Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke

Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke

Mkuu sipingani wala sina shaka kabisa na maoni yako,
Mkuu Black BackUp , kwanza asante kuja uzi huu, unaogopwa kama ukoma!, pili nikupongeze wewe binafsi kwa kuwa very objective inquisitive, mimi nimejaliwa kipaji cha kitu kinachoitwa, graphology, nikisoma andiko la mtu, naweza kumbaini mwandishi kama ni akili nzuri au akili mbovu!, hongera sana!, wewe ni akili nzuri!.
lakin ukiangalia kwa ndaani zaidi kuna watu (wanaume wa shoka) kama kina Nchimbi, Makamba, nape na wengine wapo katika bench wanasubiri nafasi hii hasa kwa mwaka 2030. Huoni katika maono yako kama itaweza kuchafua hali ya hewa ndani na nje ya chama chao?
Hapana, haiwezi kuchafua, bandiko hili linasaidia ku open up possibilities, moja ya madhaifu makubwa kabisa ya CCM, ni kitu kinachoitwa mizengwe kwenye kumpata mgombea wake wa urais.

Uchaguzi wa 1995, JK ali team up na EL, wakakodi ndege moja, wakachukua fomu siku moja, wakazunguka pamoja kutafuta wadhamini, wakarejesha fomu pamoja siku moja, huku wamekubaliana, yeyote atakaye penya, mwenzake ni PM, hivyo wakaunda kundi la "Boyz II Men".

Mwalimu Nyerere akaingilia kati kwa hoja mbili za wazi na moja ya siri!, hoja ya kwanza ya Mwalimu, JK bado ni kijana sana!, ya pili ni zamu za siri za kupokezana, akitoka Mkristo, anakuja Muislamu, sasa ni zamu ya Mkristo hivyo JK, akapigwa zengwe, tupa kule!. Kwa EL, Mwalimu akampiga zengwe la wazi kuwa ni tajiri sana!, utajiri huu amepata wapi?!, zengwe la pili ambalo halisemwi popote, Rais wa Tanzania akiwa Mkristo, lazima awe Mkatoliki!, EL sio Mkatoliki!, Tupa kule!. Ndipo Mwalimu akamuibua Ben!.

Baada ya Boyz II Men kupigwa chini 1995, ndipo wakaasisi mtandao for 2005. Jambo la kwanza ni 2005 ni zamu ya Muislamu, JK ni Muislamu, hivyo EL akajitoa kwa 2005 kum support JK kwa makubaliano mawili.
1. EL atakuwa PM, 2. JK atakaa just for one term, na kumpisha EL 2nd term. Kikwazo pekee kwa JK 2005 ni the Zanzibar factor, pili ni zamu ya Zanzibar!. Aliyekuwa amepangwa kwa Zanzibar 2005 kumpokea Mkapa, huyo mtu alishughulikiwa!, na humu jf iliripotiwa!.
Baada ya JK kuingia hiyo 2005, kweli EL akawa PM, Mkwere auona urais mtamu, auache one term?!, akaamua no!, the only way ya kuendelea ni kumfix EL, mtandao, ukamtumia Spika 6, kumshughulikia EL, wakampigwa zengwe, wakamuweka pembeni!, kundi la Boyz II Men, zikavunjika!. JK akasail through, 2nd Term, na EL, akaamua 2015 atagombea!. Changomoto pekee kwa EL ni Catholicism!, mke wa EL ni Mkatoliki, akaandika kitabu na EL akawa ndie mchangiaji mkuu wa fundraising za wa Katoliki!.

Kwa uoga EL akiingia itakuwaje, Mtandao, ukaanza kumshughulikia, ndipo akatafutwa JPM, nikaripoti humu, Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli na pia nikawaeleza watu humu Elections 2015 - Edward Lowassa sio lazima yeye tu ndiye awe Rais wetu 2015, Rais wetu wa 2015 ni..., kweli siku ya siku EL alipigwa zengwe, nikawaambia watu humu Elections 2015 - Licha ya kukubalika, Jina la Lowassa halitafika hata CC!, na kweli JK akaingia kikao cha CC na majina mfukoni!.

Hizi zengwe za CCM zimekuwa zinakiumiza chama, hivyo ili kuzuia zengwe, mgombea wa 2025 akapitishwa kwa mserereko, na mgombea urais wa CCM 2025 ni Dr. Nchimbi, kama hapo kati hili jambo, Japo hakuna ajuaye sababu za kutwaliwa kaka, isipokuwa yeye, kuna watu saw it coming, wakasema, wakapuuzwa, akatwaliwa. Dada ukisikia usipuuze hili
halitajirudia!, hivyo 2030 is a done deal!.
P
 
Ngoja nisubiri naweza kuwa mimi japo miaka yangu ni michache sana kikatiba na sijawahi kuwa kwenye siasa ngoja nijipange
 
Mkuu kwa maono yako mpaka sasa rais samia hana habari juu ya jambo hili na sasa tunamwona anazunguka mikoani kwa maana ya ziara ya Rais lakin chini ya kapeti ni kampeni za chinichini...
Kwanza inaweza kuwa ni kweli Rais Samia hana habari, kwasababu yeye hajaambiwa, ndio maana anayafanya hayo anayoyafanya, mimi kazi yangu ni kuandika tuu na kushauri,
Ikifika kipindi cha kampen rasmi huoni katika maono yako kwamba itampa ugumu mrithi wake kukubalika na wanachi maana itakua kama kadandia tren kwa mbele?
Kili nilichokisema kwenye bandiko hili, kama ni sauti ya kwake YEYE mwenyewe, then Rais Samia ataambiwa, na litatimia, lani kwasababu CCM wameisha maliza kazi, akiisikia sauti wakati tayari ameshateuliwa, then utaratibu wameushafanya, atampisha Dr. Nchimbi, na ni yeye atambeba, ila pia kuna sometimes, huu uteuzi wa Dr. Nchimbi ndio utekelezaji wenyewe wa lile jambo lake, yeye atakuwepo kama fugure head tuu, halafu Dr, ndie atakuwa ana run the show!. Hakuna tatizo kabisa!.
P
 
Uchaguzi wa 1995, JK ali team up na EL, wakakodi ndege moja, wakachukua fomu siku moja, wakazunguka pamoja kutafuta wadhamini, wakarejesha fomu pamoja siku moja, huku wamekubaliana, yeyote atakaye penya, mwenzake ni PM, hivyo wakaunda kundi la "Boyz II Men
Asante sana Mkuu kwa kuendelea kunijuza kwa nyuzi zako za kibabe sana.
Kulingana na mfano wako uliotoa wa mwaka 1995 kunaonekana kulikua na mtu mmoja mweye say na final decider ambaye ni yeye. Hii itakaaje 2025, kulingana maono yako tuamini katika yeye ambaye ali team up na EL au yule YEYE mwenyewe?
 
Mkuu sipingani wala sina shaka kabisa na maoni yako, lakin ukiangalia kwa ndaani zaidi kuna watu (wanaume wa shoka) kama kina Nchimbi, Makamba, nape na wengine wapo katika bench wanasubiri nafasi hii hasa kwa mwaka 2030. Huoni katika maono yako kama itaweza kuchafua hali ya hewa ndani na nje ya chama chao?
Uliowataja wote hakuna hata mmoja atakuja kuwa rais wa Tanzania hata kama ni kwa wizi haitawezekana....period
 
Back
Top Bottom