Wanabodi
Haya mambo ya mtu kusikia sauti, sio mambo ya ulimwengu huu wa mwili, haya ni mambo ya ulimwengu wa Roho.
Hii ni thread ya maono ya unabii, na sio utabiri na sio trends reading, ni unasikia tuu sauti inakuambia jambo fulani bila kuambiwa sababu na huwezi kuuliza, hivyo nami naomba kuwaeleza tuu sauti niliosikia na naomba msiniulize kitu kwasababu sio mimi ni sauti
Leo nilikuwa naandika bandiko fulani humu JF, ndipo ghafla nikaisikia sauti (voices from within) kuwa Rais wa JMT kwa 2025 should be Dr. Hussein Mwinyi kwa kipindi kimoja, then 2030 ndipo tuje na mgombea mwanamke!.
Sauti hiyo inamaanisha inamtaka Rais Samia awe ni Rais wa JMT kwa kipindi kimoja tuu hadi 2025. Sauti hiyo ikasema ni Rais Samia mwenyewe willingly anatakiwa kumuomba Dr. Hussein Mwinyi, 2025 aje kugombea urais wa JMT, kuimalizia awamu ya pili ya Samia, kwa awamu moja tuu,.
Na kipindi hicho cha 2025- 2030 ndio sasa sasa tufanye grooming ya Mwanamke atakagombea urais wa JMT kwa 2030.
Japo sio sio lazima kusema kila unachosikia, kwa sababu sometimes sio kila unachosikia from within ni sauti kutoka kwa Mungu au ni maono, sauti nyingine ni sauti za shetani tuu na sio sauti za Mungu, kama zilivyo ndoto nyingine, ni ndoto za shetani kama ile "ndoto ya Lema", ukisikia sauti ukahisi inaweza isiwe sauti ya Mungu, au ukiota ndoto ya jambo la ajabu ajabu ukahisi jambo hilo sio la kheri, sio lazima uliseme). Mfano ni tangu August 14, 2014 nilielezwa rais ajaye wa Tanzania ni Magufuli, na nilielezwa sababu kwanini ni Magufuli, nami nikaeleza humu lakini sikuzisema.
Wanabodi, Leo nimekutana na rafiki yangu wa siku nyingi tuliyepotezana naye kipindi kirefu nyuma, ambaye ni mtu wa sehemu na wa kuaminika sana ambaye yuko attached CCM kama kada tuu wa kawaida wa Chama cha Mapinduzi-CCM, akanieleza seriously habari za kushtusha kidogo ambazo mimi zimenitisha...
www.jamiiforums.com
Hiyo 2014 wakati mimi nikisema mgombea wa CCM kwa 2015 ni Magufuli, wakati huo unaweza kukuta hata JPM mwenyewe alikuwa hajui kuwa ndiye yeye.
Hivyo hata sauti hii niliyoisikia leo, 2022, kuhusu 2025, usikute hata Samia mwenyewe hajui, na kwasababu ni Rais Samia aliyependekeza 2025 twende na mgombea mwanamke, unaweza kuta ni Samia anajipanga kuendelea, huku Dr. Mwinyi akiji set kwa his second term in Zanzibar, wala hahui kuwa yeye ndiye rais wa JMT, 2025.
Mimi naona hiyo 2025 Hussein Mwinyi angekuja kugombea Tanganyika! Halafu huyu mama aende akagombee Zanzibar, au apumzike na kuwapisha wengine.
Maana ni ukweli kwamba kwenye hii nchi, bado tulikuwa hatujafikia hatua ya kumkabidhi mwanamke madaraka kutokana na aina ya Katiba tuliyo nayo, lakini pia uwepo wa mfumo dume katika mazingira mengi yaliyo tuzunguka.
Na binafsi naamini pia hata Mheshimiwa aliye tutoka, hakuwa na imani kama msaidizi wake atakuja kuichukua nafasi yake kabla ya muhula wake wa pili alioshinda kwa zengwe kukamilika!
Na madhara ya kutojiandaa kuwa na Rais wa jinsia ya kike ndiyo haya sasa! Watu wanafanya vile wanavyo ona inafaa! Wafanyabiashara wakubwa wamekuwa ni majeuri kweli kweli, kiasi watu wa chini wanataabika! Huku mama akiwa hana cha kufanya.
I wish angetumia hii miaka michache iliyobakia, kutengeneza mazingira bora ya uchaguzi huru na wa haki hiyo 2025! Na hakika akifanya hivyo, basi atakumbukwa na vizazi vyote hapo baadaye! Badala ya kulazimisha kugombea tena kwa mashinikizo ya wachumia tumbo wachache, na mwisho wa siku kuishia tu kukumbana na upinzani mkali kutoka ndani na nje ya chama chake.
Paskali mzee wa voices from within or ancestral umekuwa unatabiri mambo mengi na kugeuka ukweli. Mi nakuunga mkono lakini sababu zangu zinatokana na Mrumishi mmoja wa mungu kutoka Zimbabwe Dr Ian Ndlovu mtafuteni you tube msikilize prophecy zake kuhusu Namba wani.
Lakini kwa mtazamo wangu usemi wako wa ampishe Mwinyi halafu yeye aje agombee baadae sidhani kama itawezekana. Ukimsikiliza mtumishi huyu wa mungu anasema mheshimiwa kuna makosa ya kiutendaji atayafanya na asipokuwa mwangalifu qoute " People from within her party will try to remover her. Binafsi naona suala la Kupanda gharama za mafuta na maisha kwa ujumla halipewi uzito unaostahili na wahusika, Nafikiri pia issue iliyomngoa Ndugai na hawa wanaomsagia kunguni mwendazake kila kukicha kwenye majukwaa mbalimbali ikiwemo humu online hawana siha kwenye mustakabali kwa wananchi.
Binafsi napenda raisi wangu aendelee kutuongoza na mola amlinde na ampe hekima,akili zaidi na busara za kutatua changamoto zinazotukabiki wananchi moja kwa moja na si kutegemea mawaziri wakae vikao ndio waje watende. Na naamini Mama atatupa mkeka wa katiba mpya 2026 na hiyo itawaumiza zaidi wale chawa wa chama chake wasiojua kuwajibika,Kazi iendelee mama mpaka 2035.
Kwa maoni yangu, Rais Samia Suluhu Hassan anafanya vizuri sana. Hali ya uchumi inasababishwa na matatizo ya uchumi wa kidunia. Lakini anafanya vizuri naa Hana uchu wa MADARAKA. Aachwe, apewe nafasi AFANYE KAZI Kwa uhuru mpaka kipindi CHAKE kiishe.
Bernard Camilius Membe pia ataweza kuwa Rais mzuri sana baada ya Rais Samia kumalizwa muda wake.
Mwingine ambae atamrudisha mshikamano, ataondoka dhulma ni Mzee WA chuga AbdulRahman KINANA. Pia anafaa Sana kuwa Rais wa Tanzania.
Mmeambiwa hiyo ni sauti yake kutoka ndani ndio ameisikiliza, na hii sio mara yake ya kwanza kuizungumzia hiyo "voice from within", sasa mnampigia kelele za nini?
Kama mnamuhumkumu PASKALI kuwa ana chuki kwa huyo aliyepo sababu ni mwanamke, basi nami nawahukumu nyie kwa mahaba yaliyopitiliza, kwangu hivyo vyote ni makosa, nyie wote hamfai kuwa majaji wazuri kwenye hii kesi.
Tatizo lililopo mpaka sasa kwa viongozi wa vyama vya upinzani ni kukosekana kwa umoja na mshikamano baina yao!
Halafu wengi wa viongozi wa hivyo vyama ni mamluki wa CCM! Imagine mtu kama John Cheyo, John Shibuda, Augustino Lyatonga Mrema, Seif Rashid Mohamed, Prof. Ibrahim Lipumba, huyu mwamba Zitto Kabwe, nk.
Kiukweli hawaaminiki hata kidogo! Chadema nao wanaamini sana katika siasa za harakati kuliko zile za maridhiano! Yaani kukaa meza moja na CCM kwao wanaona kama ni jambo lisilo wezekana kabisa! Mwisho wa siku CCM inazidi tu kuneemeka kutokana na haya mapungufu ya wapinzani.
hahahahaha bila shaka wazo lako ndio kitakachotokea... CCM wajanja sana...hii ndio karata yao 2025 -2030-2035....Upepo utakuwa umetulia halafu mnaletewa christiana na watakuwa wameshajipanga tena..
Huna macho ya kuona yajayo. Pia hata kulinganisha issue hii na ingine kujumlisha na kupata hesabu na jumla yake pia huwezi. Reading between the lines Kwa GT ktk masuala ya siasa ni jambo muhimu.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.