Voyager 1: Chombo cha binadamu kilichosafiri mbali zaidi angani

Voyager 1: Chombo cha binadamu kilichosafiri mbali zaidi angani

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014
Voyeger 1.png

Chombo cha anga cha Voyager 1, kilichozinduliwa na Shirika la Anga la Marekani (NASA) mwaka 1977, kinaendelea kushikilia rekodi ya kuwa chombo kilichotengenezwa na binadamu kilichosafiri umbali mkubwa zaidi kutoka Duniani. Chombo hicho kimevuka mpaka wa eneo linalotawaliwa zaidi na upepo wa Jua na kuingia katika anga kati ya nyota, ambako kinaendelea kuchunguza mazingira ya angani.

Safari iliyoanza mwaka 1977​

Voyager 1 ilirushwa angani Septemba 5, 1977, kutoka Cape Canaveral, Florida, Marekani. Lengo lake la awali lilikuwa kuchunguza sayari kubwa za mfumo wa Jua, hususan Jupita na Zohali (Saturn), pamoja na miezi yake na mifumo ya pete inayozunguka baadhi ya sayari hizo.

Katika safari yake, chombo hicho kilikusanya taarifa na picha muhimu zilizosaidia wanasayansi kuelewa zaidi sayari za nje za mfumo wa Jua.

Miongoni mwa mafanikio yake ni kugundua pete nyembamba zinazozunguka Jupita na kuchunguza miezi ya sayari hiyo pamoja na Zohali. Baada ya kukamilisha malengo yake ya awali, Voyager 1 iliendelea na safari kuelekea maeneo ya mbali zaidi ya mfumo wa Jua.

Voyager 1.png


Agosti 25, 2012, Voyager 1 ilivuka heliopause — mpaka wa nje wa eneo ambalo upepo wa Jua na uga wake wa sumaku hutawala — na kuingia katika anga kati ya nyota, maarufu kama interstellar space.

Hatua hiyo iliifanya kuwa chombo cha kwanza kilichotengenezwa na binadamu kufikia eneo hilo. Pacha wake, Voyager 2, ulifuata Novemba 5, 2018.

Katika eneo hilo, Voyager 1 imekuwa ikikusanya taarifa kuhusu chembechembe za angani, mawimbi ya plasma na uga wa sumaku. Taarifa hizo huwasaidia wanasayansi kuelewa mazingira yaliyopo nje ya eneo linalotawaliwa na upepo wa Jua.

Hata hivyo, kuingia anga kati ya nyota hakumaanishi kuwa chombo hicho tayari kimeondoka kabisa katika mfumo wa Jua kwa maana pana ya kisayansi. Bado kiko katika safari ndefu kuelekea maeneo ya mbali zaidi, huku wanasayansi wakikadiria kuwa kinaweza kuchukua maelfu ya miaka kabla ya kuvuka Wingu la Oort, eneo la mbali lenye miili ya barafu inayozunguka Jua.

Ujumbe kutoka Duniani kwenda angani

Mbali na vifaa vya kisayansi, Voyager 1 inabeba diski maalumu ya dhahabu inayojulikana kama Golden Record. Diski hiyo iliwekwa kama ujumbe wa kuwakilisha Dunia na maisha ya binadamu endapo siku moja chombo hicho kitakutana na viumbe wenye akili kutoka nje ya Dunia.
Gold Disc.png



Diski hiyo ina salamu katika lugha 55, muziki, sauti mbalimbali za mazingira ya Dunia na picha zinazoonyesha maisha na ustaarabu wa binadamu.

Ujumbe huo unaonyesha jitihada za binadamu kueleza uwepo wake kwa viumbe wanaoweza kuwa katika maeneo mengine ya ulimwengu.

Je, Voyager 1 bado inafanya kazi?

Kwa mujibu wa NASA, Voyager 1 bado ilikuwa katika shughuli za uchunguzi wa anga kati ya nyota mwaka 2026, ingawa wahandisi wamekuwa wakizima baadhi ya vifaa ili kuhifadhi nishati inayozalishwa na mfumo wake wa umeme wa mionzi.

Kwa kuwa chombo hicho kiko mbali sana na Dunia, mawasiliano yake huchukua muda mrefu kufika. Hata hivyo, bado kina umuhimu mkubwa kwa sayansi kwa sababu kinatoa taarifa kutoka eneo ambalo hakuna chombo kingine cha binadamu kilichofika kwa namna hiyo.

Safari ya Voyager 1 ni mojawapo ya mafanikio makubwa ya uchunguzi wa anga, ikionyesha uwezo wa binadamu kutengeneza teknolojia inayoweza kuendelea kufanya kazi kwa miongo kadhaa na kuchunguza maeneo yaliyo mbali sana na sayari yetu.

 
Pamoja na yote hayo,kuna wahuni wanaobisha na kusambaza nongwa zao kwamba hakuna ukweli katika hilo.Na,wanaenda mbali zaidi kwa kusema Osama bin Laden hakuuwawa na yupo hai anabugia tende huku anahesabu ndevu zake polepole.
 
Pamoja na yote hayo,kuna wahuni wanaobisha na kusambaza nongwa zao kwamba hakuna ukweli katika hilo.Na,wanaenda mbali zaidi kwa kusema Osama bin Laden hakuuwawa na yupo hai anabugia tende huku anahesabu ndevu zake polepole.
Dogo The Icebreaker mtu wangu wa nguvu, je haya ni ya kweli? Ebu tupate maoni yako kiongoz.

secretarybird
 
Umbali kati ya nyota hupimwa kwa kipimo cha light year.

Mfano, nyota iliyo karibu kabisa na jua letu, ni Proxima Centauri iliyo 4.246 Light Years away.

Sasa ili kujua nyota hii iko mbali kiasi gani, katika miaka inayokaribia 50 ya safari ya Voyager 1, mpaka sasa ndiyo kwanza inakaribia kufika umbali wa one light day from earth.

Yani kama safari ya Voyager 1 ingekuwa inakwenda Proxima Centauri, umbali wa light years 4.246, katika miaka hii 49-50 ndiyo kwanza tumefikia umbali wa siku moja kati ya umbali wa miaka 4.246.

Sasa piga hesabu, miaka hiyo katika light days ni 1,551 light days.

Tukichukulia every light day takes 50 years (including acceleration and deceleration) 1,551 light days x 50 years =77,550.

Safari ya Voyager 1 kwenda nyota ya karibu kabisa na jua letu, Proxima Centauri, kwa mwendo huu, ingechukua miaka 77,550.

1977 + 77,550 = 79,527

Ingefika umbali huo (bila kujali mwendo zaidi wa Proxima Centauri, the very minimal time dilation na course correction) takriban mwaka 79,527 AD.
 
Back
Top Bottom