Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Juzi katika kikao cha bunge, Spika wa Bunge, Mhe. Anne Maklnda, alimtaja Mbunge wa Singida, Mhe. Tundu kama ndie Mbunge anayeongoza kuwa chanzo cha vurugu za bungeni, kwa kuongoza kwa utovu wa nidhamu, kuleta fujo na vurugu mbalimbali za bungeni, hali ambayo sio tuu inahatarisha hali ya usalama, utulivu na amani bungeni, bali pia kumevuruga hadi baadhi ya ratiba za Bunge kulikopelekea Spika kufuta ratiba za Bunge ambazo zilikwisha ridhiwa na kuingizwa kwenye Order Paper ikiwemo kupokea hoja binafsi za wabunge, kwa kilichoelezwa kuepuka vurugu zaidi!.
Jana kikao cha kamati ya Uongozi kimekaa kujadili hali ya usalama Bungeni na matokeo yake, tutayapata kesho asubuhi baada ya kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo kwa PM!, ni hakika rungu la kiti, lazima litamshukia Mhe. Tundu Lissu!.
Swali la kwanza ambalo wengi mtapenda kujiuliza ni, ni jee ni kweli, Mhe. Tundu ni mtundu na ndie chanzo cha utovu wote wa nidhamu wa bunge hili la kumi kama anavyoelezwa na Madam Speaker?!, au huo utundu wa Mhe. Tundu, sio utundu bali ni kusimamia haki na uzingatiaji wa kanuni za uendeshaji wa Bunge kwa haki, kufuatia Madam Speaker kuonyesha udhaifu mkubwa katika kuliendesha Bunge kwa kutokuzingatia, sheria, taratibu na Kanuni?!.
Kwa vile mimi ni mmoja wa watu tunaomfahamu vizuri Mhe. Tundu, tangu zamani tukiwa shuleni, Ilboru (sio darasa moja, mimi nikiwa A-level, yeye alikuwa O-Level) naomba kuchukua fursa hii kumfariji Mhe. Spika, kwa kumshauri na kumuomba asiumize sana kichwa chake kuendelea kubishana na Mhe. Tundu Lissu kuhusu kanuni za Bunge, ni kujipotezea tuu muda wake bure kwa kubishana na Lissu kwa kitu ambacho Lissu ana uhakika nacho 100/100!. Nashauri wala Bunge wasipoteze muda na kujisumbua kumuadhibu kwa jambo ambalo liko wazi kabisa watu wote wenye macho tunduizi tunaona wazi ni wapi udhaifu wa uendeshaji wa Bunge letu ulipo, sababu za udhaifu huo zinajulikana tangu chanzo chake, ulipo sasa na labda utaendelea kuwepo, hivyo hata Lissu akiadhibiwa vipi, kwa sababu Mhe. huyu ni mbishi hakuna mfano!, haswa pale anapokuwa na uhakika kuwa yuko right!.
Nashauri Mhe. Spika, lazima ufike mahali, umkubali huyu jamaa hivyo hivyo jinsi alivyo na lile jina lake la Tundu, sio jina tuu la kupewa, bali huyu bwana analiishi jina lake kwa kuwa ni mtundu kweli!, na haswa pale anapogundua kuwa katiba, sheria, taratibu na kanuni zinakiukwa na zinapopindishwa ili kufavour na kutoa mteremko kwa upande fulani mule Bungeni.
Nimebahatika kusoma na Mhe. Lissu shule moja kule Ilboru, (sio darasa moja) miaka hiyo enzi za Mkuu mmoja wa shule aitwae Mwalimu Mushi, kwa jina la utani, tulimuita Bino!. Huyu Bino alikuwa ni Mwalimu Mkuu bingwa wa nidhamu, ila kwa Tundu Lissu, alinyanyua mikono juu na kisha kuishusha chini, baada ya kuthibitika kuwa japo Tundu Lissu shuleni alikuwa "toto tundu", ila pia ndie aliyekuwa kipanga wa darasa lake!, kwani pepa alikuwa akizifumua, utadhani mtihani katunga yeye!.
Tundu Lissu alijiunga shule ya vipaji ya Ilboru akitokea Singida, wakati huo shuleni akiitwa Antipasi Tundu, na alikuwa ni mtoto mtundu kweli!. Wakati huo, O-Level ya Ilboru ilichukua wanafunz vichwa tupu wenyeji wa Arusha, Singida na Shinyanga!. Sisi Wasukuma tukiitwa "Wasukusu", wenyeji wakiitwa "wamenye" huku jamaa wa Singida wakijiita watu wa "Singapore", A-Level wakichukua vipanga wenye Div 1 kali, enzo hizo uji ukiitwa "sumu", na nje kulikuwa na kaduka kwa "Akwii".
Utundu wa Tundu Lissu ulkikuwa ni kwenye mishe mishe tuu hizi za zile, haijulikani alikuwa akisoma muda gani, ila pepa zikija, anafumua ile mbaya kama mitihani katunga yeye!, hivyo huyu jamaa ni kichwa, very bright and na very intelligent upstairs!.
Moja ya maeneo ambayo Tundu Lissu alikuwa ni mtundu au tusema ni mbishi, ni kwenye school debate!. Tundu Lissu alikuwa Bingwa wa school debate, akishakuwa na uhakika yuko right and on the right side and on the right track, ni mbishi hakuna mfano!.
Hata mimi nami sikuwa malaika, nilikuwa na matatizo yangu tangu shule, yale matatizo ya kawaida ya watu wa Kanda ya Ziwa, sisi Wasukuma wa Chapa Ng'ombe, tukiongoza, unapokutana bidhaa adimu za kumwaga!, vile vibinti vya vyeupe vya Kiarusha pale Mlimani Ilboru, ukigusa tuu...!, ukijumlisha na lile baridi kali la Ilboru , tena wakati huo, "bwawa bado halijaingia luba!'...
Tundu Lissu aliondoka Ilboru na Div. 1 kali ya point 7!, akaenda Galanos huko nako akafumua Div. 1 ya point 3!, na hatimaye kujiunga UDSM alikofumua upper 2nd Class (inasemekana alipata 1st class Ila wakambania). Sisi na vilaza wengine tukaishia kwenye vile vyuo vya mashenzini!.
Tulipoteana kwa kipindi cha takriban miaka 10!, tulikuja kukutana tena jijini Atlanta, nchini Marekani, yeye akiwa na yake nami nikiwa na yangu, ndipo akanieleza sasa yuko LEAT, na huko aliichachafya serikali vivyo hivyo kama anavyo mchachafya Madame Spika, kwa kumsulubu bila huruma!.
Pamoja na utundu wote huu wa Mhe. Tundu Lissu, kiukweli kabisa this guy is dam good upstairs tangu academically akiwa shule na kwa kujenga hoja akiwa wakili na hadi sasa mule Bungeni.
Hivyo wakati tukisubiria kusikia ni adhabu gani itamfika Lissu hapo kesho, kuna maswali matatu tujiulize!.
Paskali
(Skulu Meti wa Toto T).

- Jee ni kweli Mhe. Tundu Lissu ni mtundu kihivyo na ndie mbunge anayeongoza kwa utovu wa nidhamu hadi kustahili adhabu kali?.
- Au ni Spika ndiye Spika dhaifu hadi kushindwa kulisimamia Bunge kwa kanuni, kuliendesha Bunge kwa haki hivyo Tundu Lissu akisisitiza kufuatwa kwa Sheria taratibu na kanuni, anaonekana kama analeta vurugu?.
- Baada ya kuthibitisha, Mhe. Tundu Lissu alikuwa ni mtundu toka shuleni, jee nani wa kubadilika kati ya Mhe Tundu Lissu na wabunge wa upinzani, yaani wakae kimya wakati sheria, taratibu na kanuni za Bunge, zikikiukwa, na kupindishwa?,
- Au Mhe. Spika ndie abadilike na kukuendeshea Bunge kwa mujibu wa kanuni na sio kujiendeshea Bunge kwa kuliburuza atakavyo, ili tuu kudumisha utii, na nidhamu ili Bunge liwe la amani?,
- My Take: It's about time, wakuu wa Bunge ndio wabadilike baada ya kugundua mule Bungeni wameingia wabunge vichwa makini wanaojua katiba, sheria, taratibu na kanuni, hivyo sio watu wa kupelekwa pelekwa!. Huwezi kuwaburuza kibwege bwege, hivyo lazima wabadilike na waliendeshe Bunge kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni kwa kutoa haki na usawa kwa wote, kwa vyama vyote, hivyo kupatikana kwa amani ya kweli ya kudumu mule Bungeni.
- Akifanya hivyo Mhe Madam Spika, atawathibitishia Watanzania kuwa hata yeye, japo ni Spika wa majaribio ya "jinsia" ,"ameweza" kuliendesha Bunge vizuri tuu, ambalo ni mhimili mmoja wa dola, hivyo 2015, hivyo kuuthibisha wanawake wakiwezeshwa, wanaweza, hivyo tunaweza kuendelea na majaribio ya "jinsia" kwa mihimili miwili iliyobakia, ili nchi yetu iwe ni nchi ya usawa halisi wa kijinsia.
Paskali
(Skulu Meti wa Toto T).