Voices From Within: Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni, Kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani

K
Kaka naamini ni mmoja ya watu unaelewa vizuri sana mambo ya karma na jinsi inavyofanya kazi.
๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ....

Naam sababu ya kutokea jambo ni huyo aliyeruhusu na kadhalika kutotokea ni huyo pia.

Binadamu hukumu zetu zinaongozwa sana na nyakati zilizopita ila Mungu nafikiri anahukumu kwa wakati uliopo sasa hapo ndio pagumu kuelewa iweje mwenye historia ya uovu akubalike na Mungu kumbe Mungu anahusika na wakati uliopo na hata sekunde chache kabla ya Roho na mwili kuachana Mtu anaweza kuiona Mbingu kutokana na neema.
 
Ni kweli kabisa Mungu hutoa hukumu katika wakati uliopo sasa, haijalishi mtu alifanya makosa gani, ukitubu kabla hujafa, unasamehewa na unaingia peponi, ila kitu kikubwa zaidi ni "tunaokolewa kwa neema na sio kwa matendo". Neema hiyo imemshikia JPM.
P
 
Ndiyo maana Mungu akamtupilia jehanam
Mkuu Stuxnet , huyu mwamba hakutupwa jehanam, alipitia toharani na sasa yuko mbinguni peponi!.
Sisi Wakristo, tunaokolewa kwa neema na sio kwa matendo!.
P
 
ushahidi uwepo au usiwepo, ukweli ni kwamba nchi hii ilishawahi kutawaliwa na mtu katili sana ambaye anajutia alichokifanya huko kuzimu hata sasaivi mnavyoandika. Mwogopeni Mungu, na ninyi mlio karibu nao washaurini vyema.
Mkuu Yesu Anakuja, Huyu ni Mkatoliki, Mkatoliki akipata sakramenti ya Upako Mtakatifu kabla hajafa, dhambi zake zote zinakuwa zimeondolewa!, hivyo akifa, haendi kuzimu, anakwenda toharani, kisha anaingia mbinguni!, hivyo saa hizi yuko peponi mbinguni kwa Baba yake, yuko na Baba yake!.
P
 
ndugu yangu pascal, mwanasheria mwenzangu, hii ndio sababu huwa tunasema muokoke, muachane na imani potofu kabisa ya shetani, aliyowadanganya kwamba ukipata sakrament unasamehewa dhambi, au ukiombewa vizuri siku ya maziko unasamehewa dhambi, au ukifa watakuombea ukiwa kaburini ukasamehewa dhambi. hii haijathibitishwa na eneo lolote la Biblia, na ni uongo wa shetani.

Biblia inasema, saa ya wokovu ni sasa, nia uishi ukijua kuwa, baada ya kifo ni hukumu, hakuna kutubu wala kutubiwa, na kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe, padre hawezi kutubu kwa ajili yako ukasamehewa. huu ndio ukweli mchungu. hii ndio sababu imefanya mapadre wa katoliki wanaishi kama miungu watu, kwa sababu wanaamini wameshika funguo za kukufanya uende mbinguni au motoni kwa kukuombea ukifa, na ndio fimbo wanapigia watu wasiohudhuria jumuia, wanaweza kuamua tu kwamba hawakuziki, na wanaamini wakifanya hivyo hautaenda mbinguni. wakati wao weneywe ni watenda dhambi wakubwa,wazinzi na wachawi.

WAEBRANIA 9:27 imeweka wazi kwamba, "baada ya kifo ni hukumu", nafasi yako ya kutubu ni sasa, wewe binafsi kutengeneza mambo yako na Mungu, ikitokea umetoka hata hapo nje ukagongwa na gari ukafa kabla ya kutubu, kifuatacho ni hukumu, hata wakikuombea maombi miliono its a waste of time.

kwa sababu ni usiku sana,ngoja nikuache na mstari huo, kesho nitakuletea mingine, God willing.
 
Hata ya kutoka kwa kitabu cha Eric Kabendera๏ผŒ hoja za bandiko hili bado zinasimama kwa mujibu wa maelezo ya Eric mwenyewe
View: https://youtu.be/HfQqupIGlKM kuwa JPM alitenda kwa hasira๏ผŒbaada ya kutenda alijutia๏ผŒkwa sisi Wakristo Wakatoliki ukitenda dhambi๏ผŒukaenda kuungama๏ผŒdhambi zako zinaondolewa๏ผŒunatakasikaใ€‚

JPM siku za mwisho alitubu dhambi zake zote๏ผŒakasamehewa akapata sacrament ya mwisho ya upako mtakatifu๏ผŒ ndipo akatwaliwa๏ผŒ kwa vile wakati wa mpako mtakatifu ni tayari alikuwa kitandani๏ผŒthen alipotwaliwa alifikia toharani kwanza ndipo akaingia mbinguniใ€‚Hivyo JPM๏ผŒ yuko peponi๏ผŒpia anakisoma kitabu cha Eric๏ผŒ kama kuna uongo wowote mtu anamsingizia marehemu ambaye hawezi kujitetea๏ผŒsasa hivi mtu atanyakuliwa๏ผใ€‚
P
 
Frm saba saba special miaka ya 2005 +ad kuja kua chawa wa Siasa za Ccm

Wacha nisome komenti kuna ving sana vyakujifunza
 
Hii kisheria imekaaje!? Hawezi kishitakiwa na familia au serikali maana hizi ni Tuhuma nzito sanaa na kashifa kwa serikali. Vinginevyo labda kama kuna ushahidi wa kutosha.
 
Hii kisheria imekaaje!? Hawezi kishitakiwa na familia au serikali maana hizi ni Tuhuma nzito sanaa na kashifa kwa serikali. Vinginevyo labda kama kuna ushahidi wa kutosha.
EK ana ushahidi wa kuambiwa na mashuhuda, sisi waandishi tuna kinga ya kisheria, kutotaja ma source wetu inaitwa the confidentiality of the source, huyo aliyemwambia ni wale jamaa zetu wenye kinga ya kiofisi ya non disclosure, hovyo serikali ikimfungulia kesi ni itachafuka, inachoweza kufanya ni kuchutama tuu, msemaji
Wa serikali atakanusha tuu, lakini hakuna mashitaka yoyote yatafunguliwa.
P
 
Ila heko sana Godbless lema alituambia utabili wote juu ya kaka alietwaliwa (shetani akateseke mbwa yule)
Huwezi kumuita binadamu shetani, huwezi kumtukana mtu mbwa!.
P
 
Huwezi kumuita binadamu shetani, huwezi kumtukana mtu mbwa!.
P
Huwezi mpangia alieumizwa na aliye juu ya sheria ajilipie vipi na kiasi gani kwa namna gani ,kwan sifungwi na maadili ya dini bali katiba ,mbwa haijakaa sawa nafuta ni kenge.
Biblia imeonya vikali juu ya kuambatana na mtu mbaya

Avoiding association with sinners
  • Psalm 1:1: "Blessed is the man who walks not in the counsel of the wicked, nor stands in the way of sinners"

  • 1 Corinthians 5:11: "Do not associate with anyone who bears the name of brother if he is guilty of sexual immorality or greed"

  • 2 Corinthians 6:14: "Do not be unequally yoked together with unbelievers"

  • 2 Corinthians 6:17: "Come out from among unbelievers, and separate yourselves from them"
So kama mkristo mwenzangu weka mbali bawa lako na yule muovu watu tumezika ndugu zetu .
 
Voices from within-Advocate Mayalla
 
Voices from within-Advocate Mayalla
Voices from within ni kitu cha kweli, Mungu kweli yupo, ila pia na shetani yupo!, hivyo hizi voices from within, ni sauti ya YEYE aliye ndani yako!, ila pia hata yeye, naye pia yumo ndani yako, hivyo sauti nyingine zinaweza zikawa sio sauti za kwake YEYE bali ni sauti za yeye tuu!. Kama ni sauti ya YEYE, lazima itatimia!. Mfano mimi mpaka leo, mpaka kesho, bado naamini HII kitu ni sauti kwake YEYE!.
P
 
JPM alikuwa Rais katili kuwahi kutokea Tanzania, apumzike panapomstahili
 
Mshana Jr leo umeongea kama mtumish wa Mungu aliyepakwa mafuta. Ukiamua kujikita kusoma zaidi Biblia na kuifafanua unaweza ukawa mtumishi mzuri sana kuliko zile thread za ushirikina.

Mungu akupe neema yake.
 
Mshana Jr leo umeongea kama mtumish wa Mungu aliyepakwa mafuta. Ukiamua kujikita kusoma zaidi Biblia na kuifafanua unaweza ukawa mtumishi mzuri sana kuliko zile thread za ushirikina.

Mungu akupe neema yake.
Aamen๐Ÿ˜€๐Ÿ™๐Ÿฟ๐Ÿ™๐Ÿฟ๐Ÿ™๐Ÿฟ๐Ÿ’ช๐Ÿฟ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ