Voices From Within: Sultan Jamshid bin Abdullah Al Said atafurahi zaidi kama atarudi Zanzibar. Rais Samia, Rais Mwinyi, sameheni, utabarikiwa sana!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995

Wanabodi,​

Baada ya kuisoma hii story hapa chini, nimeisikia sauti ya ndani yangu, the voices from within ikiniambia huyu Sultan Jamshid bin Abdullah Al Said, ambaye alizaliwa tarehe 16 Septemba 1929 na kuwa Sultan wa Zanzibar baada ya kifo cha babake, Abdullah Bin Khalifa mwezi Julai 1963, sasa akiwa na umri wa miaka 95, sauti hiyo imeniambia huyu Sultani anatamani sana kurejea Zanzibar, kuja kukamilisha ile safari..., na kuwa atafurahi sana, na atakuwa na amani sana, iwapo kama ile siku, itamkuta akiwa Zanzibar mahali alipozaliwa!.

Natoa wito kwa Rais Samia, na rais Mwinyi, kufanya application ya zile 4R za Rais Samia kwa kumsamehe, kumjengea mazingira wezeshi arejee Zanzibar, ili ile siku yake ikifika, ifike ikimkuta akiwa Zanzibar, mahali alipozaliwa!.

Huko nyuma niliandika Dear Mama, Can you Offer An Unconditional Amnesty to All Zanzibaris Waliokimbia After Revolution, Incl Sultan, Be Free to Return & Start Afresh?

Hili likifanyika, then lifuatiwe na kuundwa kwa truth and reconciliation commission kama ile ya South Africa, Rais Samia na rais Mwinyi, mtabarikiwa sana for healing machungu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, na Zanzibar itabarikiwa sana!, ambapo wapinzani wakishinda, watapewa. Kila mtu mwenye akili timamu anajua kuwa wapinzani huwa wanashinda lakini hawapewi kwa uoga wa kitakachofuata!, hata uchaguzi wa 2015 ni CUF ilishinda Zanzibar kidume akapindua meza, Elections 2015 - Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar, Maalim Seif na CUF ndio walioshinda

The story ni C&P from BBC Swahili.

Jamshid bin Abdullah Al Said: Fahamu aliko Sultani wa mwisho wa Zanzibar​

29 Septemba 2020
Imeboreshwa 12 Januari 2021


CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES: Maelezo ya picha, Jamshid bin Abdullah Al Said
Rejea za Mwandishi kuhusu Zanzibar
Ombi kwa Rais Samia ni kufuatia Ombi hili Watanzania tumshukuru Mungu kupata mtu mwenye moyo wa kusamehe. Je, tumuombe asamehe tu bila kuombwa msamaha au akomae naye? ambapo Rais Samia alimsamehe mtu bila kuombwa msamaha. Hivyo anaweza kabisa kumsamehe Sultan Jamshid bila hitaji la Sultan huyo kuomba msamaha.

NB. Kuna gaps nimeziacha, ili ujumbe huu uwafikie wale tuu wenye uwezo to read in between the lines!.

Nawatakia Mapumziko mema ya maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Paskali.
 
Mmh hii kali sasa!! Tumsamehe sultani au Yeye atuombe msamaha sisi kwa kuwafanya babu zetu vinyago

Sultani anakumbukwa tena kwa mara ya kwanza basi ujue maisha yamekuwa magumu sana huko zenj

Hawa si ndio walioleta mambo ya LGBT zanzibar kwa wakati huo na kuyarasimisha kabisa

Mkuu Pascal,Kwani huelewi kwanini mambo ya kinyume na maumbile yameshamiri zanzibar? Chanzo ni hao akina sultani

Huyo sultani alipaswa kuwaomba msamaha wanzanzibar kama utawala wa kibelgiji huko kongo

Tatizo la zanzibar la kimaadili hata Rais Samia alishaliongea kuwa kuna shida kubwa zanzibar ya LGBT ingawa hakutaja chanzo kwa kuheshimu diplomasia

Cha kushangaza na kusikitisha unakutana na msukuma huko zanzibar mweusi kama mkaa lakini anajifanya na yeye ni mwarabu na kudharau wasukuma wenzake wa shinyanga na mwanza

Lakini kwa kuwa wenyewe wamesahau mateso ya sultani na bado wameendeleza LGBT hakuna haja ya sultani kutuomba msamaha bali akaribishwe tu kuendeleza alipoachia kwenye LGBT

Ikitokea kura ya maoni na ukawauliza wanzanzibar wanataka wawe Oman au Tanganyika watachagua Oman ,

Hawa unaowaita weusi wajukuu wamsamehe sultani kwanza ndio wanakanda vichogo vionekane kama sultani

Unakutana na mtu amekanda chogo aonekane kama sultani ,
 
Historia ya sultan huyu na maisha yake baada ya mapinduzi na kuhamia uhamishoni ni ya majonzi na majuto.Ni vema akakaribishwa zanzibar kama Bado yu hai huenda nafsi yake ikapata faraja na inawezekana akataman kufia Zanzibar
 
na kisiwa hicho kilikuwa chini ya utawala wa Uingereza baada ya kifo cha sultan Bargash bin Said
Hapa kuna gap na hapa ndio kiini cha Mapinduzi kilipoanzia Mwingereza kuacha Uhuru chini ya Sultan na Sultan akampa M Shamte (Mpemba/Mshirazi) madaraka,

Nilikua sijui kwamba washirazi ndio wa Pemba yaan hili neno washirazi kwenye neno Afro-Shiraz Party limenipigisha msamba sana kwenye uwezo wangu wa kufikiria yaan hii neno Shiraz ndio ukawa misamiati mgumu kumbe wanakwambia ni wa Persia sijua walitoka ghuba ya uajemi walikua waajemi kutoka Iran mara walikua huko Shiraz Iran wakahamia pwani Afrika Mashariki miaka elfu 3 iliyopita mara ni watu wa dhehebu la Shia mara ni wale waliounda vyama vya ZNP na ZPFP/ZPPP mara ni wahizbu lakini kumbe wanazingumziwa wa Pemba
 
Acha kwanza sauti zako nyingine zikamilike, unatuchanganya sasa.
 
Huu sasa uchuro.
 
Hapo ndipo ule MSTARI MWEKUNDU unapita kati ya Unguja na Pemba!!!.
 
Walio hasiwa, walioamriwa kudondoka kwenye minazi, waliotumbuliwa mimba, waliotoswa baharini na hawa waarabu nani anawaombea dua, nani anawafidia hata kwa kufikirika tu, nani anawakumbuka, nani anajali basi?? Leo unataka kurejesha kumbukumbu mbaya miongoni mwa jamii?? Afterall huko aliko bado ni kwao.
 
Kama anatakiwa asamehewe je kosa lake ni lipi?
JokaKuu zitto junior Nguruvi3 Mohamed Said
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…