Financial Analyst
JF-Expert Member
- Nov 27, 2017
- 1,849
- 3,506
- Thread starter
- #201
Yap mister..i wont forget.Mkuu respect una feelings sana.
Mpaka una sound track ya hizi memories.
Dah...
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yap mister..i wont forget.Mkuu respect una feelings sana.
Mpaka una sound track ya hizi memories.
Dah...
Haha dah umenikumbusha mbali pub alberto.Mawenzi advanve na umbwe advance walikuwa wanaiva sana....pub Alberto ndo yalikuwa makutano. Naomba ziku zirudi nyuma. Mguu wako tu uko town halafu kinywaji kutoka umbwe[emoji12][emoji12][emoji12][emoji12]
[emoji1787][emoji1787] mkuu hapo nilikuwa nimetembea takribani 11km kwa mguu mpk town, msosi wa mwisho ulkuwa wa jana yake jioni na misosi yenyewe mibovu mkuu! Siku 3 labda ukiwa ktk resting state[emoji1787]Mkuu unazimia kwa njaa ya siku 1 tu ? Dah kweny harakati za kibandidu watu tunakaa siku 3 hatujagusa ktu had ukinywa maji unaskia utumbo unavyouma
Naikumbuka,japo haikuwa na impact kama hiyo fujo ya 2009Umesahau ile fujo ya mwaka 2003 mlipokuja mpirani pale Umbwe mzee.?
Before vurugu hizo, umbwe kulikuwa na viti vya ushindi ambavyo vilichukuliwa lyamungo miaka ya nyuma kwenye vurugu zingine, hii ilikuwa inahamasisha sana na vijana wa umbwe tulijiona kina Rambo,Leo nimeamka na kuwaza kwa machungu sana na maumivu moyoni nikikumbuka vurugu zilizotokea kati ya shule niliyokuwa nasoma Umbwe Sec na Lyamungo Sec 2009, vurugu zilizoacha vifo, majeraha na uharibifu. Shule mbili zilizopo katika wilaya mbili tofauti (Moshi Vijijini na Hai), zilizopo katika jamii mbili tofauti za wachaga zilizokuwa na mgogoro miaka ya nyuma (Wakibosho na Wamachame), Umbwe sec ikiwa na idadi kubwa ya vijana kutoka Arusha, Kilimanjaro, Singida, Manyara, kanda ya juu kusini, kanda ya ziwa kwa uchache ...Wakati Lyamungo ikiwa na idadi kubwa ya vijana kutoka Mara, mikoa mengine ya kanda ya ziwa, Arusha, Manyara Kilimajaro kwa uchache
Mzozo ulianza Umbwe Sec tulipoenda kucheza mechi na Lyaskika, shule ya kata iliyopo karibu na Lyamungo. Vijana wa Lyamungo walikuja kuishangilia shule ya lyaskika, wakiwa kwa uchache, kulianza mvutano wa maneno kati ya vijana Lyamungo na Umbwe. Kutokana na wingi wao, Vijana wa Umbwe waliweza kuwapelekesha vijana wa Lyamungo. Vijana wa Lyamungo waka-organize na kurudi shuleni kwao ambapo walienda kuwakusanya wenzao waliobaki shuleni na kurudi uwanjani wakiwa na mafyekeo, fimbo..etc. Walikuja kwa kwasi sana wakiwa na silaha. Hii ilwapelekea vijana wa Umbwe kukimbia hoe hae, wengine kwenye mashamba ya mahindi na coffee. Wachache waliweza kufikiana na kuanza kupigana huku vijana wa Lyamungo wakiwa na advantage kutokana na silaha zao. Katika harakati za mapigamo, kijana mmoja wa Lyamongo alizungushiwa waya ya senyenge shingoni na vijana wa Umbwe na kuivutia shingoni hadi ikatoka na nyama za shingoni.
Vijana wa Umbwe kwa kukimbia waliweza kurudi shuleni, tukiwa katika jaziba na hofu kuwa vijana wa Lyamungo wanaweza kurudi, wale ma-brother wakubwa walitupangia mawindo ya usiku kwa makundi kila kona ya shule. Na story kubwa iliyokuwepo ni kuwa ikifika asubuhi na mapema tunatakiwa kwenda kuwavamia Lyamungo shuleni kwao. Asubuhi ilifika kila mtu akiwa na silaha, tukiwa tumevalimia vitambaa vyeupe kichwani ili tutambuane na kupeane code names ili tusiweze kushambuliana kimakosa. Tukaanza safari, nakumbuka tulipita sehemu na mama mmoja alikuwa akipalilia shambani akaanza kulia na kutuomba tusiende ila vijana hatukuelewa tukazidi kwenda.
Tulipofika shuleni Lyamungo tukaingia kwa kasi sana na kuanza kuwashambulia vijana wa Lyamungo na kuharibu miundombinu yao. Nakumbuka kuna jamaa alikuwa akitumia kombeo alimlenga kichwani jamaa mmoja aiyekuwa ana piga mswaki dirishani. Tulifanya shambulizi kwa kasi sana na kurudi shuleni ambapo tulikuta polisi wameshafika shuleni Umbwe na tukakalishwa chini wote. Bila mategemeo wala kudhania, tukapata taarifa kuwa kuna mwanafunzi mwenzetu amefariki kutokana na kupigwa na wanafunzi wa Lyamungo. Maan, my whole world collapsed....baada ya siku kadhaa pia tukapata taarifa kuwa yule mwanafunzi wa Lyamungo aliyezungushiwa waya ya senyenge shingoni amefariki dunia.
Zile nyakati ni moja ya kati vitu vigumu vilivyowahi kutokea maishani mwangu. Nikikumbuka jinsi yule mama wa yule kijana aliyefariki alivyofika shuleni na kuanza kuangua kilio pale administration block, huwa naumia sana. Nikimfikiria kijana wa lyamungo aliyezungushia senyenge na baadae kufariki naumia pia. Nafikiria zaidi kuhusu familia zao, mategemeo waliyokuwa nayo juu yao.
12 years later, bado moyo wangu ni mzito, kama bado haukuwahi ku-experience vita usiombe iweze kutokea katika mazingira yako.
May the Lord grant us his Mercy.
Huwa napenda ku-reference hii ishu na nyimbo ya Dr Dre ft Snoop Dogg - Lil ghetto boy
Ngoja waje watuletee za Tambaza v/s Azania, na story za Jamaa wa Tambaza alietokaga Sauz akaleta teknolojia ya mabomu ya petrol. Ndio kisa cha O-Level kuvunjwa Tambaza.Chuki dhidi ya shule na shule ni mbaya sana nakumbuka kilichotokea baina ya Bishop Moshi secondary na Mboni secondary 2002 hakukutokea vifo ila vipigo vizito
Hii nilikuwepo..Lyamungo walianza kwa kuutooa mpira wa Umbwe..kuna mwamba wa Umbwe akaukamata mpira wa Lyamungo hadharani tena mpira ukiwa unaendelea na akautoboa toboaUmesahau ile fujo ya mwaka 2003 mlipokuja mpirani pale Umbwe mzee.?
Chimbo matata sana lile dah nimerudi moshi nkapachekii ila ipo siku nitaingia tenaHaha dah umenikumbusha mbali pub alberto.
Pale pub alberto, Kuna mdingi flani aliagiza aletewe demu ghafla anaona ni binti yake ndio analetwa ambae alikuwa anasoma shule flani hivi ya boarding pale moshi
Yale wote walichokaa..
Huyu jamaa (financial analyst) analeta hisia za kidada humu. Hata jana nashangaa anapanic alafu hata hatujuani. Alihadithiwa huyu hakuwepo kwenye pira.Haha
Acha kulialia na kuleta hisia kama mtoto wa kike, thus is manhood mwanaume lazma uwe na dark side katika ukuwaji wako (from boys to men) na kikubwa nikujua jinsi ya kuji control mwenyewe mbeleni, huwezi ukaishi ki slope tu kama demu eti tukio lililotokea 12 yrs ago liku hunt hadi leo, bro upo serious?
Nyie hamkuwa na umoja mkakimbia na kumuacha mwenzenu, nae alifanya mistake ilo cost maisha yake kutotii matakwa katika himaya ya watu unachotakiwa kukubali ni kwamba Lyamungo walifanye self defense
Na hiyo kusema kuna mtu alikufa lymungo halafu hakuna hata jina lake wala makumbusho take kama ilivyo kwa Ayubu ni stori za nyie kwa nyie kujifariji
Dah basi headmaster alitupiga kamba alikuwa Wandiba kutoka mara. Alikuwa mbabe ila alinyoosha mikono baada ya ile fujo alihamishwa. Ila vioo na milango ilivunjwa na Umbwe je? Ni nani aliyetoa hela ya marekebisho?kaka haya ndo yaliyosababisha vurugu zile, kusoma hizi shule ni kama kupigwa muhuri wa moto, taarifa fake, kwa vizazi vinavyobaki halafu hata viongoz wa shule hawasemi, ndo maana nasema labda vile vita vya umachame na ukibosho unahusika,,, mimi nilikua kiongoz pale hatukuchangishwa fedha zozote, taarifa zilikua zinatolewa hivyo kama kuwatuliza tuu na kuona kuna adhabu, hata sisi tuliambiwa nyie kuna fedha mmetoa na tuliambiwa hayo tukiwa kwenye kikao cha serikali ya shule na walimu..
.
.
heb niambie madogo kule na zile mori waambiwe aidha last revenge lyamungo walipigwa, au last revenge umbwe walipigwa, ndo maana hizi fujo haziishi,
Aaa wapi ni sababu ya pisi za Lyasikika yaani Umbwe walikuja kushika pisi zetu kalio huku tunaona. Ndo kilichoharibu hadi mechi haikuisha.Na ugomvi wenu ulikuwa sababu ya sisi watoto wa kibosho na weruweru.
Ni noma mkuu ila saa nyingine shetani ana nguvu. Ilibidi waletwe mashehe na wachungaji waje kutuombea.Meku damu ya mtu hutesa sana,waliohusika lazima wanapata msongo wa mawazo mpka leo hii
Kukata mkia maana yake ni kukaribishwa,wanachokifanya ni kuwaogesha wageni wote form five or form one kwenye maji ya mtaro yatokayo mlima Kilimanjaro saa sita kamili usiku,huku wakisindikizwa na kipigoNini maana ya kukata mkia mkuu??
Mzee Manase. Mzee kenge sana yule ila uboyzini akili huwa fyatu. Kuna wanafunzi walikua wanakula mke wa mpishi dah.Sure mkuu. Kuna tukio moja headmaster. Alipokelewa beg lake na mwanafunzi alafu akatembea nalo mazima . Lyamungo ilikua vituko sana, mpishi mwenyewe alikua mbabe sana ukijichanganya huna bahati,anatembea na sime maana wanafunzi hawatabiriki muda wowote wanakugeuka.
Vile viti vilirudishwaga Lyamungo mkuu.Hii story haijakamilika ....
Anywa ngoja niongezee kipande
Katika purukushani watu wakarudi shuleni (ubwe) wakafika mapaka stoo!
Stoo ikavunjwa kwamba haiwezekani watu wapigwe kizembe vile .
Kila kifaa kikatolewa wakati huo wengine wamepewa zamu ya kulinda maeneo yanayozunguka shule kwa code names .
Wadau wakasema haiwezekani kwenda Lyamungo na miguu hivyo karandinga la shule (gari ya kuni) ikawashwa kuna mwamba mmoja wa chuga akapiga gea watu wakaelekea lyamungo huku wengine wanaenda na miguu yaani ni kama hawa wa gari walikuwa watu wa backup Mlinzi alitulizwa chuma ikawashwa.
Wazee wa karandinga walipakia viti na mazaga kibao pale lyamungo ni kama walienda vitani waka teka nyara mali za wapinzani.
Lyamungo walikusanywa katikati kama mateka na kupigwa sana makofi .
Nafikiri bado baadhi ya viti vya lyamungo viko pale Umbwe karibu na dorm three au maeneo ya karibu na lab ya biology.
Hii story ni kwa mujibu wa dodoso za miaka hiyo .