yahoo
JF-Expert Member
- Sep 9, 2011
- 3,526
- 1,409
Masao Bwire akiongea na RFA amedai kuwa 'Yanga ni gari bovu lililokata breki halafu limekuwa likizuiwa na vigingi dhaifu', akaongeza kuwa 'Ruvu Shooting ni kigingi imara kitakachozuia hilo gari bovu'. Amejinasibu kuwa endapo wataifunga Yanga watajipatia heshima kubwa na kutambuliwa na Watanzania kwani Yanga ndiyo inaongoza ligi kwa sasa.
Swali linabaki kuwa: je, ni kweli Ruvu Shooting ni kigingi imara kwa Yanga?
Wewe kwa kukariri nakupa tuzo unafaa kuwa mwandishi,umenukuu vilevile kama nilivomsikia...