Vurugu Mbeya: Waendesha bajaji wagomea agizo la Mkuu wa Mkoa kubadilishiwa ruti

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
267
Reaction score
1,014

Kuna taarifa za kuwepo kwa vurugu zinazohusisha madereva wa bajaji jijini Mbeya wakipinga maelekezo ya Serikali ya kupangiwa ruti nyingine ambazo haziingiliani na daladala.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, mgogoro ulitokana na kuingiliana kwa njia za bajaji na daladala.

Video zilizosambaa mitandaoni tangu Oktoba 19, 2026 zimeonyesha waendesha bajaji wakipinga mpango mpya uliowekwa na Halmashauri ya Jiji la Mbeya wa ruti zao.

Mzozo huo ndio ulisababisha mgomo wa daladala Septemba 7 lakini zilirejea kutoa huduma Septemba 8 baada ya mgomo wa siku moja, lakini suluhisho la kudumu lilikuwa bado linahitajika.

Soma pia: Mgomo wa Daladala Mbeya

Oktoba 13, 2026 inaeleza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Jumanne Abdallah Sagini, aliwapa viongozi wa serikali za mitaa siku saba kuandaa mpango wa kuratibu maeneo ya shughuli za machinga na waendesha bajaji, leseni na usimamizi wa usafiri.

Ofisa Mfawidhi na Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) katika Mkoa wa Mbeya, Shaaban Mdende alipoulizwa kuhusu mzozo huo, alisema wanaopaswa kuzungumzia Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Justice Laurent Kijazi alipoulizwa kuhusu vurugu hizo, aliomba kutumiwa ujumbe, lakini hata vyo hakuujibu.
 
View attachment 3694337

View attachment 3694338

Oktoba 13, 2026 inaeleza kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Jumanne Abdallah Sagini, aliwapa viongozi wa serikali za mitaa siku saba kuandaa mpango wa kuratibu maeneo ya shughuli za machinga na waendesha bajaji, leseni na usimamizi wa usafiri.

Ofisa Mfawidhi na Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) katika Mkoa wa Mbeya, Shaaban Mdende alipoulizwa kuhusu mzozo huo, alisema wanaopaswa kuzungumzia Halmashauri ya Jiji la Mbeya.

View attachment 3694339
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya, Justice Laurent Kijazi alipoulizwa kuhusu vurugu hizo, aliomba kutumiwa ujumbe, lakini hata vyo hakuujibu.
Kimsingi Bajaji wakae pembeni ila Kwa kuwa ni suala la survival hakuna atakaekubali kirahisi.
 
Bajaji na Dala Dala waachwe wote watumie ruti hizo hizo ili abiria awe huru kuchagua usafiri anaoutaka. Shida ipo wapi? Mbona Dar Bajaji na Dala Dala zinachangia ruti na amani ipo tele.
 
Wanakurupukaga tuu hao Wanaoitwa viongozi
 
Back
Top Bottom