Volkswagen Golf - Mkombozi wa Wanyonge!

Volkswagen Golf - Mkombozi wa Wanyonge!

We jamaa una madini sana.

Japo unayaachia kidogo kidogo, humohumo tunaunganisha dots.

Ila shida yangu kubwa kuhusu S.A ni usalama.
Mkuu usisite kuniuliza hapa hapa nakupa address ya chochote unachotaka huko kama ukiweza kwenda unaenda na hotel salama za kufikia huko Forsberg na tax driver alie muaminifu mimi napakia vitu vyangu huko miaka yote Mkuu usalama mbona Tanzania ndio hatari zaidi polisi wanaua kwa 70M wakati SA watu wanaingia na pesa nyingi sana na maisha yanaenda ni ngumu wale wahuni kumuibia mtu wasiemjua labda ulengeshwe na mtu wako...na SA matajiri ni wengi mpaka uje uibiwe wewe sio leo na pia ubebi hela unalipa kwa swift code tuu ila unatakiwa ushuke ili ujue unaofanya nao kazi wengine wametapeliwa kwa kuwalipa wahuni wa mtandaoni..
 
SA ukiyakanyaga huko mamelodi hata kama huna kitu unaweza kuuawa maana hawataamini kwamba mgeni harafu huna kitu..yapo maeneo ni hatari sana ila kwa wafanyabiashara hawafiki huko hata uende miaka yote utasikia tuu kama huko Soweto utaenda kufanya nini...
Mkuu usafiri wa meli kuleta hizo spair ukoje ?
 
Mkuu usafiri wa meli kuleta hizo spair ukoje ?
Meli unanunua unalipia wanaosafirisha mpaka Durban ports ingawaje wapiga hesabu wengi wanasafirisha kwa maroli ya kukodi au kulipia Kg kadhaa maana wanachaji 30 rand kwa kilo na ushuru wanalipa wenyewe kama una uwezo unanunua truck yako hata tani 7 au 10 inakua inabeba mizigo yako tuu..iwe car parts,mablangeti,vyombo au electronics ni wewe tuu na kodi vinalipika kwa wauzaji wa pombe wananunulia messina border hapo au Kemptoni park(Johannesburg) na VAT wanarudisha kwa mizigo inayotoka nje..urudishaji wake inatakiwa uonyeshe karatasi uliyolipia kodi Tanzania unawatumia email utaipata ulirudi trip ingine au unanunua kwa dealer wa pale yeye anakupa asilimia kadhaa sio zote..
 
Hio gari hapo pichani ni gari ya aghali kuimiliki wala sio ya wanyonge😅 ingekuwa starlet sawa ningekubali!
Hio kubadili set ya shock absobers tu inaweza fika million na ushee!
Mwambie huyo..kuna jamaa yangu aliishia kulifunika na turubai uwani kwake!
 
Back
Top Bottom