Tumepoteza pointi mbili lakini binafsi nimeona sababu kadhaa, za ndani ya Simba na nje ya Simba.
Nje ya Simba moja ni uwanja kuwa mbovu hali iliyosababisha timu isicheze vizuri, pili Mtibwa kucheza muda mwingi mchezo wa kujihami na kutafuta droo.
Ndani ya Simba kuna mambo kadhaa. Kwanza wachezaji wanaonekana kuchoka, pili wanaonekana kukosa morali. Tatu kocha anaonekana kukosa ubunifu wa kutumia wachezaji mfano mtu kama Said Khamis Ndemla ni mzuri sana na mwenye uwezo wa kubadili matokeo kwenye mechi ngumu. Nne lakini zaidi safu ya ushambuliaji imekuwa butu sana. Bila ya kocha kuwa na mkakati mpana katika kuboresha fowadi Nina wasiwasi kama tutatwaa ubingwa.