VPL: Tar. 22\04\2015: Simba vs Mgambo JKT

VPL: Tar. 22\04\2015: Simba vs Mgambo JKT

namanyele

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2012
Posts
1,852
Reaction score
610
Jana tumeshuhudia vijana wa Jangwani wakishinda kwa mbinde sana mbele ya Stand Utd, Leo kivumbi kingine ambapo Simba watakuwa na kibarua kigumu sana mbele ya Mgambo JKT toka jijini Tanga timu ambayo Simba inapata wakati mgumu sana pindi wanapokutana uwanjani.

Simba inayosaka nafasi ya pili kwa udi na uvumba ili mwakani na yenyewe iweze kushiriki michuano ya kimataifa itacheza kufa na kupona kuhakikisha wanaibuka na ushindi mnono leo na sio kuishia wasindikizaji tu kwenye kama timu zingine. Kama kawaida kutakuwa na live updates hapa hapa jamii forum.

Hii game itakuwa ni kali sana kuliko game ya jana maana Simba wanataka kulipa kisasi baada kufungwa 2 kule jijini Tanga, pia Mgambo wanataka kuendeleza uteja kwa Simba.

================
================


Matokeo ya Mwisho: Simba 4 - 0 Mgambo
 
Kila la kheir timu ya Mgambo Jkt....
Funga hao mikia fc warudi porini huku mjini mambo yamewashinda.
 
Utabiri wangu Mikia Fc 1 - Mgambo 2


Mimi nasubiri tamko tu la uongozi wa SIMBA kama waliotoa kwa timu ya Mbeya city kuwa wasiikomalie tu simba wazikomalie na timu nyingine.
 
Naona mgonjwa wa homa ya vipindi leo anaendelea vizuri.hivi kuna wanasimba wanaweza kusimama hadharani na kusema kuwa timu yao ina uwezo wa kushika nafasi ya pili?
 
Yebo yebo mpo?

Simba akishinda leo atakuwa na point ngapi ?. Atabakiwa na mechi ngapi kumaliza ligi ?. Atahitaji point ngapi kumfikia Yanga ambaye anaweza kufungwa mechi zote zilizobaki ?
 
Back
Top Bottom