Wakaguongo
Member
- Sep 23, 2026
- 95
- 38
Baadhi ya video hizo zinaonyesha vumbi likipeperushwa na upepo, hali iliyowafanya watumiaji wa mitandao ya kijamii kuzungumzia kilichokuwa kikiendelea jijini humo.
Tukio hilo limeibua udadisi kuhusu kilichosababisha hali hiyo, hasa kwa wakazi ambao hawakutarajia kuona vumbi likipeperushwa kwa kiwango hicho wakati wa usiku.
Hata hivyo, bado hakuna uthibitisho wa kutosha kuhusu chanzo cha upepo na vumbi hilo, maeneo yote yaliyoathirika au iwapo tukio hilo lilihusishwa na mfumo maalumu wa hali ya hewa.
Kwa wale waliokuwa Nairobi Alhamisi jioni, hali imekuwaje katika maeneo yenu? Uliiona hiyo hali ya vumbi na upepo?