Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Je Makinda naye ni Kinda bado katika uendeshaji wa shughuli za Bunge ?
walimfanyia fitna sitta, sasa kamasi inawatoka, sitta alikua anajitahidi sana ku-balance mijadala, na sheria na kanuni anazijua kwelikweli, haya mazezeta mawili yalipewa uspika for a reason, to serve their masters, hata mimi nisingekubali hoja muhimu kama ya mnyika kuhusu maji zezeta ndugai linakataa tu lenyewe, kazi yake kuibana serikali, anajisahau yeye anakua part ya serikali, kwanini wapinzani wasikasirike kwa usenge kama huo?
let them reap what they sow,
ningependa zichapike siku moja bungeni, tena waanze na makinda au ndugai
Mh. Tundu Lisu ananikumbusha mbali! Mwaka 1961 tukiingia Form 1, haikuchukua muda darasa letu, pamoja na kuwa vinyoya, likajulikana kama "siasa kali" (wakati huo hatujapata uhuru). Bahati mbaya wengi wa vipanga darasani walilazimika kuchukua masomo ya sayansi kwani huo uhuru wa kuchagua haukuwapo sana. Nina hakika mtu kama Tundu Lisu, angesoma wakati huo, labda siasa angeisikia tu kwa mbali...sana sana angeishia kuwa Injinia au dakitari! Linalosikitisha ni kuwa wengi wa viongozi wa baadaye kutoka kundi letu (Wabunge na Mawaziri) ni wale ambao somo la "additional & applied mathematics" walikaa nao mbali kama ukoma. Kweli mambo yalikuja kubadilika!
Ni kweli Tindu Lissu ana kipande cha lawama katika hili, lakini ukiangalia kwa undani, tatizo ni baadhi ya wabunge kuingia kwenye mob mentality na deindividuation kuchukua nafasi huku wakiamini hakuna adhabu itakayotolewa kwa sababu inavyoonekana wanaamini kila lile alifanyalo Mh. Tindu Lissu ni kweli.
Ukiangalia video ya bunge la siku tatu zilizopita, baada ya Tindu Lissu kuanza kugonga meza na kuimba, Mh. Msigwa naye papo hapo akaungana naye na wengine wakafuatia.
Cha kushangaza, Naibu spika (Mh. Ndugai) ambaye ndiye alishiriki katika uandishi na utengenezaji wa kanuni za bunge, inafikia sehemu anashindwa hata kujua ni kanuni ipi inasimamia lipi kama ilivyoonekana siku tatu zilizopita alipokuwa akihangaika kuuliza kanuni kwa wasaidizi wake pembeni. Hii nayo inajenga picha kwa wabunge kama spika na naibu kile wakifanyacho wala hakieleweki.
Nashindwa kuelewa, kwa nini watu wanalinganisha bunge la kipindi cha Mh. Sitta na la sasa na wanaona utendaji wa Mh. Sitta ulikuwa mzuri wakati tofauti zake ziko wazi kabisa ambazo ni nje ya utendaji mahiri wa spika bali ni idadi, aina ya wabunge na utendaji wa serikali bungeni. Kipindi cha Mh. Sitta, hakukuwepo na Mh. Lissu, Mh. msigwa, Mh. Nasari n.k
Kwa majumuisho, lawama ziko pande zote, ila mwanzilishi mara nyingi wa mabishano ya kanuni (Mh. Lissu) ndiyo anaonekana kwa macho ya Watanzania kama analeta vurugu kwa vile wananchi hawajawa na mazoea ya kuona bunge makini la vyama vingi ( No More Rubber-Stamp)
Je Makinda naye ni Kinda bado katika uendeshaji wa shughuli za Bunge ?
Wanamuonea madam speaker makinda,Je Makinda naye ni Kinda bado katika uendeshaji wa shughuli za Bunge ?
JK alishawahi kusema kuwa "Ni afadhali Slaa awe Rais lakini sio Tundu Lissu awe Mbunge(sio Rais)"
Kumbe alishasoma alama za nyakati kitaambo.