Sijui budget yako, na unataja nunua used Tanzania au unaagiza nje, na umepanga kutumia mjini au masafa ila izo gari zote ni nzuri sana, ingawa MIMI ningeenda BMW X5.
Kama umepanga kuspend between Mil 25-30 hivi BMW E53 ingefaa. Kuna wide range ya choice ya engine size hapa kuanzia 3.0L 4.4L 4.6 hadi 4.8L na zipo i6 hadi v8 na zaidi kuna diesel models, so wewe tu uchaguzi wako. Ni gari nzuri, ndio BMW X ya kwanza kabisa kabla ya hao X3, X6. Ilitengenzwa enzi zile BMW inawamiliki Land Rover so inashare some components with Range Rover HSE.
Ndani haina mbwembwe nyingi sababu ya uzamani but can be upgraded.
Kama budget kubwa zaidi basi E70 itakuhusu ingawa andaa hela kubwa above 40M. Nayo nzuri sana na zina technology ya xDrive kutoka BMW, unaweza bahatika ukapata X5M performance. Engine size ni sawa tu E53 ingawa zimeongezeka options za Twin Turbo.
Hizi F15 ni more advanced na bei zake zitakua mbaya zaidi kwakua ni very recently, 2014 ndio zimeanza kuingia sokoni so sizijui.
Sasa usichanganyikiwe na kujua aina ya BMW unayoinunua mkuu, hawa jamaa wana nomenclature yao kidogo inasumbua kichwa. Kwahiyo mfano ukiona kwenye BMW X5 ubavuni kwenye mlango wa mbele pana xDrive 30d iyo gari ni diesel, ina xdrive technology na engine size yake ni 3.0L. ukiona kuna herufi i hafu maybe 4 or 6 (i6 au i4) ujue cylinders zake ni straight inline, yaani izo cylinders zipo kwenye mpangilio wa mstari mnyoofu. hazijakaa V shaped. BMW zingine kama tulivosema zina V8 yaani cylinders zimekaa in V shaped, 4 zipo upande huu na 4 mwingune
Sijui kama nimesaidia but nimesema nnayoyajua ingawa nimemix sana