Vurugu Umbwe-Lyamungo: Miaka 12 baadae

mlikatazwa kwenda baada ya kifo cha ayubu au kabla ya ayubu kufariki poleni it was sad indeed
 
kaka haya ndo yaliyosababisha vurugu zile, kusoma hizi shule ni kama kupigwa muhuri wa moto, taarifa fake, kwa vizazi vinavyobaki halafu hata viongoz wa shule hawasemi, ndo maana nasema labda vile vita vya umachame na ukibosho unahusika,,, mimi nilikua kiongoz pale hatukuchangishwa fedha zozote, taarifa zilikua zinatolewa hivyo kama kuwatuliza tuu na kuona kuna adhabu, hata sisi tuliambiwa nyie kuna fedha mmetoa na tuliambiwa hayo tukiwa kwenye kikao cha serikali ya shule na walimu..
.
.
heb niambie madogo kule na zile mori waambiwe aidha last revenge lyamungo walipigwa, au last revenge umbwe walipigwa, ndo maana hizi fujo haziishi,
 
ni kweli, kwa umbwe ni zile bangi za Arusha, kuna jamaa alikua na beto kama jambazi, zile za kubonyeza ina fyatuka, mshkaji akitoka prepo usiku anaitoa alafu anaifyatua, fyaah!
.
.
ila lyamungo ni ukurya na mr. wandiba, kwakweli, kwenye vikao vya shule mzee yule kama vile alikua anaenjoy zile, ila lyimo walau alikua anatimua timua,
 
Na ugomvi wenu ulikuwa sababu ya sisi watoto wa kibosho na weruweru.
 
Mkuu respect una feelings sana.
Mpaka una sound track ya hizi memories.
Dah...
 
Ha ha ha Vita ya Box 2 na Ruhuwiko ilikua mbaya maana jamaa walikua mpka wanasaidiwa na walimu wao wanajeshi...

Ilikua kikinuka ile njia ya kwenda Tunduru usikatishe maana Boys wanajaa njia yote....
 
Na ugomvi wenu ulikuwa sababu ya sisi watoto wa kibosho na weruweru.
Toa ujinga hapa..sisi tugombee nyie Weruweru au Kibosho girls? Kwanza mlikua mnanuka Midomo na mauniform yenu! Kitu ilikua ni Machame girls..unajua kitu kinaitwa UMACHA? UMBWE MACHAME.
Mgogoro wa Umbwe na Lyamungo ni wa kurithi..na sio sababu ya wanawake
 
Nyuzi kama hizi ndo zinatofautisha JF na platform nyingine uchwara kama Instagram na Facebook..

Mafuta ya taa yanatumiwa sana nowdays tuliza munkari kwa vijana lakini bado..mfano hao Lyamungo mwaka jana walitimuliwa wote baada ya kugoma, na wakarudishwa baada ya mwezi mmoja.
 
I can feel it mzee..Waziri alifika?
 
Kipindi Cha makange (Mungu amlaze mahali pema peponi) umbwe ilifika hatua tukaiita college kulikua na ufree uliopitiliza, migomo isiyoisha, walikua kupigwa ilikua ni mwendo wa uharamia, watu mda wowote wanaenda kulewa mpaka wanazima wanaletwa shuleni hawajielewi

Kipindi hicho form one mpaka six sare moja ya kaki ukija mgeni ukikaa vibaya unaingizwa mjini sababu huwezi tofautisha uyu ni form one au form four
 
Sio tu mwaka Jana lyamungo form three na form four ya 2008 walitimuliwa wote walikua ni wakorofi sana, kwa hiyo 2008 na 2009 hawakua na matokeo ya kidato Cha nne
 
Sio kukimbia na kumwacha Ile ilikua ni ambush na jamaa alikua anaumwa na pumu ikambana ndo kilichomkuta

Waliattack na wakakimbia kumbuka walikua ugenin kulikua hakuna mda wa kupoteza
 
Tatizo idadi ya wanafunzi, wakati tunasoma Kuna wanafunzi kama 2000, munalala wanafunzi wawili kitanda cha futi 2 na nusu, matundu ya vyoo hata 10 hayafiki Maputo huko. Kula chakula vurugu, prepo vurugu, darasani vurugu, kwenye mpira vurugu, kila sehemu vurugu.

Vyoo vya mabweni vya kisasa vina space unakuta vimefungwa na wababe wanaishi huko, Dorm leader na marafiki zake.

Just imagine mamia ya wanafunzi wanakaa kwenye bwalo la shule Wana Angalia Ngono, hizo guts wanazitoa wapi? Viongozi wenyewe wa shule wanachaguliwa kwa kuangalia nguvu na influence, wengi nguvu nyingi kichwani sifuri. Unakuta mtu ana miaka kama 20 ama 30 hivi yupo form 1, hajielewi hata kidogo.
 
Mimi Advance nimesoma mixture (girls+boys) na idadi ilikuwa ya wanafunzi haikuwa kubwa..ilikuwa ni nadra sana kuona hata watu wakigombana..

So naungana na wewe idadi kubwa ya wanafunzi ni chanzo kimojawapo cha mavurugu na migomo kwenye hizi shule.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…