Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 yanayotarajiwa kufanyika nchini Morocco kuanzia tarehe 21 Desemba 2025 hadi 18 Januari 2026, yamefungua rasmi milango ya volunteering program. Takribani watu 4,000 wanahitajika kushiriki katika maandalizi na uendeshaji wa mashindano haya makubwa ya kandanda barani Afrika.
Programu hii ni kwa wote wenye umri wa kuanzia miaka 18 na zaidi, bila kujali uraia. Hii ni nafasi ya kipekee ya kupata uzoefu wa kimataifa, kujifunza vitu na stadi mpya, na kushiriki katika tukio la kihistoria la michezo. Wajitoleaji watashiriki katika maeneo mbalimbali ikiwemo **utoaji wa huduma kwa mashabiki, mawasiliano na vyombo vya habari, mapokezi ya wageni, usaidizi wa huduma ya kwanza first aid response, pamoja na kazi za uendeshaji na uratibu wa mashindano.
Wale watakaochaguliwa watapewa mafunzo rasmi kabla ya mashindano kuanza, sare kamili za AFCON, na vyeti vya kushiriki. Aidha, watakuwa sehemu ya mtandao wa kijamii na kitaaluma unaowaunganisha na vijana wengine kutoka nchi tofauti za Afrika.
Mchakato wa maombi upo wazi sasa mpaka 8 Oktoba 2025 kupitia tovuti ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) na Kamati ya Maandalizi ya Morocco. Waombaji wanahitajika kujaza fomu rasmi mtandaoni, kuonyesha nia yao, maeneo wanayotaka kushiriki, na kujitolea kuhudhuria mafunzo.
Kwa vijana wa Kitanzania, hii ni fursa adimu ya kushiriki moja kwa moja katika historia ya michezo barani Afrika. Ukipata nafasi hii, hutakuwa shuhuda tu wa AFCON 2025, bali pia sehemu ya roho na mafanikio yake.
INGIENI HAPO MSISUBIRIE TFF WAJE WALETE TANGAZO WAKATI TAYARI WATU WAMEANZA KUFANYA APPLICATION. AMA CAFONLINE.