Vuguvugu la Muungano taratibu linaanza kupata joto

Vuguvugu la Muungano taratibu linaanza kupata joto

Kisipotosha tutanunua ya kwenu bara

Maana yangu ni kwamba ubaguzi,huchanua mpaka itafikia hatua wenyewe kwa wenyewe mnapigana pini.


Kuhusu nyinyi kununua bara wala hatuna tabu tunawahesabu nyinyi kama watanzania huku ni kwenu pia.
 
Sie Zanzibari twastaarabika, hatutaki wahuni waje kuvuruga ustaarabu wetu

Mmeruhusu wageni waje kisa wanawaletea mapesa,lakini ndugu zenu mnasema wanavunja ustaarabu wenu.

Ustaarabu wenyewe ni upi,kutokula ramadhani hadharani[emoji23][emoji23]
 
Zanzibar ni kiwilaya Fulani hivi na wala sina haja ya kuhangaika na Wilaya hiyo
 
Huo Muungano wanaoung'aninia ni nyie nyie Wadanganyika, wenyewe hawautaki hata kuusikia, sasa jiulize kwanini mnawang'ang'ania licha ya kuwawekeeni vikwazo
Siombei, ila siku kukichafuka wataelewa
 
Niliwah kusema Muungano wa Tanzania una makosa na mapungufu mengi kiutekelezaji tunakoenda tutake tusitake utavunjika kama hautafanyiwa mabadiliko kufatia kero za kimuungano zilizopo.


Mfano
1....Mzazibari anaweza kumiliki ardhi bara lakin mtanganyika Hilo kwa Zanzibar haliwezekan.

2....Mzanzibar anaweza kupewa UONGOZI bara lakin mtanganyika Hilo haliwezekan,Mfano watu wamehoji sana Shaka kupewa ukuu wa wilaya Tanzania bara wakati mtanganyika huwez kuwa mkuu wa wilaya Zanzibar


3 .... Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikikusanya kodi Zanzibar fedha hizo zinabaki huko kwa ajili ya matumizi ya Zanzibar, pia kuna Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) ambayo nayo inakusanya mapato lakini pia nayo yanabaki kuwa kwenye matumizi ya Zanzibar.

4....kutozwa kodi ya bidhaa pale unaponunua bidhaa kutoka upande Mmoja wa MUUNGANO.
Mbona hilo ni kawaida mzee. Kwa mfano mchina bara hawez kununua ardhi Hong Kong au hata kuingia tu wanaruhisiwa kuingia mara mbili kwa mwaka. Na hata Taiwan Macao ni hivyo hivyo. Kuna sheria wanaiita ni sheria ya kulinda visiwa. Mkisema muende tu baada ya muda mchache maana huku tuko wengi tunaweza kununua eneo lote.ndicho wanakikwepa.
 
Ndio maana yake. Nini hujaelewa hapo?
Hoja mfu kabisa,,

Kwamba wabara wakipewa ardhi ya visiwani watamaliza ardhi.

Mbona wao wanajenga na ardhi haiishi.

Na huku bara,,mbona hakuna zuio lolote kwa wazanzibar,,,

Uchoyo na ubinafsi unawasumbuwa.

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
 
Siyo kwamba watanzania wote ni mazwazwa kuhoji mambo kama hayo ndiyo kipimo harisi Cha uhai wa akili ya mwanadam

Na mm nasema Kuna kizazi kitakuja hakitakubaliana na huu MUUNGANO wa hovyo wenye kunufaisha upande Mmoja wa muungano na viongozi wa juu tu
 
Kuhoji mambo kama haya siyo uhaini

Ni kuwakumbusha wakubwa wasiendelee kula kodi zetu tu bila kutatua vitu vidogo vidogo kama hivi ambavyo kadri vinavyoachwa ndiyo vinakuwa kero zaidi


Na sisi wengine hatuogopi kama nyie


Unaiogopa SERIKALI kuliko hata Mungu wewe ni kichaa tu kama vichaa wengine, yaani unashindwa kuhoji mambo ya msingi kwa kuogopa SERIKALI wakati hata usipohoji wewe ipo siku watahoji watoto wako huenda wasitumie busara za kuhoji badala yake wakaukataa muungano kwa nguvu na maandamano bila kusubili kero za muungano kupatiwa ufumbuzi.


Siku zote ninapopata muda wa kuzungumza na wenye vyeo Huwa nawaambia muda ndiyo Kila kitu unaweza ukatumia nguvu za Dora kuwanyamazisha watu wasizungumze kuhusu jambo furani kama Hilo jambo nilakudumu ipo siku litazungumzwa na wengine ambao hutakuwa na uwezo wa kuwanyamazisha tena.
 
We mbona unafanya uhaini hadharani?

Mod ondoa uzi mara moja vingine uwajibike[emoji2959]
Kuhoji mambo ya msingi ni uhaini!? Unajua maana ya uhaini wewe!? Hiki ninachokifanya kinaitwa kuruhusu akili iwe hai yaani iwe na uwezo wa kuchambua vitu vikubwa ambavyo vinagusa jamii na kuleta mtikisiko kwa watawala walioshindwa kutatua kero hizo

Lakini pia haya mambo hta nisiposema mm Bado yatasemwa na wengine, kwahiyo hatuna haja ya kuyakwepa zaidi Zaid yapatiwe ufumbuzi.
 
Ukichukua chumvi kijiko kimoja ukakimwaga kwenye pipa la maji, maji hayataharibika kwa chumvi na chumvi itapotelea kwenye maji.

Wazanzibari wakiwa sehemu ya Tanganyika ni rahisi kumezwa na kuwa watanganyika, ila watanganyika wakiwa sehemu ya wanzanzibari, wanzanzibari watapigana wakiamini wamevamiwa ardhi yao.

Kwani ile 1964 kuuliwa watu kwa maelfu na kila uchaguzi kuuliwa watu ili kuwekwa kibaraka wa Dodoma , huo si Uvamizi ??
 
Kwani ile 1964 kuuliwa watu kwa maelfu na kila uchaguzi kuuliwa watu ili kuwekwa kibaraka wa Dodoma , huo si Uvamizi ??
Ile ni siasa za madaraka sio vita vya muungano. Hata huku bara kuna vifo huwa vinatokea.
 
Ile ni siasa za madaraka sio vita vya muungano. Hata huku bara kuna vifo huwa vinatokea.

AN-NUUR Jamaduthan 1414 A.H, Desemba 1993

MJADALA unaendelea nchini kote juu ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika na muundo wa Muungano wa Zanzibar na Tanganyika. Inavyoelekea yapo matatizo, dosari na sababu za msingi zilizopelekea wananchi kuhoji muundo wa sasa wa Muungano na kuleta hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika ni yenye kuundwa kama si leo kesho.

Lakini wapo pia wanaopinga kabisa kuundwa kwa serikali ya Tanganyika.

Aliyejitokeza kwa nguvu na kwa ukali hadharani kupinga hoja hiyo ni Mwalimu Julius Nyerere, katika kupinga hoja hiyo Mwalimu anatoa hoja zifuatazo:

Hoja ya kuundwa kwa serikali ya Tanganyika imeletwa kwa kuwachoka Wazanzibari na Waislamu. Ufupi wa maneno Mwalimu Nyerere anadai hoja ya kuundwa Serikali ya Tanganyika imetokana na chuki za kidini - Wakristo kuwachukia Waislamu.

Hoja haipo katika sera za CCM na taratibu zimekosewa.

Kuundwa kwa serikali ya Tanganyika kutavunja Muungano na kutavunja Tanganyika pia.

Ukizingatia sifa nyingi ambazo Nyerere alijilimbikizia wakati wa utawala wake na sasa si vigumu kuelewa kwa nini anapinga kuundwa kwa serikali ya Tanganyika. Mambo yake yote aliyoyaanzisha kwa vishindo huku akisifiwa kuwa zidumu fikra zake, yamekuwa yakiporomoka moja baada ya jingine huku mwenyewe akiona. Lililosalia ni Muungano; nao ukiporomoka haitaleta picha nzuri katika historia yake katika siasa.

Lakini lililo gumu kueleweka ni hatua ya Mwalimu Nyerere kutumia Turufu ya udini kuwagawa Wabunge; wana-CCM na Wa-Tanzania kwa ujumla katika suala hili. Kauli hiyo ingesemwa na Muislamu ingepewa mtizamo tofauti na labda isingeeleweka hasa miongoni mwa Waislamu. Lakini kusemwa na Mwalimu Nyerere kunaleta mkanganyiko zaidi. Kwanini; (udini ulikuwa umejengeka). Hali hiyo ilipelekea Masheikh kumlalamikia lakini akawanyamazisha kwa kuwashutumu kuwa wanachanganya dini na siasa. Miongoni mwa Masheikh hao wapo waliofukuzwa nchini; waliowekwa kizuizini, waliofukuzwa katika chama na kadhalika.

Sheikh Hassan bin Amir katika waraka wake kwa Waislamu mwaka 1963 aliutaja udini uliokuwa unajengwa Tanzania kwa kutoa mifano ifuatayo:

Kuingizwa nchini Tanganyika mara tu baada ya uhuru vimedali vidogo vidogo vyenye picha ya bendera ya Tanganyika usoni na katikati ya bendera hiyo amesimama Mama Maria na mtoto mchanga na nyuma yake maandiko 'MARIA MTAKATIFU ULINDE UHURU WA TANGANYIKA'.

Gazeti la KIONGOZI la tarehe 1/8/1963 lilimuonyesha Bwana George Kahama akipewa cheo cha dini na Pope kwa kuwakilisha serikali ya Tanganyika katika mkutano wa Makanisa ya Roma.

Mwaka huo huo wa 1963, mnamo tarehe 24 mwezi wa nane, Baraza Kuu la Makanisa ya Kilutheri Tanganyika lilitoa matangazo kuwa Uhuru wa Tanganyika ulikuwa 'Chini ya Msalaba'.

Tarehe 17/5/1963 Makanisa yalifanyia mkutano wao ndani ya Bunge.

Alipokufa Pope Yohana wa 23 bendera ya taifa ilipepea nusu mlingoti nchi nzima!

Kabla ya kifo chake Pope Yohana wa 23 alimletea Mheshimiwa Nyerere barua ya pongezi kwa kuupanua Ukristo- barua ambayo ilitiwa saini na Pope mwenyewe. Barua hiyo imetangazwa kwenye gazeti la Tanganyika Standard.

Gazeti la Reporter la Kenya la tarehe 20/6/1963 lilitangaza katika ukurasa wake wa mbele: "KUIBADILI AFRIKA YA MASHARIKI KUWA KATIKA DINI YA ROMANI CATHOLIC". Ndani ya gazeti hilo ukurasa wa 18 liliwataja waliopewa dhamana ya kufanikisha jambo hilo kuwa ni: Uganda - Kiwanuka, Kenya - Mboya na Tanganyika Mheshimiwa Nyerere.
 
Kipindi alipokuwepo raisi kutoka Tanganyika mada hizi hazikuwepo sijuwi kwanini.
 
Kwahiyo wabara wakinunua ardhi zanzibar ni sawa na kuinajisi hiyo ardhi??!!--- Tuanzie hapo.
Mbona watu mnapenda kubishana sana!?
Kwani jibu si nimetoa hapo juu yaani umeruka jibu umetafuta kistatement kidogo cha kuanza kubishana....
Msinichoshe mimi
 
Hoja mfu kabisa,,

Kwamba wabara wakipewa ardhi ya visiwani watamaliza ardhi.

Mbona wao wanajenga na ardhi haiishi.

Na huku bara,,mbona hakuna zuio lolote kwa wazanzibar,,,

Uchoyo na ubinafsi unawasumbuwa.

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
Eti mbona nao wanajenga na haiishi, 🤣
Ila Watanzania mnapenda sana kubishana sijui mna matatizo gani aisee!

Jibu la Population hamlitaki ila mmekazana kubisha tu,

Kama mmeshawajua ni Wachoyo na Wabinafsi ndio mkae kwenu sasa Kibaha tu hapo kuna Mapori tele huko Znz mnaitaka Ardhi yao ndogo kwanini???
 
Mbona watu mnapenda kubishana sana!?
Kwani jibu si nimetoa hapo juu yaani umeruka jibu umetafuta kistatement kidogo cha kuanza kubishana....
Msinichoshe mimi


Basi hata sisi kwenda huko twende kwa idadi maalumu ya watu ili kisiwa kisije kuzama kutokana na uzito wa watu kutoka bara.--- huo ndio Muungano safi wa nchi mbili.
 
Basi hata sisi kwenda huko twende kwa idadi maalumu ya watu ili kisiwa kisije kuzama kutokana na uzito wa watu kutoka bara.--- huo ndio Muungano safi wa nchi mbili.
Kwani hata kwenda hua mnaenda wengi? Mkafanye nini kwenye kisiwa cha utalii wenzenu wanafanya manunuzi kwa Dollar 😀

Sie tukae hapa hapa bado tuna mapori ya kutosha tulime na kufuga.
 
Back
Top Bottom