Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
Wanabodi
Angalizo
Kwa vile mimi mwenzenu humu, na niliisha wahi kuuliza kitu kwa kuandika, kitu hicho, kikaniletea matatizo nikaitwa hadi Bungeni Dodoma kuhojiwa na Kamati ya Bunge kwanini nimesema kile nilichosema?, nikajibu sijasema kitu chochote, bali ni nimeuliza kitu na alama ya kuuliza ilikuwepo!. Wabunge wale wa kamati ile, walipoangalia tena kile nilichoandika ndipo wakaiona hiyo alama ya kuuliza, kesi ikaishia hapo!. Hivyo ninapoandika kuuliza jambo lolote sensitive, nakumbushia na kusisitiza kuwa ni sijaandika statement yoyote, bali ni nimeuliza swali na alama ya kuuliza ipo!.
Bandiko hili pia ni la swali Voices from Within: Mauaji ya wananchi Dar, tusiwalaumu polisi, ni walikuwa wanatimiza wajibu wao tuu!, swali ni je amri ya kuua hao watu, ilitoka kwa muuaji huyu?. Hapa sijamtaja mtu yeyote kwa jina kuwa ndie muuaji wetu wa wale watu wa jiji la Darisalama, waliouliwa kama kuku katika maeneo, tofauti tofauti, lakini kwasababu mimi, kuna mtu namjua kuwa ni muuaji, na muuaji huyo, aliwahi kujitqmba kuwa ni muuaji na kutambia jinsi alivyomuua mtu mmoja kwa kumpiga risasi mbili za kichwa na risasi zile kumfumua kabisa kichwa pale pale na ikawa ni kifo hapo hapo!, kisha akajipongeza kwa kunywa bia mbili huku akiiangalia hiyo maiti ya huyu mtu, na nikamsikia mwenyewe kwa masikio yangu kupitia picha jongefu, akimuamrisha RPC fulani wa mkoa fulani, awaue vibaka wote!. Kwenye uzi huu sijamtaja muuaji huyo, kama ni yeye kama Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Jiji letu, bali nimeuliza kama ni yeye tena ndiye aliyempa amri RPC wa Kanda Maalum kufanya hicho kilichofanyika kwa watu wetu wa Darisalama ???
Hapa naomba alama ya kuuliza niibold kabisa, nisije itwa polisi nikatakiwa kuthibitisha kuwa nimesema fulani ni muuaji!, hapa mimi ni, nimeuliza tuu!.
Kitu Chenye Thamani Kuu Duniani ni Uhai
Kwenye nchi yoyote duniani, kitu cha kwanza chenye thamani kubwa kuliko kitu kingine chochote ni uhai wa binadamu, uhai wa mwananchi.
Mwananchi ndiye mwenye nchi, ndiye mwenye katiba, ndiye mwenye mamlaka kuu ya nchi ambayo ni katiba, na katiba hiyo inapata mamlaka kutoka kwa mwananchi.
Rais wa nchi na mihimili yake yote mitatu na serikali yake yote ni waajiriwa wa huyu mwananchi ambaye ndie mwenye mali, the big boss!, nani anatoa amri boss auliwe?.
Rais wa nchi anaajiriwa na mwananchi kupitia kura yake na na kumlipa mshahara wake na serikali yake yote kupitia kodi yake, hivyo the real big boss wa nchi ni mwananchi, rais wa nchi na serikali yake yote ni watumishi wa mwananchi, wanawezaje kumuua mwenye mali?
Uhai ndio haki kuu ya kwanza ya binadamu, tena kwa nchi yetu uhai ni unahesabiwa tangu ile ya kutungwa mimba ndio maana abortion ni kosa la jinai kwa nchi yetu, sisi ni pro life.
Kuna nchi ni pro choice, wao kufanya abortion ni legal kwa hoja kuwa wazaliwe watoto wale tuu wanaotakiwa, ikitokea mimba imetunga katika ile starehe tuu bila kupangwa, rukhsa kwenda kuiflush as if its nothing.
Ibara ya 14 ya Katiba yetu ina haki ya kuishi, hata hii adhabu ya kifo kwa watu kuhumiwa kifo kwa kunyongwa mpaka are, ni kinyume cha katiba, japo ipo kwenye katiba.
Adhabu ya Kifo
Hii adhabu ya kifo kwa mtu kunyongwa kwa kamba hadi afe, kwanza ni adhabu batili kinyume na ibara ya 14 ya katiba!, pili ni adhabu ya kikoloni ambayo lengo lake ni barbaric ili kuwaogofya wananchi, kwa serikali ya mkoloni maisha ya mtu hayana thamani, Tanzania baada ya kujipatia uhuru wetu tulitakiwa kuachana kabisa na hizi adhabu barbarian tulizo zikuta.
License to Kill
Serikali zote duniani zinatoa kibali cha kuua mtu yoyote ambaye ni tishio kwa usalama wa taifa au wa raia na mali zake, endapo njia nyingine zote za kumdhibiti zitashindikana.
Mtu pekee mwenye mamlaka ya kuruhusu mtu auliwe ni rais wa JMT kwa kusaini hati ya kifo, ideath warrant!
Watendaji wote wa serikali, wanatekeleza majukumu yao kwa niaba ya rais wa JMT, hivyo wakiua mtu yoyote kwenye utekelezaji wa majukumu yao, anayehesabika ameua ni rais wa JMT kwasababu yeye ndiye pekee mwenye kibali cha kuondoa uhai wa mwananchi kwa mujibu wa sheria!.
Jeshi la polisi na wana usalama, wamepewa mamlaka ya kutumia nguvu kutuliza ghasia lakini hawatakiwi kutumia nguvu kupita kiasi. Na ili kuepusha madhara ya kuwaua wasio husika, polisi na usalama huwatumia askari maalum wanaoitwa snipers ambao ni ma sharp shooters wa kulenga shabaha ili mlengwa tuu ndiye auliwe!.
Katika kutuliza ghasia, kuna mazingira fulani ambapo wanaruhusiwa kuua, na ikitokea watu ambao sio walengwa wameuwawa kwa bahati mbaya katika purukusha, wanatakiwa kufidiwa.
Je ni katika mazingira gani polisi wanaruhusiwa kuua?
Je kuwauwa waandamanaji, polisi wauwaji wale wamekidhi vigezo vya to be linceced to kill?. Kama hawajakidhi, wanashitakika!.
Amri ya Kutotoka Nje Baada ya Saa 12:00 Jioni.
Hii ni amri kama ya kutangaza hali ya hatari ambayo mtu pekee mwenye mamlaka hii ni rais wa JMT, na amri hii kwa mikoa inatolewa na RC, ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, hivyo japo amri ile ilitolewa na RPC Kanda Maalum, ilitokana na kikao cha dharura cha ulinzi na usalama, IGP ana Juliana na kumjulisha CinC kwasababu wote wanatimiza majukumu yao kwa niaba ya rais wa JMT.
Maamuzi ya Kikao Cha Ulinzi na Usalama
Kwa kawaida majadiliano na maamuzi ya kikao cha Kamati za ulinzi na usalama la mikoa na wilaya huwa ni siri na baada ya hapo kila mjumbe anapeleka taarifa kwa mkuu wake, RPC anapeleka kwa IGP, RSO anapeleka kwa DGIS, yule mjeshi anapeleka kwa CDF na wote lazima wanamjulisha CinC pamoja na maoni yao hivyo rais wa nchi yuko well informed kwa hot line yake ya kila kinachotokea ikifuatiwa na taarifa ya maandishi kwasababu japo tuna egovernment, lakini serikali yetu bado inafanya kazi kwa black and white, yaani kwenye makatatasi, hata ukituma email, inaprintiwa inaandikiwa Pokémon ndio inashighulikiwa.
Hii ina maana yale mauaji yalipangwa, amri halali ilitolewa kwa maandishi.
Hii maana yake uamuzi wa zile patrol za usiku mitaani na ku m shoot mtu yoyote atakaye onekana nje, yalifanywa kwenye kikao kikao halali cha ulinzi na usalama, hivyo nawaomba sana, tusiwalaumu polisi wetu, wao ni wawekezaji tuu, wa kulaumiwa ni aliyetoa amri ya kuua Watanzania, au mwenye uwezo wa kuzuia Watanzania wasiuliwe lakini hakutimiza wajibu wake.
Mauaji ya Mwanza na Shinyanga ya Mwaka 1976.
Mwaka 1976 kulitokea mauaji ya kikatili ya vikongwe mikoa ya Mwanza na Shinyanga wakituhumiwa kwa uchawi kutokana na kuwa na macho mekundu kutokana na moshi wa kuni za kupikia.
Kikafanyika kikao chini ya Rashidi Kawawa akiwa Makamu wa pili wa Rais na Waziri Mkuu, waziri wa usalama, waziri wa mambo ya ndani, IGP, DGIS, RC Mwanza na Shinyanga, RPC na RSO, maamuzi yakapitishwa.
Kukafanyika kamata ya mamiq ya watu wakiwemo waganga wa kienyeji, katika mahojiano na polisi, eneo la Kigoto Mwanza, watuhumiwa wawili, Masaga Makhula Mazengenuka na Isaac Ng'wana Nkhoboko, walifariki dunia.
Taarifa zilipomfikia Rais Nyerere, kiliwaka, Mwalimu alikasirika sana, akaanza na Kawawa, akamtoa kwenye umakamo wa rais na waziri mkuu, akawa waziri asie na wizara maalum, Sokoine akaingia, akatoa amri nikute mezani kwangu kabla ya saa 10 jioni, barua za kujiuzulu waziri mambo ya ndani, Ali Hassan Mwinyi na Waziri wa usalama Peter Siyovelwa. Piga chini IGP, Samuel Pundugu, DGIS Emelio Mzena, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Peter Kisumo,na wa Shinyanga.
Kisha staafisha kwa manufaa ya umma RPC, OCD. RSO, DSO wa Mwanza na Shinyanga, kisha maofisa wote hao wakashitakiwa kwa kesi ya mauaji Mwanza na Shinyanga.
Hiyo ndivyo awamu ya Nyerere ilithamini maisha ya watu, yaani vifo vinne tuu vya mahabusu mikononi mwa polisi, angalia viliwagharimu watu wangapi?
Idara ya Usalama wa taifa ikavunjwa na kuundwa upya kwa sheria mpya, tukaleta sheria ya magazeti ya 1976.Thread 'TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!' TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!
Waliofanya Mauaji Haya Wanaweza Kushitakiwa
Kama mauaji ya Mwanza na Shinyanga watu walifutwa kazi, wa kujiuzulu walijiuzulu, waku shitakiwa walishitakiwa, kitendo cha hakuna aliyejiuzulu mpaka sasa, ina maana polisi wetu walitumwa kufanya hicho walichokifanya, tusiwalaumu na kuwaonea bure.
Juzi nilipoona video ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka na wananchi wake wanalia na kusali kwa kifo cha mwananchi wake mmoja na kuwaombea waliokufa, nikajiuliza Mtaka angekuwa ndie RC DSM, angewaruhusu polisi wafanye unyama ule?.
Ndipo nikaisikia ile sauti toka ndani yangu, the voices from within, kuwa aliyetoa amri kwa polisi, piga risasi ua mtu yoyote atakaye onekana nje baada ya saa 12:00 jioni ni mtu fulani!.
Ilipaswa kuwatendea Haki Watanzania, lile tangazo la amri ya kutotembea, lilipaswa liandamane na uamuzi wa kikao kuwa atakayukutwa nje baada ya saa 12: 00 jioni, atauwawa kwa kupigwa risasi.
Baada ya sauti hiyo kunitajia ni fulani, ndio nikakumbuka, niliwahi kuandika kitu humu kumhusu RC fulani kuwa ni muuaji, aliwahi kumiminia kibaka fulani risasi mbili za kichwa at close range hivyo zikakifunua na kukisambaratisha , kisha akaita polisi, wakati akiwasubiria polisi waffle kuichukua ile maiti ya yule kibaka aliyefumuliwa kichwa kwa risasi mbili, akachukua bia mbili kwenye friji, na kujipongeza huku akiangalia hiyo maiti ya kibaka!.
Nikauliza humu Thread 'This man is either a sadist or alimuua kibaka, akanywa bia kusherehekea?' This man is either a sadist or alimuua kibaka, akanywa bia kusherehekea?
Kwenye bandiko hilo nilisema
Je inawezekana ushauri kama huo ndio aliutoa kwa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Dar es Salaam?, na baada ya mauaji yote hayo, huyu jamaa had the audacity kuitisha press conferences na kusema polisi haijaua mtu!, hivyo mauaji yale ni polisi wetu walikuwa wanatimiza tuu wajibu wao ?.
Iundwe Tume ya Kijaji Kuchunguza
Ikiundwa tume ya kijaji kuchunguza mauaji ya raia wasio na hatia kufuatia kilichotokea, ushahidi utambaini huyo muuaji aliyetoa amri ya kuwaua wananchi wana Darisalama.
Kama Waandamanaji Wameshitakiwa, na Wauaji Pia Washitakiwe!.
Kwa vile waandamanaji wameshitakiwa kwa makosa ya uhaini, maandamano yale sio chanzo, ni matokeo tuu, naomba tutibu na chanzo, kilicho sababisha maandamano hayo, na kuwashitaki waliotoa amri ya kuwaua wananchi wetu. Thread 'Haki Huinua Taifa. Kilichotokea ni matokeo na sio chanzo. Kama matokeo yanapandishwa kizimbani na chanzo pia kipandishwe!' Haki Huinua Taifa. Kilichotokea ni matokeo na sio chanzo. Kama matokeo yanapandishwa kizimbani na chanzo pia kipandishwe!
Kama Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alikasirika vile kwa vifo 4 tuu mikononi mwa polisi, Tunamuomba Rais wetu mpendwa Dr. Samia Suluhu Hassan, na yeye pia akasirike kama Nyerere, awawajibishe wasaidizi wake waliosababisha kilichotokea, ila ikitokea na yeye akakaa kimya, yaani ameridhika, hii maana yake itakuwa ni... naomba nisimalizie, ila tusiwalaumu bure polisi wetu, wenzenu ni walikuwa kazini, wakitekeleza majukumu yao kwa kutimiza amri halali.
If this be the case, hata hawa wanaitwa wasiojulikana, kwa vitendo wanavyo vifanya, vya utekaji, utesaji, kupoteza watu na mauaji ya wanaotekwa, kuendelea kuwalaumu ni kuwaonea bure, wao ni watu wa kazi tuu kutekeleza amri halali ya wakubwa wao wa kazi kama nilivyoeleza hapa. Thread 'Kama Walioua ni "Wasiojulikana" Then Karma, Albadir Itawahusu, ila kama ni 'Wasiojulikana', Hata Albadir Haisaidii Kitu, Wametimiza Tuu Wajibu Wao!' Kama Walioua ni "Wasiojulikana" Then Karma, Albadir Itawahusu, ila kama ni 'Wasiojulikana', Hata Albadir Haisaidii Kitu, Wametimiza Tuu Wajibu Wao!
A Way Forward
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali

Wanabodi,
Siamini ninachokisikia hapa kwa kiongozi
Japo wote tunamasikio inawezekana sio wote tunaweza kusikiliza kitu tukasikia, hivyo kwa faida ya wengine naomba kusema kwa kifupi tuu mimi nilichosikia na kilicho nifanya nipandishe bandiko hili.
Kiongozi huyu anasema kibaka akiingia kwako hata kama ni kuiba chumvi, anakuwa ameomba mambo matatu.
1. Ameamua kuiba
2. Ameamua kuua
3. Ameamua kuuwawa
Amewaambia polisi wa mkoa wake kuwa kufuatia magereza kufurika, wayajibu maombi ya vibaka wote mkoani kwake kwa kuwapatia ombi lao la tatu yaani wauwawe!.
Kwa vile huyu ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, ndie mwakilishi wa rais, hapa amewapa polisi amri ya a license to kill vibaka wote!. Hivi ndivyo katiba aliapa kuitekeleza inavyosema?.
Kubwa kuliko ni akajitolea mfano yeye mwenyewe jinsi alivyomuua kibaka aliyevamia nyumbani kwake kwa kumpiga risasi mbili za kichwa na kufa papo hapo, na yeye ili kukamilisha furaha yake kwa kufungua bia moja kunywa kwa kujipongeza huku akiitazama maiti ya kibaka alimfumua kichwa!.
Hivi kweli Tanzania tumefikia hapa, kiongozi wa umma, senior public servant anatoa amri ya summarily killing ya kibaka aliyeiba chumvi?, na kujitapa yeye aliua kibaka na kujipongeza kwa kunywa bia!, na bado yuko ofisini!.
Kwa watu wanaojua kitu kinachoitwa psychoanalysis ya binaadamu, unaweza kumbaini a person of unsound mind kwa jinsi anavyoongea.
Kwa jinsi mtu huyu alivyoongelea hili tukio la kumuua kibaka na Kusherehekea kwa kunywa bia, I seriously doubt the soundness of his mind, this is a psychopath or a sadist!.
Naombeni sana msi question mamlaka yake ya uteuzi huwa inawaokotaga wapi watu kama hawa, kwa sababu huwa hakuna kipimo cha soundness of persons state of mind kabla ya uteuzi, hivyo nina amini kabisa alipoteuliwa, mteuzi hakujua his state of mind ya mteuliwa huyu!.
Kwa vile state of mind is not static, ni dynamic, inawezekana kabisa wakati anateuliwa he was OK, akaja kubadilika mbele ya safari, kama hata baada ya kuyasema haya ataachwa aendelee tuu kuwako ofisini, huu sasa ndio utakuwa uthibitisho kuwa hali hii inafahamika vyema kwa mamlaka yake ya uteuzi, hivyo mwacheni apige kazi.
Kitu nitakachowaomba wana jf wenzangu mfuatilie, ni kitu kinachoitwa Karma kinavyoshughulikia watu kama hawa, hivyo bandiko hili liwekeni pending kwenye kumbukumbu zenu, ili siku karma itakapo anza to take its toll kwa ma psychopath kama hawa kwa kumshungulikia, mkumbuke kuna watu humu tuliona na tukasema kabla.
Psychoanalysis ya ma psychopath, na ma sadist, kwa kadri anavyofanya mauaji ya ki sadist, na kuendelea ku practice sadism huku akiachwa bila kubainika, ndivyo anavyozidi kuwa blood thirsty hadi atafikia stage ya kuwa na insatiable blood thirsty appetite hivyo atakuja kupiga tukio kubwa zaidi na zaidi la ajabu, na ndipo watu watashituka na kubaini kuwa mtu huyu is a psychopath!.
It's only a matter of time.
Paskali
Je inawezekana ushauri kama huo ndio aliutoa kwa Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Dar es Salaam?, na baada ya mauaji yote hayo, huyu jamaa had the audacity kuitisha press conferences na kusema polisi haijaua mtu!, hivyo mauaji yale ni polisi wetu walikuwa wanatimiza tuu wajibu wao ?.
Iundwe Tume ya Kijaji Kuchunguza
Ikiundwa tume ya kijaji kuchunguza mauaji ya raia wasio na hatia kufuatia kilichotokea, ushahidi utambaini huyo muuaji aliyetoa amri ya kuwaua wananchi wana Darisalama.
Kama Waandamanaji Wameshitakiwa, na Wauaji Pia Washitakiwe!.
Kwa vile waandamanaji wameshitakiwa kwa makosa ya uhaini, maandamano yale sio chanzo, ni matokeo tuu, naomba tutibu na chanzo, kilicho sababisha maandamano hayo, na kuwashitaki waliotoa amri ya kuwaua wananchi wetu. Thread 'Haki Huinua Taifa. Kilichotokea ni matokeo na sio chanzo. Kama matokeo yanapandishwa kizimbani na chanzo pia kipandishwe!' Haki Huinua Taifa. Kilichotokea ni matokeo na sio chanzo. Kama matokeo yanapandishwa kizimbani na chanzo pia kipandishwe!
Kama Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alikasirika vile kwa vifo 4 tuu mikononi mwa polisi, Tunamuomba Rais wetu mpendwa Dr. Samia Suluhu Hassan, na yeye pia akasirike kama Nyerere, awawajibishe wasaidizi wake waliosababisha kilichotokea, ila ikitokea na yeye akakaa kimya, yaani ameridhika, hii maana yake itakuwa ni... naomba nisimalizie, ila tusiwalaumu bure polisi wetu, wenzenu ni walikuwa kazini, wakitekeleza majukumu yao kwa kutimiza amri halali.
If this be the case, hata hawa wanaitwa wasiojulikana, kwa vitendo wanavyo vifanya, vya utekaji, utesaji, kupoteza watu na mauaji ya wanaotekwa, kuendelea kuwalaumu ni kuwaonea bure, wao ni watu wa kazi tuu kutekeleza amri halali ya wakubwa wao wa kazi kama nilivyoeleza hapa. Thread 'Kama Walioua ni "Wasiojulikana" Then Karma, Albadir Itawahusu, ila kama ni 'Wasiojulikana', Hata Albadir Haisaidii Kitu, Wametimiza Tuu Wajibu Wao!' Kama Walioua ni "Wasiojulikana" Then Karma, Albadir Itawahusu, ila kama ni 'Wasiojulikana', Hata Albadir Haisaidii Kitu, Wametimiza Tuu Wajibu Wao!
A Way Forward
- Majaji walikuwa wanateuliwa na rais kwasababu hatukuwa na wanasheria wa kutosha, lakini sasa Tanzania, tuna wanasheria wengi wa kutosha, hivyo nafasi zote za majaji hadi Jaji Mkuu zitangazwe, wanasheria wenye sifa waombe, watakao kidhi vingezo, ndipo rais apelekewe majina kuteua.
- Ofisi ya DPP ipunguziwe mamlaka ya kuwa ndicho chombo pekee cha kuendesha mashitaka ya jinai, Tanzania tuanzishe Private Investigations Bureaus ili inapotokea matukio ya kihalifu kama kupotea kwa Ben Saanane, Azory Gwanda, shambulio la Lissu, kupoea kwa Soka, Mdude, na kutekwa kwa Humphrey Polepole, tunaona serikali inavyokumbwa na kigugumizi kufanya uchaguzi, Watanzania wawe huru kuwatumia private investigators kuchunguza na kumpa DPP kufungua kesi.
- Tuanzishe Private Prosecution Bureaus, na kuifuta ile sheria ya kuomba kibali kwa DPP kuishitaki serikali, ili serikali yetu ikifanya madudu kama mauaji haya yaliyotokea, private investigators wachunguze na private prosecutors waishitaki serikali mahakamani by then majaji sio wa uteuzi wa hisani ni competent walioomba kazi.
- Ikithibitika kuna watu sio waandamanaji, wameuliwa kwa makosa, serikali inashitakiwa mahakamani na kulazimishwa kulipa fidia
- Kwa vile haya maandamano ya kupinga uchaguzi mkuu sio chanzo bali ni matokeo tuu, damu zisizo na hatia, zitafidiwa na karma, kupitia private investigations tunaweza kuchunguza kukibaini chanzo, na private prosecution tukawashitaki mahakamani hao wasababishi na kulazimishwa kulipa fidia kwa uharibifu wote wa mali uliotokana na vurugu zilizosababishwa na maandamano hayo.
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali