VPL leo tar. 21/04/2015: Yanga vs Stand United

VPL leo tar. 21/04/2015: Yanga vs Stand United

nimekuona kaka ila nduguyo Masuke kishakata tamaa, hapana chezeya Yanga. Mikia tumewafunga midomo kabisaaaa

Nipo sana ila tu ujenzi wa taifa ndo unanifany napotea potea si unajua hili Taifa unajenga leo kesho ukiamka unakuta baadhi ya sehemu limebomoka hivyo ujenzi wa hili Taifa haushi.

Mwaka huu kweli chama letu limepoteza mwelekeo, inabidi tutafute namna ya kubadilisha namna ya kucheza hii ligi, iwe inachezwa kwa mtoano.
 
tusahau kuwa na timu kama tp mazembe au zamelik bongo.!!
Sasa wewe unategemea kuwe na timu imara kama tp mazembe na zamalek kwa kuendelea kuwatumia hawa wachezaji wa ndani kama akina singano, ndemla na wengine???
Jiulize hao tp mazembe wana wachezaji wangapi kutoka mataifa mengine tofaut tofaut!!!
Hiyo ni kaz ya tff sio ya yanga kuifanya ligi kuwa na timu imara kama tp mazembe...... Waambie waongeze idadi ya wachezaji wa nje uone kama hatufiki mbali kimataifa.
 
teh teh teh zamani mlikua mkilalamika timu za ligi hazina ushindani, leo zimepatikana timu bora mnazihujumu uwanjani. Yanga atakuwa bingwa lakini kwa mwendo huu tusitegemee kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa.

Hivi ukiambiwa nitajie timu bora 5 Tanzania, Je Stand United CLW nayo itakuwa miongoni mwa hizo timu 5 bora? Kama siyo ni nini kinakufanya udai kuwa timu bora zimepatikana halafu mnazihujumu uwajani? Penati ni sehemu ya maamuzi katika mchezo wa soka, hata siku ya Etoile Sportive du Sahel Yanga tulipata penati na tukaitumia vizuri, marefa hawakuwa Watanzania mbona Etoile hawakulalamika?

Stand United CLW walishindwa wenyewe kutumia udhaifu wa defence ya Yanga iliyokuwa ikipwaya kwa kuwakosa Yondani na Cannavaro, wangekuja na plan B wangeweza kushinda badala ya kumlalamikia mwamuzi kwa kutoa penati kwa Yanga.

Mkuu Maziku Masunga Jr. jifunze kupokea matokeo bila kunung'unika.
 
Last edited by a moderator:
teh teh teh mdau hatuwezi kubashiri timu 5 bora wakati ligi bado inaendelea. Ligi ikiisha ndio tutajua ni timu zipi bora, Stand Utd bado ana nafasi ya kuingia tano bora kwa hizo game zilizobaki. Yanga tayari ni bingwa lakini kwa mchezo wa jana ulikuwa ni suluhu sema tu referees wetu huwa waoga wanapochezesha michezo ya Yanga au Simba.

Siyo kweli ndg, hiyo ilikuwa zamani, lakini siku hizi TFF wamewabana sana huwezi ona upendelea wa kijinga kama zamani, wewe angalia hata gemu la leo utaamini ninachokwambia, makosa ya marefa ya ligi yetu kwa sasa ni ya kibinadamu zaidi kama tunayoona kwenye ligi za ulaya

Sema timu nyingi zina inferiority complex zinapocheza dhidi ya yanga, simba na azam. Zamani sawa hata mimi nakubali zilikuwa zinapendelewa, lakini siku hiz hakuna kitu kama hicho mkuu, na hii ni sababu mojawapo ya kuongezeka kwa ushindani kwenye ligi yetu.
 
Back
Top Bottom