia
I was dam right about this lady!.
Nilisema Dr. Tulia akitulia she can make the best Spika!. That video clip is the proof, she is the best!.

Tena nadhani huyu mwanamke aliyezungumzwa hapa for 2030, could be Dr. Tulia!. Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke
Hongera sana Spika Dr. Tulia, umeonyesha uwezo to be the best,
God bless you.
God bless Tanzania.

P
 
Uzi wako umekunyima ubunge wa Afrika mashariki.
Huwezi kumshusha rais aliyeko madarakani kuwa hafai 2025 tena wa ccm na ukapewa nafasi yoyote...sahau[emoji23]
 
Uzi wako umekunyima ubunge wa Afrika mashariki.
Mkuu Amazon2 , kwanza sio kweli uzingizini huu ndio umenyima ubunge wa EALA!. Kule nimezidiwa sifa kama nilivyo eleza hapa EALA: Waliopitishwa CCM, ni Kwa Haki!, Tulioachwa ni kwa Haki, Tumezidiwa Vigezo!. Thanks4 for Support, Nimekubali Matokeo Kiroho Safi! Kazi Iendelee!
Huwezi kumshusha rais aliyeko madarakani kuwa hafai 2025 tena wa ccm na ukapewa nafasi yoyote...sahau[emoji23]
Kwanza sijamshusha popote na wala sijasema popote kuwa hafai 2025!. Nilichosema ni kuisikia tuu sauti kuwa kwa vile tumepanga 2025 twende na mwanamke, Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye! hii sauti imesema tuendelee kwanza na mwanamume halafu mwanamke aje 2030!.

Mimi ni miongoni wa watu wanaomkubali sana Samia na mimi ni miongoni mwa tuliomuumbia rais Samia urais wa Tanzania kwa kauli umba zetu "Ombeni Mtapewa", "Tafuteni Mtapata", "Bisheni Hodi Mtafunguliwa" Je Wajua Kuna "Kauli" na "Kauli Umba" Ambazo Huumba?. Shuhudia..
P
 
Juzi Ansbert Ngurumo naye ameskia sauti ikimsemesha.....

Nchi ngumu hii- Ulimwengu one said.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…