VPL: Simba v Prisons 28-02-2015

VPL: Simba v Prisons 28-02-2015

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Wadau wote wa soka, tukutane hapa kupeana updates, hoja, majadiliano na mawazo mbalimbali yanayolenga mechi hii ya Leo.

Muda_ [10:00 jioni.]
Uwanja_[ Taifa Dar es Salaam]
====================

Matokeo
Simba 5-0 Prisons

Wafungaji wa Simba
Ibrahim Hajib (3), Emmanuel Okwi(1) na Ramadhani Singano(1)
 
Simba( Mnyama) vs TZ Prisons (Wajelajela)
 
Ninaomba sana simba leo tufungwe...naomba sana tufungwe...ili viongozi wa timu wakubali kukaa chini na kujua tatizo ni nini.

Kushinda leo kutaendeleza mtindo wa viongozi wa simba kuendelea kupiga siasa kuwa mamb yatakuwa sawa.

Leo mimi nashabikia Prisons.

cc Makoye Matale Amavubi grafani11 sembo barafuyamoto
 
Last edited by a moderator:

Kheir yako wewe umekata tamaa mapemda manake baadae mkifungwa hautaumia sana kuliko wale wenye matumaini ya kushinda na wajelajela wakianza kuwatembezea mkong'oto wataumia sana.
Kila la kheir Tz Prisons.
 
Sio suala la kukata tamaa....ni bora tuongelee uhalisia ili kutatua tatizo

Kushinda leo kwa simba kunawapa ahueni viongozi ili kupiga siasa zao wakati kiwango cha timu hakiridhishi

Hapa tulipo hata nafasi 2 za juu haiwezekani

Sasa tunataka nini kwenye ligi?

Ni bora leo tufungwe ili tugawane mbao pale klabuni tuanze upya.

Klabu yetu inahangaishwa na wapuuzi wa matawi mawili tu

Tawi la Mpira Pesa (Friends of Simba) na Tawi la Mpira Maendeleo (UKAWA).

Simba inapitia kipindi kigumu kwa sababu ya misuguano ya hao wapuuzi
 
Ninaomba sana simba leo tufungwe...naomba sana tufungwe...ili viongozi wa timu wakubali kukaa chini na kujua tatizo ni nini.

Kushinda leo kutaendeleza mtindo wa viongozi wa simba kuendelea kupiga siasa kuwa mamb yatakuwa sawa.

Leo mimi nashabikia Prisons.

cc Makoye Matale Amavubi grafani11 sembo barafuyamoto

Mkuu hii ya kwako haikubaliki, wachezaji inabidi waachane na mgogoro wa nje ya uwanja, wawaache viongozi wao na wenyewe wafanye yao.
 
Mkuu hilo unalolisema haliwezekani...kwa mfumo wa usajili wa timu yetu na namna ya umiliki wa wachezaji wa timu yetu huwezi kuwatenga na yanayoendelea nje......

Mkuu...nadhani unajua wachezaji wa simba hawamilikiwi na timu bali na watu binafsi

Mishahara wanalipwa na watu binafsi na hao ndio waliowasajili

Timu haina pesa ya kusajili wala kulipa mishahara.

Kwa hio hawa watu waliopo nje kama hawaelewani basi obvious uwanjani hatuwezi kufanya kitu

Ivi umefikiria kitendo cha timu yetu kwenda kucheza ndondo kahama ili wapate hela ya hoteli na mafuta ya gari...na bado unaombe timu leo ishinde? Kweli? hapo hautakuwa fair
 
Ushindi kwa Prisons leo, tunataka wavurugane hasa. Kuna wanaohama timu, waliochanganyikiwa wiki nzima, waliokuwa wakali kwa wiki hii.
prisons tupeni raha, piga mikia aka paka, Simba alishakuwa paka.
Jangwani full furaha, Ngassa tunakupenda wewe acha tu.
 
Mmmmmmmm...na wewe kwa kushadadia hujambo Komeo La Chuma kuja huku kuna mchumba hapa
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hilo unalolisema haliwezekani...kwa mfumo wa usajili wa timu yetu na namna ya umiliki wa wachezaji wa timu yetu huwezi kuwatenga na yanayoendelea nje......

Mkuu...nadhani unajua wachezaji wa simba hawamilikiwi na timu bali na watu binafsi

Mishahara wanalipwa na watu binafsi na hao ndio waliowasajili

Timu haina pesa ya kusajili wala kulipa mishahara.

Kwa hio hawa watu waliopo nje kama hawaelewani basi obvious uwanjani hatuwezi kufanya kitu

Ivi umefikiria kitendo cha timu yetu kwenda kucheza ndondo kahama ili wapate hela ya hoteli na mafuta ya gari...na bado unaombe timu leo ishinde? Kweli? hapo hautakuwa fair

Mkuu, hata watoto wanaolipiwa ada na wazazi/walezi wao ikitokea kuna mgogoro kwenye familia kwa anayejitambua yeye atakazania masomo yake na kujitahidi kufaulu mtihani.
 
Ninaomba sana simba leo tufungwe...naomba sana tufungwe...ili viongozi wa timu wakubali kukaa chini na kujua tatizo ni nini.

Kushinda leo kutaendeleza mtindo wa viongozi wa simba kuendelea kupiga siasa kuwa mamb yatakuwa sawa.

Leo mimi nashabikia Prisons.

cc Makoye Matale Amavubi grafani11 sembo barafuyamoto

He! Makubwa, kama mmefikia hatua hiyo ni balaa!
 
Mkuu, hata watoto wanaolipiwa ada na wazazi/walezi wao ikitokea kuna mgogoro kwenye familia kwa anayejitambua yeye atakazania masomo yake na kujitahidi kufaulu mtihani.

Sasa hapa tunaongelea teamwork....haiwezekani ikawepo....Teamwork ni kila kitu

Mkuu pale simba kuna matatizo makubwa sana mkuu

Wachezaji kadhaa hawajalipwa mishahara ya miezi zaidi ya miwili

Alafu unataka washinde....wataanzaje mkuu? Tunatakiwa tuwe fair masuke
 
huyu kaburu atuachie Simba yetu tumechoka kudharaulika...
 
Pamoja na yote hayo, bado hatutakiwi kuomba kufungwa hizo zitakuwa ni hasira.
 
Ushindi kwa Prisons leo, tunataka wavurugane hasa. Kuna wanaohama timu, waliochanganyikiwa wiki nzima, waliokuwa wakali kwa wiki hii.
prisons tupeni raha, piga mikia aka paka, Simba alishakuwa paka.
Jangwani full furaha, Ngassa tunakupenda wewe acha tu.

mmeshindwa kumlipia mil 45...
 
huyu kaburu atuachie Simba yetu tumechoka kudharaulika...

Kaburu si mtu mzuri, ana kasumba sana ya kuingilia mambo ya kiufundi. Muulizeni Juma Nyoso kwanini aliondoka Simba? Akikosana na kocha basi lazima ataihujumu timu kupitia wachezaji
 
Back
Top Bottom