Vurugu Umbwe-Lyamungo: Miaka 12 baadae

Jamaa walimuulia uwanjani karibu na bweni ka mkapa,. Niliposoma uzi huu nimejikita ninawaza mengi ila mkuu washule wa lyamungo kipindi hicho wandiba alikua mtu wa kuchochea ghasia maana ninakumbuka tulienda pale form 5 tukakuta o,lever wanapiga fimbo usiku kama nn ila wandimba alikua akituelezea komaa nyie ni wakiume. Dah ninatamani tuwasiliane na ww mtoa uzi wenda tuna fahamiana.
 
Ndiyo maana siku hizi watoto wa boarding wanawekewa mafuta ya taa kwenye chakula kwa makusudi kwa sababu inaaminika yana control hormones hizo za testosterone na adrenaline n.k kupunguza munkari.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Nikikumbuka ni ujinga tu,Tambaza vs Azania....tukapigwa suspension mwaka mzima wa mwaka uliofuata tukaripoti shule za bweni tena za huko mbali kabisa,vijana kibao walishindwa kuendelea na shule,maana shule za karibu zote zilikatazwa kupokea wanafunzi kutoka Tambaza..
 
Sure bro yule mkuu wa pale alikuwa mtu fulani hivi wa kiburi..coz hata siku ile anakuja kuongea umbwe akuongea kwa staha.

DM please
 
Tulsimuliwa tulipofika lyamungo kusoma hakika lyamungo walikuwa ni wanajeshi wanaotumia falsafa za sun tuz wa art of war
Siyo kumbu kumbu nzuri sana; Lyamungo ni Jeshi maana hata Stream zilikuwa ni J,K & T badala ya A,B& C mlizizoea kwingine.Mazoezi yake ni Infrequent Soweto na kupakia lorry TX la Mzee Murri kwenda shambani Weruweru.Watu na majembe hupakiwa gari likiwa speed 50-60 km/h without injuries.
Inafikirisha lakini!
 
Way back wakati Niko uboyizini pale mbeya mjini.

Katika mashindano ya umiseta ulizuka mzozo Kati ya camp letu na watoto wa meta .

Kuna mwamba mmoja alikuwa anajiona gangwe kwakuwa ana mbavu Nene Sasa ana akawa anajipitisha mbele ya wanaume huku kapigilia pafyuma kavaa kitozi nyangema huku analeta Maneno mbofu mbofu.

Wana walimvumilia Ila wakasanda akatoa Jamaa mmoja nae mbavu Nene Lina makonfidensi Kama yote si unajua wanyakyusa wa tukuyu .

Akamtandika na mnyororo kichwani Jamaa damu hizi
Halafu msela akawa kajificha hamjui Nani kamchabanga na mnyororo kichwani .

Akaanza panic pale anataka kupigana na asie mjua

Walimu wake wakamtuliza Ila wapi eti akataka kuwachenjia walimu [emoji1787].

Like tukio na mengine nadhani yaliwapa warning watoto wa shule zingine pale mbeya kwamba "mkienda uboyizini kuweni wapole la sivyo mtapigwa"
 
Dah aisee umenikumbusha mbali sana kipindi hicho nilikua form 3. Ila kuweka kumbukumbu vizuri hiyo ilitokea 26 May 2009 na siyo August. Na kuhusu huyo aliyezungushiwa seng'enge sidhani kama alifariki maana tungetangaziwa shuleni. Nakumbuka huyo mwanafunzi wa Umbwe aliyefariki alipigwa kama mwizi uwanja A pale. Na hiyo siku ilibidi tukeshe tukiwasubiria Umbwe waje. Dah ile siku ilikua kama jeshi sipatii picha Umbwe wangekuja usiku ule ingekuaje maana tulijiandaa kama jeshi. Tulikusanya mawe, mafyekeo na mipini. Tulijigawa magroup matatu geti kubwa, geti dogo na katikati ya uwanja. Yaana nia ilikua Umbwe wakitokea sehemu yoyote wanapigika na tulipeana signature kabisa ukiulizwa "Nyeto" unajibu "Ujinga" ukishindwa kujibu unakula kichapo maana utakua sio wa Lyamungo. Dah sitaisahau ile siku, ni stori ndefu kwa kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati tupo uboyzini kwenye school baraza,

Hoja ilitolewa na mwanafunzi,

Mwalimu wa biology atoke mbele aje athibitishe kitaam,

Kitu gani aambacho kipo kwenye mafuta ya taa Ni kwa namna gani kinaweza kucontrol hiyo mihemko

Ilishindikana,

Mwishowe uo utaratibu wa kuwekewa mafuta ya taa kwenye vyakula ukafutwa rasmi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…