Hapana,adui yao no.1 ni ukabila na wala usimsingizie mzungu!Pindi watakapogundua kuwa wao ni taifa moja na hawana haja ya kubaguana kikabila,hapo watakuwa wameushinda ukabali.Mzungu hata hawachochee vipi kama hawana nia ya kupigana wakitambua kuwa wao ni wamoja.Ila wanapoanza kwa kampeni za kikabila,radio station za kabila flani kumpigia kampeni mgombea flani wa kabila ilo,vijana kuhamasishwa kwamba kabila flani limetawala nchi toka wapate uhuru ni zamu ya kabila lingine,huo ndo ukabila na ambao mpaka sasaiv tunaona unashika kasi kama moto wa kifuu.
Cha muhimu wagundue kuwa uchaguzi utapita na watu watabaki na maisha yao.Wenye ngeu watakuwa na ngeu ila wachochezi(WANASIASA) watakuwa ng'ambo na familia zao wakila maisha.
Niwaombe tu ndugu zetu Wakenya,tujali utu zaidi ya ukabila,udini au chuki yeyote ile inayopandikizwa na wanaasiasa.Nyinyi ni jirani zetu and we wish to see the best from you guys.You are a brother country to the EAC.So you should lead by exmple.
God Bless Kenya.