Vurugu Umbwe-Lyamungo: Miaka 12 baadae

Vurugu Umbwe-Lyamungo: Miaka 12 baadae

Lyamungo hakuna mtu aliyekua wala kujeruhiwa
Leo nimeamka na kuwaza kwa machungu sana na maumivu moyoni nikikumbuka vurugu zilizotokea kati ya shule niliyokuwa nasoma Umbwe Sec na Lyamungo Sec August 2009, vurugu zilizoacha vifo, majeraha na uharibifu. Shule mbili zilizopo katika wilaya mbili tofauti (Moshi Vijijini na Hai), zilizopo katika jamii mbili tofauti za wachaga zilizokuwa na mgogoro miaka ya nyuma (Wakibosho na Wamachame), Umbwe sec ikiwa na idadi kubwa ya vijana kutoka Arusha, Kilimanjaro, Singida, Manyara, kanda ya juu kusini, kanda ya ziwa kwa uchache ...Wakati Lyamungo ikiwa na idadi kubwa ya vijana kutoka Mara, mikoa mengine ya kanda ya ziwa, Arusha, Manyara Kilimajaro kwa uchache

Mzozo ulianza Umbwe Sec tulipoenda kucheza mechi na Lyaskika, shule ya kata iliyopo karibu na Lyamungo. Vijana wa Lyamungo walikuja kuishangilia shule ya lyaskika, wakiwa kwa uchache, kulianza mvutano wa maneno kati ya vijana Lyamungo na Umbwe. Kutokana na wingi wao, Vijana wa Umbwe waliweza kuwapelekesha vijana wa Lyamungo. Vijana wa Lyamungo waka-organize na kurudi shuleni kwao ambapo walienda kuwakusanya wenzao waliobaki shuleni na kurudi uwanjani wakiwa na mafyekeo, fimbo..etc. Walikuja kwa kwasi sana wakiwa na silaha. Hii ilwapelekea vijana wa Umbwe kukimbia hoe hae, wengine kwenye mashamba ya mahindi na coffee. Wachache waliweza kufikiana na kuanza kupigana huku vijana wa Lyamungo wakiwa na advantage kutokana na silaha zao. Katika harakati za mapigamo, kijana mmoja wa Lyamongo alizungushiwa waya ya senyenge shingoni na vijana wa Umbwe na kuivutia shingoni hadi ikatoka na nyama za shingoni.

Vijana wa Umbwe kwa kukimbia waliweza kurudi shuleni, tukiwa katika jaziba na hofu kuwa vijana wa Lyamungo wanaweza kurudi, wale ma-brother wakubwa walitupangia mawindo ya usiku kwa makundi kila kona ya shule. Na story kubwa iliyokuwepo ni kuwa ikifika asubuhi na mapema tunatakiwa kwenda kuwavamia Lyamungo shuleni kwao. Asubuhi ilifika kila mtu akiwa na silaha, tukiwa tumevalimia vitambaa vyeupe kichwani ili tutambuane na kupeane code names ili tusiweze kushambuliana kimakosa. Tukaanza safari, nakumbuka tulipita sehemu na mama mmoja alikuwa akipalilia shambani akaanza kulia na kutuomba tusiende ila vijana hatukuelewa tukazidi kwenda.

Tulipofika shuleni Lyamungo tukaingia kwa kasi sana na kuanza kuwashambulia vijana wa Lyamungo na kuharibu miundombinu yao. Nakumbuka kuna jamaa alikuwa akitumia kombeo alimlenga kichwani jamaa mmoja aiyekuwa ana piga mswaki dirishani. Tulifanya shambulizi kwa kasi sana na kurudi shuleni ambapo tulikuta polisi wameshafika shuleni Umbwe na tukakalishwa chini wote. Bila mategemeo wala kudhania, tukapata taarifa kuwa kuna mwanafunzi mwenzetu amefariki kutokana na kupigwa na wanafunzi wa Lyamungo. Maan, my whole world collapsed....baada ya siku kadhaa pia tukapata taarifa kuwa yule mwanafunzi wa Lyamungo aliyezungushiwa waya ya senyenge shingoni amefariki dunia.

Zile nyakati ni moja ya kati vitu vigumu vilivyowahi kutokea maishani mwangu. Nikikumbuka jinsi yule mama wa yule kijana aliyefariki alivyofika shuleni na kuanza kuangua kilio pale administration block, huwa naumia sana. Nikimfikiria kijana wa lyamungo aliyezungushia senyenge na baadae kufariki naumia pia. Nafikiria zaidi kuhusu familia zao, mategemeo waliyokuwa nayo juu yao.

12 years later, bado moyo wangu ni mzito, kama bado haukuwahi ku-experience vita usiombe iweze kutokea katika mazingira yako.

May the Lord grant us his Mercy.

View attachment 1824561
 
J
Jamaa wa Lyamungo walikuwa informed kuwa umbwe watakuja usiku ko walichofanya ni kujificha kweny mashamba ya kahawa wakiwa na slashers,wanafunz wa umbwe walitekwa na kuingizwa ndan ya gate na hapo ndo kichapo kilianza,yulr jamaa alieuawa alionekana ni mvuta bangi sanaa na aligoma kuchwapwa slasher ya mat..n ambayo kwa muda huo ilikuwa kama passward ya kuingia ndan ya gate ..nawahurumiwa sanaa wazaz wa jamanaa cz walimtuma akasome ila yy akawa ndo organizer wa fujo
Hii yote ni rubbish hakuna ukweli ndani yake.

Hakuna mtu aliyetekwa na kupelekwa lyamungo ndani.

Na ayubu hakuwa kiongozi wa vurugu, alikuwa mwanafunzi mpya wa form 5

Alikamatwa coz alichelewaa kutoka lyamungo
 
Hii yote ni rubbish hakuna ukweli ndani yake.

Hakuna mtu aliyetekwa na kupelekwa lyamungo ndani.

Na ayubu hakuwa kiongozi wa vurugu, alikuwa mwanafunzi mpya wa form 5

Alikamatwa coz alichelewaa kutoka lyamungo
Kucheleqa kutoka alikuwa amezuiliwa uwanjan,wenzake walikubali adhabu na kuondoka ila yy aligomesha
 
Usevya 2017 & 2018 siji sahau.

Msichukulie poa wali wa uboys unaweza ua mtu zile akili sijui tulikuwa tunawaza nn Mara ya kwanza kulala ardhini na katisheti nikiwa peku mlimani.
 
mkuu umenikumbusha mbali sana. yani enzi zile unafungulia maji ya bomba la mvua unahesabu moja mpaka tatu then unajitosa kwenye bomba la mvua, unatoka unajisugua kwanzia kichwani mpaka mguuni then unahesabu tena kujiingiza kwenye maji. Yani maji yalikuwa baridi kiasi ambacho maji huthubutu kuyachezea.
Umbwe tulikuwa na mambo yetu pale Somsom na soko la Kombo
 
mkuu umenikumbusha mbali sana. yani enzi zile unafungulia maji ya bomba la mvua unahesabu moja mpaka tatu then unajitosa kwenye bomba la mvua, unatoka unajisugua kwanzia kichwani mpaka mguuni then unahesabu tena kujiingiza kwenye maji. Yani maji yalikuwa baridi kiasi ambacho maji huthubutu kuyachezea.
Umbwe tulikuwa na mambo yetu pale Somsom na soko la Kombo
Haha ..duh mimi nilikuwa naoga tu pindi jua linapojitokeza tu..hahah
 
Haha ..duh mimi nilikuwa naoga tu pindi jua linapojitokeza tu..hahah
nakumbuka kipindi kile watu kutoka mikoa ya mbali walikuwa wanaamshana usiku kuangalia mlima kilimanjaro hasi kile kipindi walipo report shule,
Nakumbuka yale maisha ya ku double dah
Kipindi kulikuwa na ugomvi wa kidato cha sita na kidato cha tatu kisa kuangalia TV, naikumbuka sana Umbwe shule yangu ya kwanza ya uboyzin
 
nakumbuka kipindi kile watu kutoka mikoa ya mbali walikuwa wanaamshana usiku kuangalia mlima kilimanjaro hasi kile kipindi walipo report shule,
Nakumbuka yale maisha ya ku double dah
Kipindi kulikuwa na ugomvi wa kidato cha sita na kidato cha tatu kisa kuangalia TV, naikumbuka sana Umbwe shule yangu ya kwanza ya uboyzin
Wanafunzi wageni mlima ukijitokeza tu wanaandamana kuangalia wanakenua kabisa hahaha....
 
Wale Wazee wenzangu wa Umbwe nadhani code yetu PUTO FONGO mna ikumbuka. Kwa miaka 2 nilio soma Advance pale Umbwe haikuwa wahi tokea tuka maliza muhula bila defender ya polisi kuja kutuliza fujo. Kifupi Umbwe ni mti safi sana umetoa watu wazito na safi sana.
 
Niliikua mpenzi wa katizi za mama msele .wapi faridaaa 🤣🤣🤣🤣🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️🤸‍♂️🤸‍♂️🤸‍♂️🤸‍♂️🤸‍♂️
 
Ofcos nimepanic mpumbavu ww..

Sijaandika hapa kujivunia na chochote umbwe walichofanya zidi ya lyamungo..

Angalia sasa unavyozidi na ujinga wako , eti nyie mlilipa fine na sisi hatukulipa, mjinga sana wewe hauhitaji reply yoyote ile..jibu chochote unachojua ili tambua wewe ni mentally retarded..yani baada ya miaka 12 bado unachagua upande.. manina
Mnataka kuzipiga tena hapa JF?

Nyie jamaa bado mahasimu hata huku kitaa
 
Back
Top Bottom