Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke

Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke

Ahsante, kazi ya zamani sana duniani hiyo, hata kizazi vya Yesu kwenye biblia wako makahaba tena wa kutupwa. Siyo jipya hilo.
Hufahamu uislam na wala hujui uislam

Umezaliwa umekuta ndugu zako waislam ukapelekwa madrasa ndio mwisho wa unachokijua

Hakuna maandishi ya kiislam yanayomtaka mwanamke ajikweze na ajae matusi mdomoni

Mwanamke kamili wa kiislam Saudia anafundishwa kuwa mke wa pili, tatu na nne

Tanzania kuna mkanganyiko wa dini ya kiislam,

Angalia Iddi ya Tanzania, Tanzania kuna uislam mpya ambao haufuati taratibu za Mecca

Afrika mashariki, Tanzania wana Idi yao ambayo wanafuata mwezi wao tofauti

Swali, Nani anatafsiri upya dini hii Tanzania kuhusu kufunga na kufungua kwa waislam, Maandishi yaliyopo ni ya Abu Bakr

Na sasa waislam wamezidi kugawanywa kwa Misingi ya itikadi, Hakuna sherehe moja ya Idi tena Tanzania, Wa kweli wanafungua lakini sherehe haitambuliki na serikali

Wengine wananuna lakini hawana la kufanya wanafungua siku ya serikali

Hayo ndio mambo ya kujadili, Nani anatakiwa auone mwezi Tanzania, Mwezi upo Tabora na Tandahimba unaambiwa hujaonekana Endelea kufunga

Mwezi upo Mombasa na watu baadhi ya Tanga wanauona unaambiwa haujaonekana

Hii Idi ya Tanzania ni uislam mpya au?
 
Wanabodi
Haya mambo ya mtu kusikia sauti, sio mambo ya ulimwengu huu wa mwili, haya ni mambo ya ulimwengu wa Roho.

Hii ni thread ya maono ya unabii, na sio utabiri na sio trends reading, ni unasikia tuu sauti inakuambia jambo fulani bila kuambiwa sababu na huwezi kuuliza, hivyo nami naomba kuwaeleza tuu sauti niliosikia na naomba msiniulize kitu kwasababu sio mimi ni sauti

Leo nilikuwa naandika bandiko fulani humu JF, ndipo ghafla nikaisikia sauti (voices from within) kuwa Rais wa JMT kwa 2025 should be Dr. Hussein Mwinyi kwa kipindi kimoja, then 2030 ndipo tuje na mgombea mwanamke!.

Sauti hiyo inamaanisha inamtaka Rais Samia awe ni Rais wa JMT kwa kipindi kimoja tuu hadi 2025. Sauti hiyo ikasema ni Rais Samia mwenyewe willingly anatakiwa kumuomba Dr. Hussein Mwinyi, 2025 aje kugombea urais wa JMT, kuimalizia awamu ya pili ya Samia, kwa awamu moja tuu,.

Na kipindi hicho cha 2025- 2030 ndio sasa sasa tufanye grooming ya Mwanamke atakagombea urais wa JMT kwa 2030.

Japo Tanzania, tulipania 2025 twende na mgombea mwanamke, na mimi niliunga mkono hoja hii Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!
kama hii sauti ni yake YEYE kweli, then unamaanisha kwa uchaguzi wa 2025, Tanzania tuna mgombea mmoja tuu Mwanamke, yaani the one and only ambaye ama anatakiwa na YEYE apumzike ampishe Mwinyi ama ...

Japo sio sio lazima kusema kila unachosikia, kwa sababu sometimes sio kila unachosikia from within ni sauti kutoka kwa Mungu au ni maono, sauti nyingine ni sauti za shetani tuu na sio sauti za Mungu, kama zilivyo ndoto nyingine, ni ndoto za shetani kama ile "ndoto ya Lema", ukisikia sauti ukahisi inaweza isiwe sauti ya Mungu, au ukiota ndoto ya jambo la ajabu ajabu ukahisi jambo hilo sio la kheri, sio lazima uliseme). Mfano ni tangu August 14, 2014 nilielezwa rais ajaye wa Tanzania ni Magufuli, na nilielezwa sababu kwanini ni Magufuli, nami nikaeleza humu lakini sikuzisema.

Hiyo 2014 wakati mimi nikisema mgombea wa CCM kwa 2015 ni Magufuli, wakati huo unaweza kukuta hata JPM mwenyewe alikuwa hajui kuwa ndiye yeye.

Hivyo hata sauti hii niliyoisikia leo, 2022, kuhusu 2025, usikute hata Samia mwenyewe hajui, na kwasababu ni Rais Samia aliyependekeza 2025 twende na mgombea mwanamke, unaweza kuta ni Samia anajipanga kuendelea, huku Dr. Mwinyi akiji set kwa his second term in Zanzibar, wala hahui kuwa yeye ndiye rais wa JMT, 2025.

Hata ile siku niliyoisikia sauti hii
Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini... Spika Job Ndugai hakujua hatakuwa Spika, wala Dr. Tulia hakujua kuwa yeye ndiye spika ajae.

Hata ile siku namzungumzia huyu DC, Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam DC mwenyewe alikuwa hajui, na watu humu wakanidhania mimi ni mtu wa kule naniliu na kudhani nimeleta za jikoni.

Hili sasa ni langu, hili la Mwinyi kuja huku, usikute ni mpango ya YEYE, kumfanya huyu jamaa Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Kabla Hajamwaga Sumu Hii
Hata wakati nikiandika hayo, Dr. Shein alikuwa hajui, hivyo saa hizi, usikute huyu jamaa wala hajajijua yeye ndiye rais ajaye wa Zanzibar

Hitimisho
Kwa vile mimi ni Msukuma, naweza kutuhumiwa ni sehemu ya Sukuma Gang wasiotaka Samia aendelee 2025 to 2030. Naomba kwanza niwathibitishie I don't believe hiki kitu kinachoitwa Sukuma Gang kina exist. Mimi ni Msukuma na sio Sukuma Gang, ila pia ni Mimi ndio nilimtabiria Samia urais wa JMT toka 2017, Pascal Mayalla alitabiri mwaka 2017 kuwa Samia atakuwa Rais wa JMT baada ya 2020
nikashauri Blaza asigombee 2020 ampishe Samia, but no one takes me seriously, you never know, kama JPM angeusikiliza ushauri wa bandiko hili Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!” nilishauri

probably ange...
Mwaka 2020 nikasema humu "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
nilisema

Hivyo it's up to Mama, kuna kitu nimeambia ni kwa nini Mama amuombe Mwinyi, ila sio lazima kusema kila kitu. Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?
Hivyo mpaka umelisikia hili nimelisema, ujue lina maslahi kwa Taifa.

Kitu muhimu ni nimesikia sauti, nimesema nilichosikia, nimetimiza wajibu wangu.

Paskali
(Mzee wa The Voices Within)
Mwinyi atapata resistance kubwa sana kwamba nchi imekuwa ya kifalme, 2030 tutampa Majaliwa
 
Hufahamu uislam na wala hujui uislam

Umezaliwa umekuta ndugu zako waislam ukapelekwa madrasa ndio mwisho wa unachokijua

Hakuna maandishi ya kiislam yanayomtaka mwanamke ajikweze na ajae matusi mdomoni

Mwanamke kamili wa kiislam Saudia anafundishwa kuwa mke wa pili, tatu na nne

Tanzania kuna mkanganyiko wa dini ya kiislam,

Angalia Iddi ya Tanzania, Tanzania kuna uislam mpya ambao haufuati taratibu za Mecca

Afrika mashariki, Tanzania wana Idi yao ambayo wanafuata mwezi wao tofauti

Swali, Nani anatafsiri upya dini hii Tanzania kuhusu kufunga na kufungua kwa waislam, Maandishi yaliyopo ni ya Abu Bakr

Na sasa waislam wamezidi kugawanywa kwa Misingi ya itikadi, Hakuna sherehe moja ya Idi tena Tanzania, Wa kweli wanafungua lakini sherehe haitambuliki na serikali

Wengine wananuna lakini hawana la kufanya wanafungua siku ya serikali

Hayo ndio mambo ya kujadili, Nani anatakiwa auone mwezi Tanzania, Mwezi upo Tabora na Tandahimba unaambiwa hujaonekana Endelea kufunga

Mwezi upo Mombasa na watu baadhi ya Tanga wanauona unaambiwa haujaonekana

Hii Idi ya Tanzania ni uislam mpya au?
Mkuu Maalim Airfryer , kwanza asante kuchangia bandiko hili, pili asante kwa ilmu kuhusu Uislamu Safi, ila hii ni nje ya mada, nakuomba fungua darsa humu, ili hawa wafia dini wa humu kama , Bibie FaizaFoxy wanyoroke.
Natanguliza shukrani.
P
 
Nikisoma katikati ya maandishi naona Pasco huna imani na huyu Mama.

Nikirejea uandishi wako wa siku nyingi humu na uzoefu wako wa siasa za ndani ndani huko naona tayari upepo wa nchi haupo pamoja na Mama 2025..

Na nikimwangalia Mama mwenyewe naona kabisa hana nguvu wala ushawishi wa kulazimisha kuendelea baada ya 2025.

Hasa akiambiwa mrithi wako huenda akawa "nduguyo" basi Mama hatakuwa na nongwa kabisa.
 
Hufahamu uislam na wala hujui uislam

Umezaliwa umekuta ndugu zako waislam ukapelekwa madrasa ndio mwisho wa unachokijua

Hakuna maandishi ya kiislam yanayomtaka mwanamke ajikweze na ajae matusi mdomoni

Mwanamke kamili wa kiislam Saudia anafundishwa kuwa mke wa pili, tatu na nne

Tanzania kuna mkanganyiko wa dini ya kiislam,

Angalia Iddi ya Tanzania, Tanzania kuna uislam mpya ambao haufuati taratibu za Mecca

Afrika mashariki, Tanzania wana Idi yao ambayo wanafuata mwezi wao tofauti

Swali, Nani anatafsiri upya dini hii Tanzania kuhusu kufunga na kufungua kwa waislam, Maandishi yaliyopo ni ya Abu Bakr

Na sasa waislam wamezidi kugawanywa kwa Misingi ya itikadi, Hakuna sherehe moja ya Idi tena Tanzania, Wa kweli wanafungua lakini sherehe haitambuliki na serikali

Wengine wananuna lakini hawana la kufanya wanafungua siku ya serikali

Hayo ndio mambo ya kujadili, Nani anatakiwa auone mwezi Tanzania, Mwezi upo Tabora na Tandahimba unaambiwa hujaonekana Endelea kufunga

Mwezi upo Mombasa na watu baadhi ya Tanga wanauona unaambiwa haujaonekana

Hii Idi ya Tanzania ni uislam mpya au?
Hilo tusi liko wapi? We fala nini? Uisla unaugumu upi mtu kuujuwa? Acha kutishia watu kwa Uislam.

Tunawafahamu nyinyi, hoja zikwashinda mnaanza kujaribu "character assassination.

Unataka kuuelewa Uislam unatakiwa upige goti kwangu nikupe darsa.

Sasa ya mwezi yanahusu nini hapa, na wewe kila unaloambiwa unakubali, ndio upoyoyo wenyewe huo, si kula tu ulikatazwa na nani? Wewe hata kwa mwezi wako kula tu. Rukhsa, au huelewi hilo? Kwanini ungoje mwezi wa kuambiwa?
 
Nikisoma katikati ya maandishi naona Pasco huna imani na huyu Mama.

Nikirejea uandishi wako wa siku nyingi humu na uzoefu wako wa siasa za ndani ndani huko naona tayari upepo wa nchi haupo pamoja na Mama 2025..

Na nikimwangalia Mama mwenyewe naona kabisa hana nguvu wala ushawishi wa kulazimisha kuendelea baada ya 2025.

Hasa akiambiwa mrithi wako huenda akawa "nduguyo" basi Mama hatakuwa na nongwa kabisa.
Huyo Pasco ni Msukuma na nani asiyeelewa kuna sukuma gang?

Huyu Pasco ni mnafik wa mwisho, fitina na majungu hajaanza leo huyo.
 
Unataka kuuelewa Uislam unatakiwa upige goti kwangu nikupe darsa
Mbona unajikweza kiasi hiki ?

Sasa ya mwezi yanahusu nini hapa, na wewe kila unaloambiwa unakubali, ndio upoyoyo wenyewe huo, si kula tu ulikatazwa na nani? Wewe hata kwa mwezi wako kula tu. Rukhsa, au huelewi hilo? Kwanini ungoje mwezi wa kuambiwa?
Bakwata ndio wenye hilo jukumu la kutangaza kuanza kwa mfungo au kumalizika kwake ili kuondoa mkanganyiko.
 
Nikisoma katikati ya maandishi naona Pasco huna imani na huyu Mama.

Nikirejea uandishi wako wa siku nyingi humu na uzoefu wako wa siasa za ndani ndani huko naona tayari upepo wa nchi haupo pamoja na Mama 2025..

Na nikimwangalia Mama mwenyewe naona kabisa hana nguvu wala ushawishi wa kulazimisha kuendelea baada ya 2025.

Hasa akiambiwa mrithi wako huenda akawa "nduguyo" basi Mama hatakuwa na nongwa kabisa.
Mkuu idawa , kwanza asante sana kwa mchango wako na uwezo wako wa kunisoma in between the lines, ila naomba nikuhakikishie, it's not my making, it's the voices from within!.

Sikukisema vyote nilivyo ambiwa, na hiyo sauti labda nikivisema vyote itasaidia kwa kuvi mitigate kabla ya 2025 ili Mama aendelee.

Kinachonifanya nisiseme kila kitu ni kwasababu kauli nyingine huumba!. Nisije nikasema humu, halafu yakatokea ya kutokea tukaaanza kunyoosheana vidole!.

Hata mimi kujiunga JF nikauli za wana JF
ile 2008 nikiwa naendesha bike Morogoro Rd mitaa ya Manzese, kuna mwana JF akanianzishia uzi kuhusu uendeshaji wangu wa bike.

Kilichofuata hata wiki haikupita... mimi chali!. Uzi ule wa kwanza ukafutwa na kupandishwa huu
Pascal Mayalla apata ajali..... na ndipo nami nikatua rasmi humu JF na baada ya mwaka nikatoa shukrani
Waraka wa Pascal Mayalla - Asanteni Sana!
from then mimi ni mtu makini sana

P
 
Back
Top Bottom