Vuguvugu la kurudisha kadi za CCM watatumbuliwa ma-DC wangapi?

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
Hayati mwendazake aliifahamu vema nguvu ya uma, kuchokwa kwa chama chake na kutopendwa kwa viongozi wa chama chake ndio maana aliamua kibabe sana kukataza mikutano ya kisiasa na mijadala huru ya wananchi...

NGUVU ya uma ni kitu chenye nguvu sana maana ni muunganiko wa roho nyingi zenye nishati inayowaza jambo moja kwa pamoja, tofauti kabisa na nguvu ya kiongozi anayewaza jambo moja kwa msaada wa vyombo vya ulinzi vinavyopokea ujira na kumtumikia mtawala!

Chama tawala kimechokwa na hata wanachama wake! Hili si jambo la kushangaza hasa kutokana na ukongwe wake.. Wananchi wa Mtwara wanaojulikana kwa misimamo na utata wiki iliyopita baada ya kuchoshwa na ujinga wa viongozi wao wakaamua kwenye mkutano wa hadhara kurudisha kadi za CCM kufikisha ujumbe kunakohusika.

Watawala ama kwa kukurupuka ama kwa kutafuta huruma ya jamii ama kwa kutowaza kwa weledi wakaamua kwa haraka kuwatumbua viongozi wa kisiasa waliosababisha tatizo! Haikuwa hatua mbaya walifanya vema kusimama na wananchi. Lakini kwakuwa mambo ni mengi na muda ni mchache wakadhani hilo limeisha.

Jana kwenye mkutano wa hadhara huko wilayani Lushoto moja ya ngome kongwe za CCM wananchi wa kijiji cha View Point kwenye mkutano wa hadhara nao wakarudisha kadi za ccm kuonesha kutoridhishwa kwao na viongozi wao wa kisiasa
Mbegu iliyopandwa Mtwara imechipukia Milimani lushoto mamia ya kilometa. Moto uliowashwa Mtwara umeruka hadi Lushoto mwendo wa masaa si chini ya 20 kwa mwendo wa gari.

Tafsiri yake ninini hapa? Wananchi wamechoka na uoga hatimaye umewatoka! Hawaogopi tena! Ni ngumu kutabiri kituo kifuatacho kitakuwa wapi.. Kama kikiwa kanda ya ziwa hiyo ni habari ya kutisha sana...

Swali la kujiuliza je na DC wa Lushoto naye atatumbuliwa kwa kuzembea mpaka wananchi wakarudisha kadi za chama?

Je, asipotumbuliwa itakuwaje kwa aliyetumbuliwa? Maana makosa yanafanana.

Na je hili vuguvugu la kurudisha kadi za ccm tena kwenye mikutano isiyokuwa ya wapinzani likishika kasi. Watatumbuliwa wangapi!? Au wangapi hawatatumbuliwa?

Your browser is not able to display this video.
 
Cha Ajabu iilikuwa ni Kikao cha Kawaida tu na wala sio kikao cha Chama chochote kama unaona hapo mbele meza kuu ni Kamati ya maendeleo ya kata.....
 
Nadhani ni wakati was kuwa na mabadiliko sahihi, hi nchi sio ya kifalme.
👉Kwamba utakula Kwasababu una juana na fulani au fulani.
👉Usalama wa taifa wajiangalie, Kuna viongozi Wana tumia magari ya mabilioni, wakati Kuna vijiji havina maji ya uhakika.
👉Na ikiwapendeza walipuane tu, huko ikulu🤒
 
amekiri kuwa akiambiwa kuchagua CCM na andazi yeye atachagua Andazi [emoji1787][emoji1787] CCM tunaenda kubaya Sana..[emoji23]
 
CCM imechokwa tatizo hakuna chama mbadala
 
amekiri kuwa akiambiwa kuchagua CCM na andazi yeye atachagua Andazi [emoji1787][emoji1787] CCM tunaenda kubaya Sana..[emoji23]

Mwenyekiti inabdi afanye kitu Aisee Maana naona hali inakoelekea Mwaka 2025 tutaangukia pua..

Vijijini ndo huwa tegemeo letu sasa na wenyewe wameanza kutusaliti hapa kuna Jambo la ziada la kufanya

5
 
Kwa ufupi Mama hata sisi chawa wake huwa hatumuelewi ila kwa sababh ya uchawa lazima tumuunge mkono tu maana katiba inampa mamlaka ya kuua bila kushitakiwa etc[emoji3064][emoji848][emoji2827]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…