Vurugu Umbwe-Lyamungo: Miaka 12 baadae

Vurugu Umbwe-Lyamungo: Miaka 12 baadae

Leo nimeamka na kuwaza kwa machungu sana na maumivu moyoni nikikumbuka vurugu zilizotokea kati ya shule niliyokuwa nasoma Umbwe Sec na Lyamungo Sec 2009, vurugu zilizoacha vifo, majeraha na uharibifu. Shule mbili zilizopo katika wilaya mbili tofauti (Moshi Vijijini na Hai), zilizopo katika jamii mbili tofauti za wachaga zilizokuwa na mgogoro miaka ya nyuma (Wakibosho na Wamachame), Umbwe sec ikiwa na idadi kubwa ya vijana kutoka Arusha, Kilimanjaro, Singida, Manyara, kanda ya juu kusini, kanda ya ziwa kwa uchache ...Wakati Lyamungo ikiwa na idadi kubwa ya vijana kutoka Mara, mikoa mengine ya kanda ya ziwa, Arusha, Manyara Kilimajaro kwa uchache

Mzozo ulianza Umbwe Sec tulipoenda kucheza mechi na Lyaskika, shule ya kata iliyopo karibu na Lyamungo. Vijana wa Lyamungo walikuja kuishangilia shule ya lyaskika, wakiwa kwa uchache, kulianza mvutano wa maneno kati ya vijana Lyamungo na Umbwe. Kutokana na wingi wao, Vijana wa Umbwe waliweza kuwapelekesha vijana wa Lyamungo. Vijana wa Lyamungo waka-organize na kurudi shuleni kwao ambapo walienda kuwakusanya wenzao waliobaki shuleni na kurudi uwanjani wakiwa na mafyekeo, fimbo..etc. Walikuja kwa kwasi sana wakiwa na silaha. Hii ilwapelekea vijana wa Umbwe kukimbia hoe hae, wengine kwenye mashamba ya mahindi na coffee. Wachache waliweza kufikiana na kuanza kupigana huku vijana wa Lyamungo wakiwa na advantage kutokana na silaha zao. Katika harakati za mapigamo, kijana mmoja wa Lyamongo alizungushiwa waya ya senyenge shingoni na vijana wa Umbwe na kuivutia shingoni hadi ikatoka na nyama za shingoni.

Vijana wa Umbwe kwa kukimbia waliweza kurudi shuleni, tukiwa katika jaziba na hofu kuwa vijana wa Lyamungo wanaweza kurudi, wale ma-brother wakubwa walitupangia mawindo ya usiku kwa makundi kila kona ya shule. Na story kubwa iliyokuwepo ni kuwa ikifika asubuhi na mapema tunatakiwa kwenda kuwavamia Lyamungo shuleni kwao. Asubuhi ilifika kila mtu akiwa na silaha, tukiwa tumevalimia vitambaa vyeupe kichwani ili tutambuane na kupeane code names ili tusiweze kushambuliana kimakosa. Tukaanza safari, nakumbuka tulipita sehemu na mama mmoja alikuwa akipalilia shambani akaanza kulia na kutuomba tusiende ila vijana hatukuelewa tukazidi kwenda.

Tulipofika shuleni Lyamungo tukaingia kwa kasi sana na kuanza kuwashambulia vijana wa Lyamungo na kuharibu miundombinu yao. Nakumbuka kuna jamaa alikuwa akitumia kombeo alimlenga kichwani jamaa mmoja aiyekuwa ana piga mswaki dirishani. Tulifanya shambulizi kwa kasi sana na kurudi shuleni ambapo tulikuta polisi wameshafika shuleni Umbwe na tukakalishwa chini wote. Bila mategemeo wala kudhania, tukapata taarifa kuwa kuna mwanafunzi mwenzetu amefariki kutokana na kupigwa na wanafunzi wa Lyamungo. Maan, my whole world collapsed....baada ya siku kadhaa pia tukapata taarifa kuwa yule mwanafunzi wa Lyamungo aliyezungushiwa waya ya senyenge shingoni amefariki dunia.

Zile nyakati ni moja ya kati vitu vigumu vilivyowahi kutokea maishani mwangu. Nikikumbuka jinsi yule mama wa yule kijana aliyefariki alivyofika shuleni na kuanza kuangua kilio pale administration block, huwa naumia sana. Nikimfikiria kijana wa lyamungo aliyezungushia senyenge na baadae kufariki naumia pia. Nafikiria zaidi kuhusu familia zao, mategemeo waliyokuwa nayo juu yao.

12 years later, bado moyo wangu ni mzito, kama bado haukuwahi ku-experience vita usiombe iweze kutokea katika mazingira yako.

May the Lord grant us his Mercy.

View attachment 1824561

Dah namkumbuka huyo jamaa alikua form 5 HGE
Uji fongo
 
....miaka ya nyuma (1980 - 1990) kilikuwa na biff kali kati ya Kibohehe Sec na Kolila Sec. Ile ilidumu kwa muda mrefu, kwani ilikuwa hata mkikutana sehemu yoyote ni kipigana tu. Kibohehe chapa yao ilikuwa kuvaa Safari Boots na Kolila walitambulisha kwa kuvaa tasbihi shingoni.
Mo Town ilipata moto sana kwa ugomvi huo uliodumu kwa muda mrefu.
Aisee huu ulikuwa ni ujinga sn. Nimemaliza Kibohehe 1983... imagine kuna siku tulienda kabisa Kiborloni tukapanda mpaka njia ya kwenda Kolila kwa lengo la fujo tu.
 
Mtiti ulinishinda kila siku kuogeshwa kwenye mfereji,nakumbuka mara ya mwisho tulilala porini na mshikaji wangu tulipokea taarifa nmapema kwamba form 5 usiku huo walikuwa wanakatwa mikia...na kweli jamaa walikatwa mikia asubuhi tulikuta jamaa wanalia...kule bweni la mkapa kuna jamaa alivunjwa kichwa alisukumwa kwenye ngazi....kuna mshkaji alikuwa anaitwa Bitoz form six walikuwa hawampendi kisa tu ana perfume nzuri walitaka kumuuwa.
Nini maana ya kukata mkia mkuu??
 
Hujafikiria juu ya Golikipa SHABANI aliyeugua mpka kufa 2008?Tuliandamana mpka kwa mkuu wa mkoa...tukasambaratishwa ktk shule za kata..mpka leo sidhani kama kuna o level pale Lyaboys
Walirudishwa, walengwa wa kufukuzwa ni Nyie HAPO, mulivyoondoka madarasa mengine form 1 ya kipindi kile wakaenda form 2 na wengine wakaja form 1. Huu ugomvi unaozungumziwa kwenye huu Uzi ni Baada ya Nyie kuondoka, hata guts za umbwe Kuja Lyamungo walizipata Baada ya Nyie kuondoka.
 
Moshi fujo za kwenye mpira ni nyingi sana na ilikuwa ni afadhali game ikapigwe neutral ground ili kuepuka vurugu
Kirima vs Sungu 2008

najua watakuepo humu
 
Tulienda kwenye mechi Msufini....Mechi haikuisha zilitokea fujo kali sana..Msufini kuna mademu wakali enzi hizo..2009 Lyamungo kama kawa tukawa tunatamba na kuingeaongea na mademu kibabe....Mpira haukuisha tukavamia kwenye lori kila sehemu chini ya gari kulikuwa na silaha...ndondo mbao visu fyekeo n.k...kiongozi alikuwa jamaa mmoja Anaitwa Juma...hakuna aliyejeruhiwa
Gari iliwashwa imapotea kama upepo
 
kulikuwa na hizi battle na ilikuwa ni balaa
1. Milambo Vs Tabora Boys
Milambo washatembeza sana kichapo kwa Tabora Boys mpaka Tabora Girls tena Tabora Girls walienda kumwaga hadi Divi.
2. Musoma Tech Vs Mara Sec
hii ilikuwa vita zaidi wa Wanchari na Wairege,wakikutana lazima kiumane
3. Tambaza Vs Azania
battle la watoto wa mjini hili
4. Musoma Day ( Morembe) Vs Songe
5. Zanaki Vs Jangwani

battle za kitaaluma
1. Mzumbe Vs KIBAHA vs Ilboru
 
Tukitaka kwendaa mbelee bwana haaa ,haa shetani atuziaa......mkemee mkemee ebwaana.....ebwanaa mkemee..
 
Mungu baba mwenyezi..bariki shule yetu..
ushushe mibaraka na matunda memaaaa..
tuwapo masomoni na kazi mbalimbali..
jina Umbwe lisifike.


Hapo mwamba unaimba huku umeweka mkono mmoja kifuani! Unakuta unaipenda shule kuliko hata Taifa.
Mti safi..show some love.
 
Back
Top Bottom