VPL: Simba SC Vs Azam FC

Watoke sare ya bila kufungana. Maana akishinda mnyama, kelele zitakuwa nyingi mtaani. Akishinda lambalamba atazidi kutuacha.

Dua za kombe la mapinduzi na mechi ya ndanda zinaendelea kama kawaida. Wengine leo eti wanadanganya hakuna ibada, timu analosapoti likifungwa wanapotea humu wakiulizwa nilikuwa ibadani. Kaazi kwelikweli
 
Mashabiki wengi wa simba naona wamejawa nyuso za furaha. Mashabiki wa Simba Ukawa nao wapo upande wao ule ule wa juani.
 
Tulifunga bao, na wakati tulipodhani tumeshinda, Omar Hussein akaisawazishia Yanga zikiwa zimesalia dakika nane tu.”


Yanga kumbe nanyi mmo kwenye hizi imani? Mtatoaje droo na timu inayoroga?
 
Weka na kikosi cha mnyama ili tutoe tathmini.

Nimekipata kikosi kitakachoanza na kitakuwa kama ifuatavyo:

Manyika Peter.
Ramadhan Kessy
Mohamed Husein
Juuko Murshid
Hassan Isihaka ( C)
Jonas Mkude
Ramadhan Singano
Said Ndemla
Elias Maguli
Danny Sserukuma
Emanuel Okwi
 
Timu zinaingia uwanjani ili kuanza mtanange wa kukatana shoka, azam fc vs simba. kila la kheir lambalamba leo nipo kwenu kwa mkopo wa muda wa masaa mawili tu.
 
Leo mtani njoo kwetu tu, maana hata huku Azam tunaichukia balaa (siongelei wana-Simba wote)!!
Niwe mkweli, mi binafsi, yanga ikicheza na Azam, huwa najikuta nataka Azam ifungwe!! Sipendi kutaka Yanga ishinde, ila roho yangu inakuaga hivyo!

Mimi huwa napenda matokeo kama yale ya mechi iliyopita.
 
Mungu ibariki Simba ifungwe au itoe droo kama kawaida yake
 
MUNGU IBARIKI SIMBA ! Updates muhimu wadau!
 
Dakika 10: Simba 0-0 Azam.

Azam wanacheza kama Defending Champions wa ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…