VPL: Super Saturday 17/10/2015

VPL: Super Saturday 17/10/2015

Uwanja wa Taifa migulubaja kama kawaida yao wamekosa penati. Refa amelipa alichopewa wenyewe wameshindwa.
 
Ukiona mtu mzima anachambua matokeo ya soka kwa kuegemea zaidi historia ujue huyo amefilisika kisoka amebaki na matokeo yaliyopita kichwani. Wakati Simba SC wanatumia Science mpya wewe umeng'ang'ania historia kama fuvu la Zinjanthropus!
 
Kuna siku nilikuwa nasoma makala moja ambayo ndani yake Betram Mwombeki alikuwa akihojiwa...

Alitaja kuwa moja ya mambo yaliyomkimbiza Msimbazi ni huo ulozi ulozi...

Hizi timu zote zimebobea tu kwenye ndumba...
Nadhani umechanganya stori kidogo. Mwombeki hakukimbia Simba, ila aliachwa kwa kuwa kocha hakumkubali. Alienda JKT Ruvu na ndiko alipokutana na mambo hayo. Nakuwekea kipande hiki cha simulizi yake kutoka kwenye moja ya blogs za bongo

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Simba na sasa JKT Ruvu, Betram Mwombeki ameamua kuachana na soka na kurejea kwenye fani yake ya zamani ya uvuvi na ufugaji.

Mwombe amekaririwa na E-fm usiku huu akisema kwasasa yuko Mwanza kwa mapumziko na muda si mrefu anaanza shughuli za ya kufuga na kuvua samaki kwasababu anasumbuliwa sana na miguu inayomuuma kwenye unyayo.
"Niko Mwanza sasa hivi, nimeamua kuachana na mpira kwasababu naumwa miguu kwa chini, kama nachomwa sindano vile. Ilianza niliposajiliwa JKT Ruvu, lakini nikiwa Simba haikuwa kunitokea". Amesema Mwombeki na kuongeza: "Nimeamua kurudi kwenye fani yangu ya zamani ya ufugaji na uvuvi".

Mwamboki amebakiza mkataba wa mwaka mmoja katika klabu yake ya JKT Ruvu, lakini anaamini watamalizana bila matatizo yoyote.
 
Yebo yebo ilikuwa na wachezaji 13 uwanjani: Refa na mashabiki. Inaonekana refa ana kadi ya uanachama wa maisha wa Yanga.

Hongera refa; hata kama timu yako haikushinda.
 
Yebo yebo ilikuwa na wachezaji 13 uwanjani: Refa na mashabiki. Inaonekana refa ana kadi ya uanachama wa maisha wa Yanga.

Hongera refa; hata kama timu yako haikushinda.

Sisi tumecheza na timu bora, kutoa sare ni jambo la la kawaida kabisa. Kumbuka hii ni mechi ya 3 mfululizo inachezwa ndani ya dakika 90 na timu kutoka sare au suluhu. Kwa sasa mpinzani wa ukweli wa Yanga ni Azam FC, Simba SC amebaki kuwa mtani tu.

Huko Mbeya Simba ilikuwa na wachezaji 13 viz Kaseja alikuwa mshambuliaji katika lango la MCC FC.
 
Wewe msukuma ulipotea kwa muda. Salama lakini?
 
Back
Top Bottom